Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2025

TANZANIA YAZINDUA RASMI MRADI WA STOSAR II: KUBORESHA USALAMA NA UBORA WA CHAKULA

Picha
Tanzania kung’aa masoko ya kimataifa Na Daudi Nyingo-Dar Es Salaam Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Ulaya (EU), na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), imezindua rasmi Mradi wa STOSAR II unaolenga kuimarisha mifumo ya Sanitary and Phytosanitary (SPS) katika ukanda wa SADC ili kuwezesha biashara salama, ushindani na uendelevu wa mazao ya kilimo na vyakula. Akizindua mradi huo tarehe 1 Septemba 2025 katika Hoteli ya Four Points by Sheraton jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede, alisema mradi huo utashughulikia maeneo muhimu yakiwemo afya ya wanyama, afya ya mimea, lishe na maendeleo ya minyororo ya thamani, hususan katika nyanja za uchunguzi na ufuatiliaji wa magonjwa, udhibiti wa ubora, na upatikanaji wa masoko ya kikanda na kimataifa. “Mkutano huu ni tukio mahususi la kuzindua mradi huu wa kikanda ambao Tanzania ni miongoni mwa wanufai...

MIFUGO NA UVUVI YAANZA KIBABE SHIMIWI 2025

Picha
◼️ Yawararua Maadili 2-0 Kamba Wanaume ◼️Yatwaa Magoli 40 na pointi 2 Mpira wa pete baada ya Maendeleo ya Jamii kutokomea kusikojulikana Timu za mchezo wa Kamba upande wa Wanaume na Mpira wa pete kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi zimeanza vema kampeni ya kuwania ubingwa wa michuano ya SHIMIWI 2025 baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yao ya leo Septemba 01,2025 iliyofanyika jijini Mwanza. Nyota njema kwa Timu hizo ambazo zimekuwa gumzo jijini Mwanza tangu zilipoingia ilianza kwa upande wa mchezo wa kuvuta Kamba Wanaume ambapo walipimana ubavu na timu ya Tume ya Maadili na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mivuto yote miwili. Baada ya ushindi huo kikosi cha wachezaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kilielekea kwenye uwanja wa CCM Kirumba kulikofanyika mchezo wa mpira wa Pete baina yao na timu ya Maendeleo ya jamii ambayo ilipotea ghafla na kumlazimu mwamuzi wa mchezo huo kuipa timu ya Mifugo na Uvuvi ushindi wa magoli 40-0 na pointi 2. Kampeni ya kusaka ubingwa wa Michuano hiyo kwa Upa...

MIKATABA YA UBORESHAJI KITUO CHA UKUZAJI VIUMBE MAJI KINGOLWIRA YASAINIWA

Picha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena ameongoza zoezi la utiaji sani baina ya serikali na wakandarasi watakaotekeleza miradi ya ukarabati wa vitotoreshi ya vifaranga, ujezi wa  mifumo ya hewa kwenye mabwawa ya kufugia samaki, uchimbaji wa visima vya maji eneo la Kingolwira mkoani Morogoro na ujenzi wa Soko la Samaki  Kipumbwi katika wilaya ya Pangani mkoa wa Tanga  na kuwataka wakandarasi hao kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na kuzingatia viwango vya ubora kama mkataba unavyoelekeza.  Bi. Meena amesema hayo leo Agosti 29, 2025 katika ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma mara baada kusaini mikataba minne na wakandarasi hao ambapo aliwasisitiza kuzingatia muda na ubora wa miradi kulingana na makubaliano ya Mkataba. "Miradi hii ni ya kimkakati kwa wizara yetu na kama mnavyojua inawagusa moja kwa moja wananchi hivyo mtekeleze  kwa kuzingatia muda na ubora wa miktaba ili uwanufaishe wananchi wetu." Alis...