BI. MEENA AWATAKA WAFUGAJI NA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO KUPELEKA MIFUGO KARANTINI KABLA YA KUUZA NJE YA NCHI
Na. Stanley Brayton, WMUV Kibaha, Pwani Julai 30, 2025 ⬛ Ataka Kituo cha Karantini ya Mifugo Kwala na Kampuni ya NARCO kuweka alama kwenye mipaka ya maeneo yao. ⬛ Ataka Dawati la Ndege Wafugwao kuanzisha Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Kuku Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena amewataka Wafugaji na Wafanyabiashara za Mifugo kupeleka Mifugo yao kwenye kituo cha Karantini ya Mifugo ili kufanyiwa Uchunguzi wa Magonjwa kabla ya kuuza Mifugo hiyo nchi za nje, ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza Biashara hiyo Kimataifa. Akizungumza wakati alipotembelea Kituo cha Karantini ya Mifugo Kwala, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Shamba la Kuku la Kampuni ya Tanzania Sunshine na Kampuni ya Mkuza Chicks, leo Julai 30, 2025 Mkoani Pwani, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena amesema uwepo wa Kituo cha Karantini ya Mifugo ni fursa ya kimkakati katika kuyafikia masoko ya mifugo na mazao yake ya ndani na nje ya nchi. “Kituo hiki ni muhimu sana, na kimekaa Kim...