MAJIBU YA SERIKALI KUHUSU HOJA ZILIZOIBULIWA NA WAVUVI KUPITIA GAZETI LA NIPASHE LILILOKUWA NA KICHWA CHA HABARI ‘WAVUVI WATAKA BEI ELEKEZI SANGARA’ LA TAREHE 22 NOVEMBA, 2018 NA. HOJA MAJIBU 1. Kukosekana kwa bei elekezi ya Sangara Kufuatia malalamiko ya wavuvi kuhusu bei ya Sangara, Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi alishafanyia kazi suala hilo ambapo akiwa Kanda ya Ziwa, alifanya mkutano na wamiliki wa viwanda na bei elekezi ilitolewa kwamba kwa kila kilo moja ya Sangara bei itakuwa ni Tsh. 5,500/= . Aidha, wadau wa viwanda pia walikiri kwa barua kwamba watatekeleza bei elekezi kama ilivyoamriwa. 2. Kukandamizwa na kunyanyaswa kwa wavuvi na wanaosimamia sheria Operesheni zinazoendelea zinatekelezwa kwa mujibu wa Sheria za Nchi zikiwemo:- Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya Mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2009; Sheria ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 1998 na marekebish...
Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2018