Serikali imesema kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuifungua Nchi yetu, soko la nyama limeongezeka kwa asilimia kubwa.
Akizungumza Oktoba 25,2022 wakati wa ziara ya mawaziri wa kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye Wilaya ya mbarali Mkoani Mbeya, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), alisema mwaka 2021 Tanzania iliuza takribani tani 2000 tu za nyama huku hadi kufikia sasa tayari tani 10000 za nyama zimeuzwa.
Alisema, kwa sasa soko la nyama nchini limeongezeka mara dufu nje ya nchi na kuwataka wafugaji kufuga kisasa ili kukidhi hitaji la soko.
"Kwa mara ya kwanza Tanzania imeuza nyama nyingi nje ya mipaka, Mwaka 2021 mwezi Oktoba ni tani 2000 tu ndio ziliuzwa, lakini mwaka huu Oktoba tayari tumeshauza tani zaidi ya 10000, hii ni kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu kutangaza kuwa tuna mifugo mingi na mizuri,
Bado fursa ya soko nje ya nchi ni kubwa, hivyo Wizara kwa kushirikiana na Serikali imeshatenga fedha za mashine kwa ajili ya kuchimba mabwawa ya maji kwa ajili ya mifugo, "alisema Mhe. Ulenga.
Aidha Mhe. Ulega aliwataka wafugaji kuunga mkono jitihada za Serikali ili kwa kushirikiana waweze kufuga kisasa, kwa tija na kufikia malengo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na kamati ya mawaziri wa kisekta wa kutatua migogoro ya ardhi wakati wa ziara yao kwenye kata ya Ubaruku, tarafa ya Rujewa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Oktoba 25,2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni