IDARA
YA UKUZAJI VIUMBE KWENYE MAJI
Idara ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji ina jukumu la
kuratibu mazingira rafiki ya uwekezaji kwa kutoa miongozo mbalimbali kutegemea
na aina za uwekezaji. Taratibu za uwekezaji zitafuata miongozo na taratibu
zilizopo kulingana na viwango vilivyopo nchini na kimataifa pamoja na
kuzingatia hifadhi ya mazingira na uendelezaji wa rasilimali za uvuvi
(Fisheries Investment Guidelines and The
Environmental management Act).
1.0 Mchango wa Idara ya Ukuzaji
Viumbe kwenye Maji katika uwekezaji
Idara ina
wajibu wa kutoa ushauri juu ya mambo mbalimbali katika uwekezaji ambayo ni
pamoja na;
- Taratibu za
kufuata kabla ya uwekezaji;
- Sheria
zilizopo;
- Eneo linalofaa kwa uwekezaji;
- Aina
ya viumbe wanaofaa kufugwa/kulimwa kwa kufuata kanuni za .uvuvi na
"FAO code of conduct for transfer of species" (1988); na
- Teknolojia
sahihi ambazo hazina athari kwa mazingira, zinazofaa kiuchumi na zinazokubalika
katika jamii
2.0 Sekta au taasisi zingine za
kupata taarifa na ushauri juu ya uwekezaji
Uwekezaji katika ukuzaji viumbe kwenye maji unajumuisha sekta na taasisi
nyingi kutegemea na mradi au uwekezaji husika
kama:
1. Idara ya
misitu- kuangalia athari katika misitu hasa jamii ya mikoko na misitu mingine
2. Idara ya wanyamapori (athari katika hifadhi za
wanyama)
3. Idara ya malikale kuangalia athari katika kumbukumbu
na tamaduni zilizohifadhiwa (culture and archeologicals)
4. Sekta
ya mazingira (NEMC) –tathmini ya athari
za mazingira (EIA)
5. Kituo
cha uwekezaji (TIC) – kupata leseni za
biashara ,ardhi kwa ajili ya biashara na motisha kwa ajili ya biashara kwa
wawekezaji kwenye miradi mikubwa Mamlaka ya bandari (TPA) – tahadhari ya mwingiliano
wa maeneo na usalama wa maji
6. Idara ya ardhi
– upatikanaji wa hati miliki za ardhi
7. Serikali za mitaa – upatikanaji wa eneo pamoja na sheria
ndogo zilizopo.
8. Mamlaka ya maji – kibali cha kutumia maji.
9. Idara ya masoko - kupata taarifa za masoko
10. Taasisi za utafiti – kupata taarifa zilizofanyiwa tafiti
husika
3.0 Taratibu za kupata vibali na leseni za mazao
yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji
Vibali na leseni zote za mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji zinatolewa na Mkurugenzi wa Idara ya
Ukuzaji Viumbe kwenye Maji, chini ya Sheria ya uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni za uvuvi za mwaka 2009; kama ifuatavyo:-
• Leseni za biashara ya kuuza mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye
maji. Utolewaji wa leseni hizi umegawanywa katika sehemu kuu mbili (2)
Sehemu ya kwanza
- Leseni zinazotolewa na Serikali za Mitaa (Local
Government). Leseni hizo ni kama ifuatavyo.-
- Leseni za biashara ya kuuza mazao yatokanayo na
viumbe wanaokuzwa kwenye maji ndani ya nchi,
Sehemu ya Pili
Leseni zinazotolewa na Serikali Kuu (Central
Government licence). Leseni hizo ni:
- leseni za kusafirisha nje ya nchi mazao yatokanayo
na viumbe wanaokuzwa kwenye maji
- Leseni za
kuingiza nchini mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji (kutoka nchi za nje) ikiwa ni
mpango na vibali vitatu vya:
(i) Kusafirisha nje ya nchi samaki hai kama; Kaa, Kamba
koche, Samaki wa mapambo, Mwani na mazao mengine ya viumbe wakuzwao kwenye maji
(ii) Kuingiza samaki hai ambao hawana asili ya Tanzania kama ;
Blue gill sun fin (Catollioperca
marcothira), "Chinese carps" na jamii nyingine
(iii) Kuingiza
nchini samaki au mazao yatokanayo na ukuzaji viumbe kwenye maji (Aquaculture
products)
·
Pia wizara hutoa Leseni maalum kwa ajili ya
usafirishaji wa mazao ya Ukuzaji viumbe kwenye maji kwa muda maalum kwa sababu
za:
1. Utafiti
2. Matumizi ya nyumbani (chini ya kilo 7) na
3. Mafunzo
Mahitaji
muhimu kwa raia wa Tanzania;-
1. Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa ukuzaji viumbe
kwenye maji Wilaya au Manispaa,
2. Leseni hai ya kukusanya mazao yatokanayo na viumbe
wanaokuzwa kwenye maji iliyotolewa na Wilaya au Manispaa
3. Formu ya maombi ya leseni ya biashara ya mazao yatokanayo
na viumbe wanaokuzwa kwenye maji
4. Leseni
ya Biashara inayotolewa chini ya Sheria ya kutoa leseni za Biashara (Business
Licensing Act),
5. Namba
ya utambulisho ya kulipa kodi (Tax Identification Number)
6. Uthibitisho
wa uraia (hati ya kusafiria au cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha utaifa )
wa mmiliki/wamiliki wa kampuni,
7. Cheti
cha kuandikishwa kilichotolewa kwenye kumbukumbu (Certificate of Registration
and Extract from Register), or
8. Hati ya makubaliano na hati
ya ubia (Memorandum of Understanding and Articles of Associations), na
9. Cheti cha ushiriki
(Certificate of Incorporation)
Nyaraka zinazohitajika katika
kupata leseni kwa asiye raia ni pamoja na;-
- Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Uvuvi/ Ukuzaji
viumbe kwenye maji wa Wilaya au Manispaa,
- Uthibitisho
wa uraia (cheti eha kuzaliwa au hati ya kusafiria "passport"),
- Kibali halali cha kufanya kazi nchini (valid work
permit)
- Fomu ya maombi ya leseni ya biashara ya mazao
yatonayo na ukuzaji viumbe kwenye maji,
- Leseni hai ya Biashara inayotolewa chini ya Sheria
ya kutoa leseni za Biashara (Business Licensing Act),
Wizara inazidi kuwakumbusha
wadau wote wa sekta ya uvuvi kuwa kwa mujibu wa Sheria ya uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na
Kanuni zake za mwaka 2009 "leseni zote zinafikia ukomo wake kila tarehe 31
Disemba ya kila mwaka na kuhuwishwa kwa hiyari kufikia tarehe 30 Machi ya mwaka
unaofuata zaidi ya hapo mteja atalazimika kulipa faini ya asilimia 50 (50%) ya gharama za leseni husika.
Kumbuka yapo Maelezo ya
nyongeza kwa muombaji/ waombaji ambao sio raia wa Tanzania,
• Andiko la Mradi na
uwezekano wa mradi kutekelezwa (Project write up & feasibility study) Taarifa ya tathmini ya athari za Mazingira (EIA
report).
* Cheti kutoka taasisi ya
uwekezaji Tanzania (TIC certificate).
* Taarifa ya tathimini ya
athari za kimazingira (environment impact assessment report),
* Kibali halali cha kufanya
kazi nchini (Valid work permit) na,
* Uhakiki wa mazingira
yanayoendana na shughuli za uvuvi (A proof on the value of physical environment
relevant to fisheries activities).
Hatua
za kufuata unapotaka kuanza ufugaji wa samaki (Small scale Aquaculture
establishment)
Maombi hufanyika kwa kujaza fomu 5 na 7 (First schedule) na kibali kitatolewa
kwa fomu QA/APP/01 (First schedule)
Hatua za kufuata unapotaka
kuanza ufugaji mkubwa wa samaki (Large scale aqua farmers)
Hatua ya kwanza ni lazima mwekezaji aombe kibali cha
kufanya hivyo kwa kujaza Fomu 7 (First schedule) na baada ya ofisi kuridhika,
kibali kitatolewa kwa form QA/APP/13 (First schedule)
Mfugaji samaki
ataomba ushauri wa kitaalam katika kuchagua eneo linalofaa kwa shughuli za
ukuzaji viumbe kwenye maji kwa kuzingatia kanuni za ufugaji samaki na miongozo
yake.
Taarifa ya tathimini ya
athari za kimazingira (EIA)
itafanyika kwa uwekezaji mkubwa kwa kuhusisha taasisi za serikali zilizopewa
mamlaka ya kusimamia shughuli hizo kisheria.
Mwekezaji haruhusiwi kutumia vichochezi kama beta agonists kwa
ajili ya kuongeza ukuzaji samaki.
Mfugaji wa samaki awe na kibali cha matumizi ya maji kutoka mamlaka ya maji
husika
Mfugaji awe na hati ya kumiliki ardhi
Hatua za kufuata kwa kufuga samaki
kwenye Vizimba (Cage culture)
Mwekezaji apeleke maombi kwa Katibu Mkuu,
Maombi yafanyike kwa kujaza Form 7 (First schedule) kibali kitatolewa kwa
QA/APP/14 baada ya kufanya tathmini ya athari za mazingira na taarifa kutolewa.
(EIA ifanyike)
Uwekezaji wa Mwani (Seaweed)
Mwekezaji katika kilimo cha mwani anatakiwa:
- Apate kibali toka serikali za mitaa/Kijiji
- Atafute
eneo linalofaa
- Atumie
mbegu ambazo hazijaathirika na magonjwa
- Afuate
mwongozo wa kuendeleza kilimo cha mwani
FOMU ZINAZOTUMIKA KATIKA SHUGHULI
ZA UKUZAJI VIUMBE KWENYE MAJI
Application for a license
for fishing or dealing in fish or fishery products
(fin fish, crustaceans,
seaweed, Aquarium fish etc) - Form 3(a)
Application
for export license for fish and fish products - Form 3(c)
Application for permit to
construct / renovate /adapt a fish establishment – Form 5
Application for certificate
of transportation of fish and fish products - Form 6
Application for permit to
establish of commercial/large scale aqua farm - Form 7
Register of aqua famers –
Form 8
Evident of poisoned fish
Form – 9
Compounding offence Form –
11
Seizure Form – 12
Application for disposal of
fishery products Form – 13(a)
LICENCE
/PERMIT / CERTIFICATE
QA/APP/01 – Certificate of
approval for fish or aquaculture establishment
QA/APP/02 – Health
certificate
QA/APP/03 – Sanitary
certificate covering fish and fishery
products
QA/APP/04 – Permit for
movement of fish and fishery products
QA/APP/05 – Permit for
export of fish and fishery products
QA/APP/07 – Certificate of
ownership for fish and fishery products
QA/APP/11 – License for
fishing or dealing in fish and fishery products
QA/APP/12 – Permit for import
of fish and fishery products
QA/APP/13 – Permit for
large scale aqua farming
Dkt. C.G Mahika
DAQ