UTAFITI WA WINGI WA SAMAKI ZIWA TANGANYIKA UMEANZA RASMI
Na. Stanley Brayton, WMUV Kigoma Agosti 27, 2025 Nchi zilizopo ukanda wa Ziwa Tanganyika ambazo ni Tanzania, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi, zimezindua rasmi zoezi la Utafiti wa wingi na mtawanyiko wa Samaki katika Ziwa Tanganyika, ambao zoezi hilo linalenga kutambua wingi wa mazao ya Uvuvi katika Ziwa hilo. Akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa Utafiti wa wingi na mtawanyiko wa Samaki Ziwa Tanganyika, leo Agosti 27, 2025 Mkoani Kigoma, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede amesema Serikali imeelekeza kufanya Tathmini ya wingi wa Samaki waliopo katika Ziwa Tanganyika ili kujua wametawanyikaje na kwenye maeneo yapi, pamoja na kujua Takwimu sahihi za wingi wa Samaki katika Ziwa hilo. “Utafiti huu utahusisha mazao ya Uvuvi aina ya Migebuka, Dagaa au Samaki wanaoelea wa tabaka la juu, ili kusaidia uwekezaji wenye tija kwa takwimu na kuvutia wawekezaji.” ameseama Dkt. Mhede Aidha, Dkt. Mhede ameweka bayana kuwa zoezi hilo halifanywi ...