DKT. BASHIRU AVUTIWA NA UWEKEZAJI SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI
◼️Ahimiza Watumishi wa Wizara yake kuwajibika Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amevutiwa na uwekezaji uliofanywa na wadau wa sekta za Mifugo na Uvuvi nchini ambapo amewataka kushirikiana kwa ukaribu na Wizara yake ili kuendelea kuzalisha mazao yanayokidhi viwango stahiki. Mhe. Balozi Dkt. Kakurwa amesema hayo Novemba 27,2025 alipotembelea viwanda vya kusindika nyama (TANCHOICE na UNION MEAT) vyakula vya Mifugo na Samaki (BACKBONE) na kiwanda cha kuzalisha chanjo (TANCHOICE) vilivyopo mkoani Pwani. “Nipo tayari kuwapa ushirikiano wote mnaohitaji na mimi nimekuja kuomba ushirikiano wenu kwa sababu bila ushirikiano wetu kazi hii haiwezi kwenda inavyotakiwa na kila jambo mnaloona ni la mafanikio mtueleze ili tulidumishe na kila mnaliona ni dosari mtubainishie afu mtoe maoni ya namna ya kuondokana na vikwazo hivyo na kutatua dosari zilizopo kwa uzoefu mlionao” Ameongeza Mhe. Balozi Dkt. Bashiru. Aidha Dkt. Bashiru ametoa wito kwa watumishi wa Wizara yake ...