KUWASILI KWA WAZIRI MUV MHE DKT TITUS MLENGEYA KAMANI, KATIKA VIWANJA VYA TANZANIA VETERINARY LABORATORY AGENCY KITUO CHA MTWARA
|
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Ndile alimtambulisha Mhe Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Mlengeya Kamani, kwa Mwenyekiti wa Kijiji (wa pili kwenye watambulishwa) cha Naliendele na Makamu wake aliyeshikwa mkono na Waziri. Kuanzia wa tano ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI na mwenye koti jeusi ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo Naliendele . Nyuma ya Waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Eng Joseph Simakalia |
|
Mhe Waziri akisalimiana na Wafanyakazi wa Kituo cha TVLA na ZVC- Mtwara |
|
Mhe. Waziri akisalimiana na Mkuu wa ZVC - Mtwara Dkt |
|
Uzinduzi wa jengo la Utafiti Naliendele ambalo limezinduliwa na Mhe Dkt Titus Mlengeya Kamani Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi |
|
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt Yohana Budeba akitoa maelezo katika Ofisi za ZVC na TVLA - Mtwara mbele ya Waziri mwenye dhamana na wizara hiyo. |
|
Dkt Albano Mbiuzi Mkuu wa Kituo cha Kanda cha Veterinary Mtwara, akitoa Taarifa fupi ya Utendaji wa kazi kwa Mhe. Waziri mwenye dhamana na Wizara Dkt Titus Mlengeya Kamani |
|
Mhe Dkt Titus Mlengeya Kamani (Mp) akielekea kwenye Jengo la Utafiti atakalolizindua, pembeni mwa Waziri ni Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha Kilimo Naliendele na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo - Mtwara Dkt Rajabu Kirani mwenye suti nyeusi na karatasi mkononi |
|
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Eng, Joseph Simbakalia akibadiishana mawazo na mgeni wake Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe, Dkt Titus Mlengeya Kamani Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi |
|
Dkt Rashid Msangi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo - TALIRI, akitoa maelezo mafupi kabla ya kuzindua jengo kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Mlengeya Kamani (Mp) |
|
Mhe Dkt Titus Mlengeya Kamani (Mb) akifungua rasmi jengo la Utafiti wa Mifugo Naliendele tarehe 02/08/2014 |
|
Mhe Waziri akifunua kitambaa kuonyesha Kibao cha Uzinduzi huo kama ishara ya kukamilisha ufunguzi |
|
Mhe Waziri akitembela baadhi ya vyumba vilivyomo ndani ya jengo la Utafiti wa Mifugo akipewa maelezo na Dkt Dkt. Ezekiel Goromela Mkuu wa Kituo hicho (pamoja na picha zote hapo chini ) |
|
Mhe Waziri na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wakijongea meza kuu kuanza kupata maelezo ya Ujenzi na Mafanikio ya Kituo cha Utafiti cha Mifugo Mtwara |
|
Mhe Waziri akisaini Kitabu cha Wageni ikiashiria uwepo wake katika eneo husika. |
|
Kikundi cha ngoma kutoka Kijiji cha Lyamba kikitumbuiza mbele ya jengo lililozinduliwa kwa heshima ya Mhe. Waziri wa MUV |
|
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RALIRI Dkt Rashid Msangi akitoa Taarifa fupi ya TALIRI na Ujenzi wa Jengo la Utafiti Mtwara, ambalo limefadhiliwa na COSTECH pamoja na Wizara ya MUV |
|
Kikundi cha ngoma cha Lyamba kikiendelea kuburudisha Wageni rasmi na waalikwa |
|
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Hassan Mshinda ambaye Taasisi yake ndiyo imefadhili ujenzi huo akitoa Taarifa fupi kwa Mhe. Waziri |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni