Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2025

"SITACHOKA KUWASEMEA, KUWAPAMBANIA VIJANA WA KITANZANIA" - MHE. NG'WASI

Picha
 Na, Hamisi Hussein, Singida  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  ambae pia ni Mbunge wa Kundi la Vijana kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Ng'wasi  Damas Kamani, amesema  ataendelea kulisemea, kulitetea na kulipambania kundi la vijana kupata fursa mbalimbali za kujiinua kiuchumi hususani katika sekta ya mifugo na uvuvi. Mhe. Ng'wasi  ameyasema hayo leo Desemba, 24, 2025, Wilayani Iramba Mkoani Singida, alipomwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba katika Kikao cha Baraza la Kawaida la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani humo.   "Pamoja na majukumu haya niliyopewa sitachoka kumtetea, kumsemea na kumpambania kijana wa kitanzania, lakini pia hata katika sekta hii ninayoisimamia huku ndio nitaweka nguvu zaidi ili ikiwezekana na sekta zingine ziige  kutoka kwetu namna ya kumsaidia kijana wa kitanzania"amesema N'gwasi. Katika hatua nyingine Mhe. Ng'w...

DKT. BASHIRU AHIMIZA MJADALA ULINZI WA RASILIMALI ZA UVUVI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewataka wadau wote wa sekta ya Uvuvi kushirikiana na Serikali kujadili na kupata suluhu kuhusu ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi ikiwa ni pamoja na kukomesha uvuvi usiofuata sheria na taratibu. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo Desemba 23,2025 wakati akizungumza na wadau wa sekta hiyo waliopo mwalo wa Kakukuru Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza ambapo ameeleza kuwa katika kipindi cha uongozi wake hatochoma nyavu za Uvuvi au kupima samaki kwa rula kama ilivyokuwa awali. “Nimemsikia mtu wa “BMU” anataka achome haraka haraka, tunachoma kuna nini humo hata ukizichoma unapata samaki? “Amehoji Balozi Dkt. Bashiru. Balozi Dkt. Bashiru ameongeza kuwa kama kutolindwa kwa rasilimali hizo kunaweza kusababisha mgogoro baina ya wavuvi wa dagaa dhidi ya wavuvi wa samaki na wavuvi wa Sangara dhidi ya wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba huku lawama zikielekezwa kuhamia kwa viongozi na watendaji wa Wizara. Akizungumza kwa niaba ya Wavuvi wenz...

DKT. BASHIRU AALIKA WAWEKEZAJI WA NDANI UFUGAJI SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewataka wawekezaji wa ndani kuchangamkia fursa nyingi zilizopo kwenye tasnia ya ufugaji wa samaki.  Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji na wavuvi mkoani Mara Desemba 22,2025 ambapo amewataka wawekezaji hao kuelekeza macho yao kwenye fursa za Viwanda vya vyakula vya samaki, uzalishaji wa vifaranga vya samaki na mikopo kwa vikundi vinavyofanya shughuli hizo za ufugaji wa samaki. “Ufugaji wa samaki ni utajiri na ndio maana pamoja  na changamoto zilizopo bado hakuna ambaye yupo tayari kuacha kufanya shughuli hiyo hivyo niwaalike wawekezaji hasa wa ndani kwa sababu kwenye eneo la kuzalisha vifaranga tunataka tuwe na wawekezaji ambao watahakikisha vinapatikana wakati wote na wapo ambao kwa uwezo wao wa kimtaji wameshafikia katika hatua mbalimbali” Ameongeza Balozi Dkt. Bashiru. Aidha Balozi Dkt. Bashiru amesisitiza kuwa tasnia hiy...

MHE. KAMANI: “WAFUGAJI SHIKANENI MKONO NA SERIKALI KUHUSU MAJI.”

Picha
Na. Edward Kondela Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani amewataka wafugaji kote nchini kushirikiana na serikali kujenga mabwawa na kuchimba visima ili mifugo iweze kupata maji ya kutosha. Naibu Waziri Kamani amebainisha hayo (19.12.2025) wakati alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Manyara katika Wilaya ya Hanang, ambapo amewataka wafugaji kuanzia ngazi ya mtu mmoja hadi vikundi kutekeleza hilo badala ya kuisubiria serikali pekee. Ameongeza kuwa kwa upande wa serikali itaendelea kuweka bajeti ya kujenga mabwawa na kuchimba visima, japokuwa kuna maeneo ambayo vyanzo vya maji viko karibu ambavyo wafugaji wanaweza kujiwekea mkakati wao wenyewe wa kuchimba visima kwa ajili ya maji ya mifugo yao. Katika hatua nyingine akiwa katika mnada wa Katesh uliopo wilayani humo, ameagiza Bodi ya Nyama nchini (TMB) kufika kwenye mnada huo ili kujiridhisha miundombinu inayotumika katika eneo la machinjio. Amebainisha hayo baada ya kutoridhishwa na baadhi ya miund...

DKT. NCHEMBA AVUTIWA NA VIWANGO BANDARI YA UVUVI

Picha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amevutiwa na viwango vya ujenzi wa bandari ya Uvuvi inayokamilishwa ujenzi wake Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Mhe. Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa bandari hiyo Desemba 19,2025 ambapo amesema kuwa bandari hiyo ya uvuvi ni mwanzo wa safari ya utekelezaji wa miradi mikubwa iliyoandikwa kwenye DIRA 2050. "Bandari hii ni mojawapo ya miradi mingi inayofafanua kauli za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozitoa baada ya kuapishwa kwamba atasimamia utekelezaji wa miradi inayotoa majibu ya kero za Watanzania," Amesema Mhe. Dkt. Nchemba Aidha Dkt. Nchemba ameongeza kuwa mbali na ujenzi wa bandari hiyo Serikali ipo mbioni kununua meli tano za uvuvi zitakazoongeza kiwango cha mavuno ya samaki ili kuharakisha ukuaji wa sekta ya uvuvi. Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema kuwa watahakikisha bandari hiyo inazalis...

WAFUGAJI WATAKIWA KUWA NA UHAKIKA WA MALISHO YA MUDA MREFU

Picha
Na. Edward Kondela Jamii ya wafugaji katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, wametakiwa kuweka malengo ya muda mrefu ya kuwa na maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo yao ili kuondokana na adha ya kuyakosa nyakati za ukame. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani amebainisha hayo (18.12.2025) wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja katika wilaya hiyo na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Endonyongijape kutokana na hali hiyo ambayo wafugaji wanasema kwa sasa mifugo yao haina malisho ya kutosha. Mhe. Kamani amewakumbusha wananchi kauli aliyoitoa Waziri wa Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba hivi karibuni, ambapo moja ya sekta inayotakiwa kutazamwa kwa jicho la karibu ni mifugo kutokana na kipindi hiki cha ukame kinachosababishwa na ukosefu wa mvua pamoja na mabadiliko ya tabianchi. Ameongeza kuwa ni wakati sasa wafugaji kufanya tathmini ya kuwa na maeneo yao na kuhakikisha kuwa na malisho ya kutosha huku serikali kupitia Wizara ya Mifug...

WANAOLIMA MAENEO YA MALISHO, WAONYWA WAONDOKE

Picha
Na. Edward Kondela Wafugaji na wakulima wanaolima kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo wametakiwa kuondoka mara moja kwenye maeneo hayo ili yatumike kama ilivyokusudiwa. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani amebainisha hayo leo (17.12.2025), wakati wa ziara yake ya kikazi alipozungumza na wananchi wengi wao wakiwa ni jamii ya wafugaji kwenye kongani za malisho katika Kijiji cha Engang’uengare kilichopo Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, baada ya kubainika kuwepo kwa shughuli za kilimo katika maeneo hayo. Baada ya kusikiliza kero zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa vijiji na wananchi Mhe. Kamani amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikifanya jitihada za kudhibiti migogoro ya wakulima na watumiaji wengine wa ardhi huku ikibainika baadhi ya wafugaji kushiriki katika shughuli za kilimo maeneo ya malisho. Ameongeza kuwa ni wajibu kwa serikali na wafugaji wenyewe kuheshimu na kulinda maeneo ya malisho na wasiwe mstari wa mbele katika kukiuka sheria za ...

DKT. BASHIRU AONGEZA MSUKUMO KWENYE MAPATO UVUVI WA BAHARI KUU

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ameitaka Mamlaka ya kusimamia Uvuvi wa bahari kuu (DFSA) kuongeza kiwango cha makusanyo ya mapato yatokanayo na Uvuvi wa Bahari Kuu. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameyasema hayo mara baada ya kufika na kukagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mamlaka hiyo Desemba 17,2025 visiwani Zanzibar ambapo mbali na kuwapongeza kwa kuanza kuongeza kiwango cha makusanyo amewataka kuhakikisha wanakusanya zaidi ya fedha zinazokusanywa kwenye shughuli nyingine za Uvuvi. “Mhe. Rais hapendi michakato, anataka matokeo na nyie wenyewe mliona namna ile filamu ya Royal tour ilivyofanya mapinduzi ya sekta ya Utalii hivyo na nyie mfikirie mpango utakaofanya mapinduzi kwenye Uvuvi wa bahari kuu” Ameongeza Mhe. Balozi Dkt. Bashiru. Aidha Dkt. Bashiru ameitaka Mamlaka hiyo kuweka mikakati madhubuti itakayoainisha ushiriki wa sekta binafsi kwenye Uvuvi wa bahari kuu huku akizipongeza baadhi ya sekta zilizoanza kuwekeza kwenye eneo hilo. Kwa upande w...

DKT. BASHIRU AAGIZA MAMBO 6 KATIKA KUTEKELEZA MRADI WA MAZIWA NCHINI

Picha
Na. Hamisi Hussein, Dodoma  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally, ameiagiza timu ya wataalam wanaotekeleza Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi kuzingatia maeneo sita muhimu yatakayowezesha utekelezaji wenye tija na kwa wakati mradi huo nchini. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ametoa maelekezo hayo leo, Desemba 16, 2025, katika Ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mtumba jijini Dodoma, wakati wa kikao cha kupitia mwenendo wa utekelezaji wa mradi huo, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuzingatia upatikanaji wa mbegu bora za ng’ombe wa maziwa, upatikanaji wa maji katika maeneo yanayotekelezwa mradi, utambuzi sahihi wa wanufaika, upatikanaji wa malisho kwa wafugaji, pamoja na usimamizi na uratibu unaojumuisha wadau wote wa sekta ya mifugo. " Mfanye uratibu kwa makini kupata  mbegu za bora za ng'ombe wa maziwa, malisho na maji ili hii tasnia ilete tija" Alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru. Aliongeza kuwa wataalam wanaosimamia mradi huo kuzi...

TALIRI YATAKIWA KUFANYA TAFITI ZENYE KUONGEZA THAMANI YA MIFUGO MASOKO YA NJE YA NCHI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kuhakikisha tafiti zake zinalenga kuongeza thamani ya mazao ya Mifugo ili kukidhi masoko ya nje ya Nchi. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo aliyoifanya Desemba 15, 2025 jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ulioelekeza ufugaji wa kisasa, kibishara na wenye tija. “Mimi niwaombe mambo matatu, la kwanza tafiti zenu zielekezwe katika kuongeza thamani ya mazao ya Mifugo na hasa katika kuuza zaidi kwenye soko la nje ili mauzo yaongezeke kutoka tani elfu 14 kwa sasa hadi tani elfu 50 ifikapo mwaka 2030” Ameongeza Mhe. Balozi Dkt. Bashiru. Vilevile Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameitaka taasisi hiyo kufanya tafiti zinazohusu uhimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo amesisitiza ushirikiano wa kitafiti wa Taasisi za Wizara yake na il...