PROF. SHEMDOE AITAKA FETA KUZALISHA WANAOJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE
Na. Maria Mtambalike - FETA Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe ameitaka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi nchini (FETA) kuandaa wahitimu watakaoweza kujiajiri na kuajiri wengine badala ya kusubiri kuajiriwa kama ilivyo hivi sasa. Prof. Shemdoe ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao kilichokutanisha wadau kujadili rasimu ya mitaala 5 inayohuishwa na mitaala 12 mipya iliyoandaliwa na Wakala hiyo 26 Mei, 2025 Mkoani Morogoro. “Ni lazima tubadilike katika utoaji wetu wa elimu ili kuzingatia mafunzo yanayojikita kwenye ujuzi wa vitendo zaidi ili wahitimu wetu waweze kujiajiri na baadae waajiri wengine” Amesema Prof. Shemdoe. Aidha Prof. Shemdoe ameielekeza Wakala hiyo kutengeneza mitaala itakayozalisha wataalam wanaozingatia mabadiliko ya tabia nchi kwenye utekelezaji wa shughuli za Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji. “Mitaala hii pia izingatie teknolojia za kisasa ikiwa ni pamoja na matumizi ya zana mpya za Uvuvi, Ukuzaji viumbe Maji lakini mwisho mitaala hii ...