WAZIRI LUHAGA MPINA AMEWATAKA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA KUCHINJA PUNDA NCHINI KUPANDISHA BEI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewataka wawekezaji wa viwanda vya kuchinja Punda nchini kupandisha bei ya kununua wanyama hao badala ya shilingi laki mbili ya sasa kwa punda mmoja ili kudhibiti utoroshaji wa mifugo nje ya nchi ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya mifugo elfu kumi inatoroshwa mipakani kwa siku kwenda nje ya nchi inakonunuliwa kwa bei ya juu. Akizungumza leo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika Kiwanda cha Punda cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma alichokifungua hivi karibuni, Waziri Mpina alisema bei hiyo haiendani na gharama halisi ya ufugaji wa Punda hali inayowafanya wafugaji kuwatorosha mifugo na kulikosesha taifa mapato makubwa. Alisema ili punda aweze kufikia hatua ya kuchinjwa inachukua kiasi cha miaka miwili ambapo gharama zake za ufugaji zinakuwa juu ukilinganisha na bei ya s...