Nav bar

Alhamisi, 12 Mei 2022

SERIKALI KUKUZA SOKO LA MAZIWA NCHINI - NDAKI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki  amesema Serikali imeendelea na  mkakati wa  kukuza Soko la maziwa Nchini kwa kuimarisha na kuendeleza programu ya unywaji wa maziwa shuleni.

 

Mhe. Ndaki  aliyasema hayo Mei 10, 2022 wakati akijibu swali la Mbunge wa Busanda Mheshimiwa Bryceson Magessa  ambaye alitaka kufahamu  mkakati wa Serikali  katika kushughulikia Soko la ndani la maziwa kwa kuhimiza na kuhamasisha unywaji wa maziwa shuleni kabla ya kutafuta masoko ya nje.


Alisema mpango wa unywaji maziwa shuleni umeweza kuwafikia watoto 90,000 wa shule za msingi 39 katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Mbeya na Tanga.


Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa Nchini kwa kutoa elimu kupitia vyombo vya habari, maonyesho  mbalimbali na wiki ya maziwa  kitaifa inayoadhimishwa mwezi Mei kila mwaka.


Mhe. Ndaki amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali itakutana na wadau mbalimbali wakiwemo wa tasnia ya maziwa Ili kuandaa mikakati thabiti kwa lengo la kuongeza idadi ya shule zinazotoa huduma ya unywaji maziwa.Hakuna maoni:

Chapisha Maoni