WAZIRI ATEMBELEA WILAYA YA MVOMERO TAREHE 01/03/2012
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo David akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Waziri akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Matuminzi Bora ya Ardhi Dkt Maria Mashingo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero Bibi Joyce Mengele, akisoma taarifa ya Wilaya ya Mvomero. Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mvomero akiandika wakati Mkurugenzi akitoa Taarifa ya Wilaya kwa Mhe Waziri. Mhe Waziri akitaka ufafanuzi fulani kutoka kwa watendaji wa Halmashauri hiyo. Msafara wa Waziri uliwasili katika Kijiji cha Dakawa Sokoine na picha onaonyesha Baadhi ya waliongozana na Mhe waziri wakisalimia wafugaji mara walipowasili kijijini hapo. Wanakijiji wameketi huku wakimsikiliza Mkuu wa Msafara Afisa Tawala wa Wilaya, akimkaribisha Waziri na Ujumbe wake na Ujumbe wa Kijiji kusoma Risalla yao kwa Mgeni Rasmi ...