Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel amezitaka taasisi zilizo chini ya Sekta ya Mifugo kuhakikisha wanatumia Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE).
Prof. Gabriel aliyasema hayo Septemba
2, 2020 alipokuwa akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji
Serikalini yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini
Dodoma.
akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Prof. Gabriel aliwataka
kuhakikisha wanautumia mfumo huo kwa kuwa utasaidia kuongeza makusanyo ya
mapato, utarahisisha ulipaji wa fedha pamoja na kutunza kumbukumbu za matumizi
ya fedha.
“Kwa kutumia mifumo ya TEHAMA
sisi Wizara ya Mifugo kupitia minada tu tumeweza kuongoza ukusanyaji wa mapato
mfano mmoja ya mnada uliopo kanda ya Ziwa tulikuwa tukikusanya sh. 720,000 kwa
siku lakini baada ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA tunakusanya 7,500,000 kwa
siku,” alisema Prof. Gabriel.
Pia aliwasisitiza washiriki
kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa zinaingizwa kwenye mfumo kabla ya
kutumika kwani kwa kutofanya hivyo watakuwa wamekiuka taratibu.
Vilevile ameipongeza Wizara
ya Fedha na Mipango kwa kuendelea kuwatumia wataalam wa ndani kubuni mifumo
mbalimbali ya ukusanyaji mapato pamoja na udhibiti wa matumizi ya mapato hayo.
Naye Mkuu wa Kitengo cha
TEHAMA, Bw. Tazari Kibola amesema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kujua
namna ya kutumia mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) utakaosaidia kuongeza
ukusanyaji wa mapato na udhibiti wake katika taasisi zao.
Pia amesema kuwa baada ya
mafunzo hayo watakwenda katika taasisi hizo kuona kama kuna mapungufu ya mahitaji
yanayohitajika ili mfumo huo uanze kutumika.
Akimshukuru Katibu Mkuu kwa
niaba ya washiriki wa mafunzo, Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo
Tanzania (TALIRI), Bw. Dennis Samangwa Ndabiriwe amesema kupitia mafunzo hayo na
mfumo utakapoanza kutumika utawasaidia kuongeza mapato, hivyo watakwenda
kuainisha mahitaji ya mfumo na kuhakikisha wanaanza kuutumia.
Mafunzo hayo yamewahusisha Wahasibu, Meneja wa Fedha, Wataalam wa Manunuzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Bajeti kutoka taasisi za Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Bodi ya Nyama, na Bodi ya Maziwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na washiriki wa
mafunzo (hawapo pichani) kutoka katika Taasisi zilizopo chini ya Wizara Sekta
ya Mifugo wanaopatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE)
yanayotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango. Mafunzo haya yanafanyika katika
ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma. (02.09.2020)
Mhasibu
Mkuu wa TALIRI, Bw. Dennis Samangwa Ndabiriwe akitoa
neno la Shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof.
Elisante Ole Gabriel baada ya kuzungumza na washiriki wa mafunzo kutoka katika
Taasisi zilizopo chini ya Wizara Sekta ya Mifugo wanaopatiwa mafunzo ya Mfumo
wa Ulipaji Serikalini (MUSE). Mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma. (02.09.2020)
Picha ya pamoja ya Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel na Washiriki
kutoka LITA wanaopatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE). Aliyekaa
kushoto ni Ahmed Ndee kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kulia ni Mkuu wa
Kitengo cha TEHAMA (WMUV) Mifugo, Tazari Kibola. Mafunzo haya yanafanyika
katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma. (02.09.2020)
Picha ya pamoja ya Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel na
Washiriki kutoka Bodi ya Nyama wanaopatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji
Serikalini (MUSE). Aliyekaa kushoto ni Ahmed Ndee kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA (WMUV) Mifugo, Tazari Kibola. Mafunzo
haya yanafanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma.
(02.09.2020)
Picha ya pamoja ya Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel na
Washiriki kutoka Bodi ya Maziwa wanaopatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji
Serikalini (MUSE). Aliyekaa kushoto ni Ahmed Ndee kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA (WMUV) Mifugo, Tazari Kibola. Mafunzo
haya yanafanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma.
(02.09.2020)
Picha ya pamoja ya Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel na Washiriki
kutoka TVLA wanaopatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE). Aliyekaa
kushoto ni Ahmed Ndee kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kulia ni Mkuu wa
Kitengo cha TEHAMA (WMUV) Mifugo, Tazari Kibola. Mafunzo haya yanafanyika katika
ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma. (02.09.2020)
Picha ya pamoja ya Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel na Washiriki
kutoka NARCO wanaopatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE). Aliyekaa
kushoto ni Ahmed Ndee kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kulia ni Mkuu wa
Kitengo cha TEHAMA (WMUV) Mifugo, Tazari Kibola. Mafunzo haya yanafanyika
katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma. (02.09.2020)
Picha ya pamoja ya Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel na
Washiriki Wanawake kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara Sekta ya Mifugo
wanaopatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE). Aliyekaa kushoto ni Ahmed
Ndee kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA
(WMUV) Mifugo, Tazari Kibola. Mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa Ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi jijini Dodoma. (02.09.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini kutoka Wizara ya Fedha na Mipango. Kulia kwake ni Suleiman Nassoro na Ahmed Ndee na upande wa kulia ni Kizito Mpeka akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Tazari Kibola. (02.09.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na
wawezeshaji wa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango. Kulia kwake ni Suleiman Nassoro na Ahmed Ndee na upande wa kulia ni
Kizito Mpeka akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Wizara ya Mifugo na Uvuvi
(Mifugo), Tazari Kibola. (02.09.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni