Nav bar

Jumatano, 19 Oktoba 2022

WIZARA YATOA ELIMU KWA WADAU WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI

 

Afisa Utafiti (Mifugo) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Mathew Mgogo (kushoto) akimpa elimu ya ufugaji wa kuku mmoja wa wadau wa Mifugo kutoka Isanga mkoani Simiyu Bw. Masaka Manoni leo (11.10.2022)  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yanayoendelea kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji,  Mkoani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyonge (kushoto) akimueleza Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Ugani Bw. Samwel Mdachi (kulia) kuhusu ushiriki wake kwenye shughuli za ufugaji muda mfupi baada ya kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo (11.10.2022) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yanayoendelea kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji,  Mkoani Simiyu. Katikati ni Afisa Mifugo Msaidizi, Bi. Rehema Kombe.

Mmoja wa wadau wa sekta ya Uvuvi waliopo kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Rosemary Luhasile akimuonjesha dagaa wa Ziwa Victoria, Katibu Tawala Msaidizi upande wa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Maganga Simon (kushoto) leo (11.10.2022) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yanayoendelea kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji,  Mkoani humo.

Katibu Tawala Msaidizi upande wa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Maganga Simon akionja dagaa wa Ziwa Victoria walioletwa na mmoja wa wadau wa sekta ya Uvuvi waliopo kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Rosemary Luhasile (hayupo pichani) muda mfupi baada ya kufika kwenye banda la Wizara hiyo leo (11.10.2022) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yanayoendelea kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji,  Mkoani humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni