Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2018
Picha
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHE. LUHAGA MPINA AONGEZA MUDA WA ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO HADI JANUARY 31 MWAKA HUU Na Mwandishi Maalum, Simiyu WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina ameongeza muda wa mwezi mmoja zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa hadi Januari 31 mwaka huu  huku akitangaza kuwavua nyadhifa zao Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Erastus Mosha na Kaimu Mkurugenzi wa Ugani na Usajili, Bezia Rwengozibwa kwa kushindwa kusimamia kimamilifu zoezi hilo. Mbali na wakurugenzi hao pia Maafisa wawili wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luzangi Deogratius na Felista Kimario wamepewa onyo kali kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo la upigaji chapa kitaifa huku waliovuliwa madaraka akiagiza wachukuliwe hatua kali za kinidhamu. Akizungumza jana katika zoezi la kuhitimisha upigaji chapa kitaifa katika Kijiji cha Migato Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Waziri Mpina alisema kutokana utekelezaji wa  zoezi hilo kutokuwa w...