Nav bar

Jumanne, 18 Desemba 2018


MAJIBU YA SERIKALI KUHUSU HOJA ZILIZOIBULIWA NA WAVUVI KUPITIA GAZETI LA NIPASHE  LILILOKUWA NA KICHWA CHA HABARI ‘WAVUVI WATAKA BEI ELEKEZI SANGARA’ LA TAREHE 22 NOVEMBA, 2018
NA.
HOJA
MAJIBU
1.
Kukosekana kwa bei elekezi ya Sangara


Kufuatia malalamiko ya wavuvi kuhusu bei ya Sangara, Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi alishafanyia kazi suala hilo ambapo akiwa Kanda ya Ziwa, alifanya mkutano na wamiliki wa viwanda na bei elekezi ilitolewa kwamba kwa kila kilo moja ya Sangara  bei itakuwa ni Tsh. 5,500/=. Aidha, wadau wa viwanda pia walikiri kwa barua kwamba watatekeleza bei elekezi kama ilivyoamriwa.
2.
Kukandamizwa na kunyanyaswa kwa wavuvi na wanaosimamia sheria
Operesheni zinazoendelea zinatekelezwa kwa mujibu wa Sheria za Nchi zikiwemo:- Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya Mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2009; Sheria ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 1998 na marekebisho yake ya Mwaka 2007; Sheria ya Mazingira Namba 20 ya Mwaka 2004; Sheria ya Uhujumu Uchumi (Economic and organized Crime Act Cap 200 Re 2002 as amended by Act No. 3 of 2016); na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Namba 29 ya Mwaka 1994. Aidha, kutokana na malalamiko ya kunyanyaswa wananchi, wizara inashauri waliotendewa ukatili huo walete taarifa rasmi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
3.
Nyavu stahili hazipatikani
- Serikali imeendelea kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyavu za kuvulia samaki zinazokubalika kisheria. Mpaka sasa kuna viwanda sita (6) vya kutengeneza vyavu ambavyo ni pamoja na CFN na Nafaka, (Mwanza), Sunflag (Arusha), Nyota Venture, Nyamagana Fishing Net na Nashoni Mwita (Dar Es Salaam). Aidha, kuna maduka manne (4) yanayouza nyavu za kuvulia samaki, maduka hayo ni pamoja na Imara Fishnet, Kariakoo Fish net, Mbilinyi Enterprises na Walid Trading yote yapo Dar Es Salaam.
 Katika kuhakikisha kwamba wavuvi wanamudu bei za vifaa vya uvuvi, Serikali inatoa msamaha wa kodi kwa zana za uvuvi na malighafi zake zikiwemo nyuzi za kushonea nyavu (twines) na vifungashio. Aidha, Serikali imeendelea kushauri wavuvi kujiunga katika vikundi ili waweze kukopesheka kwa urahisi  na taasis za fedha kwa ajili ya kupata fedha za kununulia zana za uvuvi zikiwemo nyavu za kuvulia samaki.
- kwa sasa Serikali inatoa vibali vya kuingiza nyavu nchini ili kuziba upungufu ulipo.  Mpaka sasa jumla ya vibali 31vimeshatolewa toka Julai mpaka Novemba,2018 kwa ajili ya kutatua changamoto ya upungufu wa nyavu nchini.
4.
Wavuvi kutozwa Kodi nyingi kama kodi za TRA, Halmashauri, kodi za samaki, mialo na kodi za Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu
Kodi zote wanazopaswa kulipa wavuvi ziko kwa mujibu wa sheria za nchi na hivyo wavuvi wanashauriwa kufuata sheria zilizopo.




Jumatano, 14 Novemba 2018

KIKAO KAZI CHA WAZIRI MH. LUHAGA MPINA NA WASINDIKAJI WAKUBWA WA MAZIWA NCHINI.




Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Joelson Mpina (Mb) amekutana na Kampuni kubwa za usindikaji wa maziwa nchini (Tanga Fresh, ASAS,MILCOM NA AZAM) leo tarehe 12/11/2018 jijini Dodoma.

Lengo la kikao kazi hicho ilikuwa ni kujadili mikakati ya uongezaji wa Usindikaji wa maziwa kwenye Kampuni kubwa za Maziwa nchini.

 Nataka Ifikapo tarehe 12/12/2018 mkakati wa ushirikiano uwe umekamilika na kusainiwa kati ya
Kampuni za Wasindikaji wa Maziwa na Dawati la Sekta Binafsi, alisema Mh.Waziri Luhaga Mpina.

Mhe. Mpina aliwaelekeza Wakuu wa Idara na Vitengo kila mtu kwa upande wake kulitumia na
kulisimamia dawati katika kutekeleza Mikakati iliyopangwa.

 Mkakati huu unaenda kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa asilimia 84.7 kwa mwaka, alisema Mpina.

Tunazindua mkakati wa dawati tarehe 15/12/2018 na kwenda kuwakabidhi mitamba 350 kwa wafugaji wa Chama Kikuu-Tanga kama shukurani kwa jitihada za wenzetu wa TADB, Mpina.

Serikali imefanya jitihada kubwa katika kuongeza uzalishaji wa maziwa ili kusaidia wasindikaji wa
maziwa kwa kutekeleza yafuatayo:-

·         kuendelea kuboresha vituo vya Uhimilishaji (AI) kwa kutoa mbegu bora.
·         ujenzi wa maabara ya (embro transfer) inayozinduliwa mwezi Januari, 2019 Mpwapwa.
·         Kudhibiti uingizwaji wa maziwa kutoka Nje kwa kuongeza kodi ili kulinda viwanda vya ndani.
·         Serikali imetoa hekta 10,000 Ruvu kwa ajili ya ufugaji ng’ombe wa maziwa.
·         Serikali itasambaza Madume kwa bei ya ruzuku.
·         Tumehamasisha viwanda vya vyakula vya mifugo.

Tutahakikisha katika maeneo ya wafugaji Huduma zote za Ugani zitatolewa na wataalamu wetu na
zitawafikia kwa ajili ya kujua uzalishaji wa Mifugo, alisema Mpina.

Mhe Waziri aliwasisitizia Wawekezaji kuwa, kuna vijana wamemaliza vyuo mbalimbali vya Mifugo na hawana ajira watumieni kuongeza Uzalishaji.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi Kampuni ya Tanga Fresh,Bw. Michael Karata alimpongeza Mhe. Waziri Mpina kwa jitihada za kuwaunga mkono alizozichukua katika sekta hiyo mpaka sasa.

Kampuni hiyo ya maziwa ya Tanga Fresh iliahidi kuongeza Usindikaji wa Maziwa kutoka Lita 45,000 hadi 90,000 kwa siku ifikapo Disemba 2018.

Vilevile Mkurugenzi wa ASAS Bw. Fuad Abri alisema,tunashukuru na kuunga mkono Sekta hii ya maziwa na ndoto ya ASAS sio kuuza Tanzania bali kuuza nje ya Tanzania.

 Tutahakikisha tunaachana na maziwa ya unga na kutumia maziwa ghafi alisisitiza Mkurugenzi wa
Mahusiano, Bw. Hussein Ally AZAM.

 Kwa upande wake Meneja wa TADB Kanda ya Kati Bw. George Nyamrunda alisema, watakopesha
wafugaji na wadau katika kuongeza uzalishaji wa maziwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Profesa Elisante Ole Gabriel naye alisisitiza,
Wakurugenzi watumie muda wao kulijua kwa undani na kulisaidia dawati la Sekta binafsi ili liweze
kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Aidha Prof.Gabriel alilitaka Dawati hilo kushirikiana kwa karibu na Kitengo cha Mawasiliano ili
kuelimisha umma juu ya utekelezaji wa shughuli zifanywazo na dawati hilo.

Pia Katibu Mkuu Prof.Gabriel aliiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini (TADB)iangalie uwezekano wa kusaidia ununuzi wa vifaa vya Kitengo cha Mawasiliano ili kufanikisha utekelezwaji wa mkakati wa Mawasiliano wa Wizara.

Mhe. Waziri na KMM wakilikiliza maswali kutoka kwa wadau wa maziwa ( hawapo pichani)

Mhe. Waziri na KMM wakisikiliza kwa makini malengo ya kampuni ya ASAS


Jumanne, 13 Novemba 2018

MAKATIBU WAKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA WATUMISHI WA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI.


Kufuatia kikao cha watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kilichofanyika Leo tar 7/11/2018 katika ukumbi wa VETA DODOMA Katibu Mkuu Mifugo ahamasisha yafuatayo:-

Ushirikiano kati ya watumishi ni jambo la Msingi sana ili kuweza Kufanikisha shughuli zetu za kila siku pia ni lazima tufanye kazi kwa kujituma.

Changamoto siyo sehemu ya maisha ila changamoto ndiyo maisha yenyewe, kwa hiyo tunazitumia hizo changamoto kama fursa.

Wakurugenzi  na  wakuu  wa vitengo  jitahidini sana kuwasikiliza mnaowaongoza ,na  kuwasimamia na kubwa  zaidi kujali maslahi yao.

Nataka Wizara hii iende kwa kasi sana ,Idara ya Uzalishaji na Masoko Ikiwa kama Operating Engine kwa sababu ndiyo yenye activities nyingi sana

Pia napenda kuwataarifu  rasmi  kuwa Dr. Angelo Mwilawa  kuanzia  sasa nimemteua  kuwa Mkurugenzi Rasmi  wa Idara ya Ugani na mafunzo (DRTE) hapo awali alikuwa anakaimu. 

KMU asisitiza Sekta zote mbili kuwa na ushirikiano

KMM akiongea na watumishi ( hawapo pichani) na kusisitiza ushirikiano katika kazi

KMM na KMU wakiteta jambo na Mkurugenzi msaidizi wa Ukuzaji Viumbe kwenye maji




Picha ya pamoja Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi



Makatibu Wakuu, wakiwa naWakuu wa Idara, Vitengo na Tahasisi katika picha ya pamoja

Jumatano, 7 Novemba 2018

PROJECT LAUNCHING WORKSHOP, 07 NOVEMBER,2018. AT MORENA HOTEL DODOMA.

Prof. O. Gabriel receives inception report from Hon. Minister of Agriculture Dkt. Charles Tizeba

Ongoing speech from Permanent Secretary

Picture with Minister of Agriculture, Permanent Secretary, AGRA team and ESRF members

NEW ZEALAND KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI




Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), amekutana na Balozi wa New Zealand Nchini Tanzania Mike Burrell Ofisini kwake leo tarehe 06/11/2018 jijini Dodoma.

Tumekuwa tukishirikiana vyema kati ya Nchi ya Tanzania na New Zealand katika kupata madume bora ya Ng’ombe 6 kule kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) kilichopo UsaRiver jijini Arusha ambayo yamechangia uzalishaji wa mbegu bora kuongezeka zaidi, alisema Mh. Ulega.

Mh.Ulega alisema tutasaidiana katika upande wa ufugaji wa samaki, ambapo wenzetu wako mbele
zaidi katika masuala ya Ukuzaji viumbe kwenye maji.
“ Our President Dkt. John P. Magufuli is trying so hard to ensure that, our environment in Tanzania is
getting better and better”. Say’s Ulega.

Vilevile Mhe. Ulega alisema kunahitajika watu wa kwenda kusoma katika kada ya Sayansi ambapo kwa sasa bado tunapeleka watu wachache katika fani hiyo.

Kwa upande wake balozi Mike alisema, tunahitaji Ushirikiano na Tanzana katika kuwekeza kwenye
Sekta ya Mifugo na Uvuvi.
“We assure to share information and cooperate with you because the country has a huge potential”.
Say’s Hon. Mike.

Tunahitaji wanasayansi kutoka Tanzania wenye elimu ya juu hasa waliobobea katika masuala ya
Sayansi, “ We love to have Scholars in New Zealand from your country, alisema Hon. Mike.

 We encourage people to come and learn more about aquaculture,say’s Hon. Mike.

Naye Katibu Mkuu Mifugo Prof.Elisante Ole Gabriel alisema, NARCO wanahitaji kunufaika na kupata Wataalamu kutoka New Zealand kuhusina na Mifugo katika Uzalishaji.


Naibu Waziri Mhe. Ulega akiongea jambo na Balozi wa New Zealand Nchini Tanzania Mhe. Mike Burrell

Balozi Mike akisalimiana na Wakurugenzi




Jumatatu, 5 Novemba 2018

WAKURUGENZI WAPYA WATAMBULISHWA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI



Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante Ole. Gabriel leo atambulisha Wakurugenzi wapya katika kikao cha Wakuu wa Vitengo na Idara kilichofanyika katika Ukumbi wa NBC Leo.

# Prof. O. Gabriel, alisisitiza Wakurugenzi kujifunza kwa watu na kuwa na Ushirikiano.

#KM aliwataka Wakurugenzi kuwa wabunifu katika kazi zao ili kuinua Sekta.

# Prof. aliwaomba Wakurugenzi kukabiliana na changamoto zilizopo na kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuzitatua.

# Alisisitiza kujenga utamaduni wa Kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa Ushirikiano.

Katibu  Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel ampongeza na kumkaribisha Kaimu Mkuu mpya wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini Bi. Rehema ,bulalina, leo katika ukumbi wa NBC


KM Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel ampongeza na kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa Idara ya Huduma za Mifugo Dkt. H. Nonga, Leo katika ukumbi wa NBC

KM Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel  ampongeza na kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa Idara ya Uzalishaji Mifugo na Masoko Dkt. Felix Nandonde




Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza maagizo kutoka kwa KM (hayupo pichani)

























Ijumaa, 2 Novemba 2018

KATIBU MKUU ATEMBELEA SOKO LA SAMAKI FERRY KUKAGUA UJENZI WA VYOO:



Leo Katibu Mkuu wa Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama alikwenda kuangalia utekelezaji wa ujenzi wa vyoo 24 hiyo ikiwa ni katika hatua za utekelezaji wa ahadi za Mh. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina alipotembelea sokoni hapo na kubaini mapungu yaliyopo ikiwemo.

1. Uchakavu wa majengo
2. Upungufu wa vyoo;
3. Kujaa kwa mchanga katika bahari: na
4. Uchakavuwa jokofu la kuhifadhia samaki

Ambapo alisema kuwa Wizara yake itaingilia kwa kuchukua hatua za haraka katika hayo na kuagiza mara moja kwa ujenzi wa vyoo 24 ambavyo vitapunguza msongamano sokoni hapo.

Katibu Mkuu wa Uvuvi, Dkt. Rashidi Tamatamah ametembelea soko la samaki Ferri- Kivukoni kuangalia ujenzi wa vyoo 24 ambavyo vitapunguza msongamano katika soko hilo.

Katibu Mkuu Uvuvi, akielekea eneo la ujenzi akiambatana na Meneja wa soko  Bw. Mkuu Anje

Katibu Mkuu Uvuvi akiwa katika eneo la Ferry 
Katibu Mkuu akiwa na Meneja wa soko hilo akifafanua jambo sokoni hapo


Choo ambacho kinatumika kwa sasa na kutokana na wingi wa watu hakikidhi maitaji yao

Katibu Mkuu akipata maelezo juu ya ujenzi huo unavyoendelea


Jumatano, 31 Oktoba 2018

SERIKALI IPIME MAENEO YA WAFUGAJI ILI WAMILIKISHWE KISHERIA




Wafugaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro wamewalalamikia watendaji wa Serikali na kwamba wao ndio wanao chochea Migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai.

Malalamiko hayo yametolewa jana na wafugaji wa kijiji cha Sanya Station, katika kata ya Kia, katika Halmashauri ya Wilaya Hai, walipokuwa wakitoa kero zao kwa Katibu Mkuu Mifugo, Prof.Elisante Ole Gabriel, aliyefika katika kijiji hicho kusikiliza kero za wafugaji hao kwa Niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe .Luhaga Joelson Mpina.

“Sisi Wafugaji na Wakulima natuna tatizo kabisa, Shida kubwa iko kwa hao Mgambo, ambao wanatumwa na watendaji wa Serikali waje wakamate Ngombe wetu bila kosa lolote na kufanya mradi wao wa kuwaingizia fedha;.alisikika Mfugaji akilalamika.

Aidha watumishi waliopo katika taasisi za Umma za NARCO na TALIRI ,West Kilimanjaro nao wamelalamikiwa na wafugaji hao kuwa ni vinara wa kuchukua rushwa hasa Ngombe wa wafugaji wanapokamatwa wakiwa katika maeneo ya Taasisi hizo wakipata Malisho.

Aidha,Wafugaji wa kijiji cha Sanya Station wamemweleza katibu Mkuu kuwa, changamoto kubwa waliyonayo kwa sasa katika kijiji hicho ni pamoja na, uhaba wa maeneo ya Malisho, Mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda wa miaka 30, ambapo mamlaka ya kiwanja cha ndege ya KIA wananataka kuwapora ardhi waliyoridhishwa na Mababu zao ,Eneo halali lenye kubwa wa Hekta Elfu 11, lenye wakazi zaidi ya Elfu ishirini na nne (24,000) katika kata ya Kia.

Changamoto nyingine waliyotaja ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya Majosho ,ukosefu wa visima virefu vya kunyweshea Maji Mifugo na kukosekana kwa Mnada katika Eneo hilo.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha Wafugaji Taifa Bw. Magembe Makoye, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe John Pombe Magufuli kwa Kuwateua Viongozi waandamizi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ukianzia na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina, Katibu Mkuu Mifugo, Prof.Elisante Ole Gabriel ambao kwa asili wote ni wafugaji.

Makoye amewaasa Wafugaji kufuata kanuni, Taratibu na sheria za nchi ili waendelee
kuheshimika, kwani wafugaji wanajitosheleza kwa kila kitu ndio maana hawajawahi kuomba chakula Serikalini na wanasomesha watoto wao bila tatizo lolote.

Tunaomba Serikali ipime maeneo ya wafugaji ili wamilikishwe kisheria,  Sasahivi kila hifadhi
imeanzisha Mahabusu ya Mifugo, Ngombe wakikamatwa ndani ya hifadhi anapigwa faini ya
Tsh.100,000/= kwa ngombe mmoja. Hii ni rasimu ya sheria ambayo ilikuja kwa wadau tuliikataa, cha kushangaza watu wa Maliasili wanaitumia, hii ni sheria kandamizi ;alisema.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Hai Bw.Lengai Ole Sabaya amepiga Marufuku kwa watendaji wa Vijiji na Vitongoji kupokea fedha yoyote ya Migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji. Mhe Sabaya amesema kuwa Migogoro mingi inayotokea ni kwa sababu wananchi wa kifugaji hawashirikishwi  katika ngazi za maamuzi.

Akifanya Majumuisho ya Mkutano huo, Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel ameishukuru kamati ya Ulinzi na Usalama ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai kwa kutatua Migogoro iliyopo kwa Weledi Mkubwa.

Ole Gabriel amesema kuwa Serikali inatambua haki za Wafugaji,katika nchi hii wafugaji ni
wawekezaji, Lakini ni lazima wafugaji wazingatie sheria, kwani wanamchango mkubwa sana katika Uchumi wa Viwanda.

Rais Magufuli anawapenda wafugaji lakini pia yeye mwenyewe ni Mfugaji, ndio maana katika ilani ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 25 yote inaongelea Wafugaji na namna Bora ya kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Prof.Gabriel amesema kuwa changamoto mbalimbali walizozieleza Wafugaji hao zinafanyiwa kazi kwani Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Sikivu.

Pia Katibu Mkuu Mifugo aliwakumbusha wafugaji kuachana na kufuga kwa mazoea, amewambia wakati umefika sasa kubadilika na kuanza kufuga Kisasa na Kibiashara.



Katibu Mkuu Mifugo na Mbunge wa Siha Dr. Mollel wakifurahia jambo mara baada ya Mzee wa jamii ya kimasai kuja kuwasalimia mara baada ya mkutano kumalizika.

Katibu Mkuu akiongea na wafugaji


Jumatatu, 29 Oktoba 2018

SERIKALI YATEKETEZA NYAVU ZA WAVUVI HARAMU NYUMBA YA MUNGU


Serikali imepiga marufuku uvuvi haramu na kuteketeza nyavu aina ya makokoro 35 , makila 6 na nyavu za zenia 25 zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo Mkoani Kilimanjaro

Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kagongo kata Lang’ata leo amesema serikali haitamwonea huruma mtu yeyote atakayekamatwa akijihusisha na uvuvi haramu kwani serikali imekua ikipoteza kiasi kikubwa cha mapato kutokana na uvuvi huo.

“Hatuna utani na mtu asiye na huruma na rasilimali za nchi hii, Tanzania ndio nchi yenye sehemu kubwa yenye maji kuliko sehemu nyingine lakini bado tunaagiza samaki kutoka nchini china, tumeagiza sato., perege hadi kibua wa kichina, tusipotokomeza leo bwawa litakuwa historia kwa vizazi vijavyo” amesema Ulega

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alisema uwepo wa bwawa hilo
umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika eneo hilo na sasa ni wakati wa wananchi kuwa walinzi kwa kila mmoja ili kutokomeza uvuvi haramu.

“Hebu leo amueni kabisa kwamba biashara ya samaki ndio mfumo wa maisha yenu, Ninyi mkifanya
hivyo sisi hatutahitaji kufunga hili bwawa , wakati wote tutahitaji kuongeza kizazi cha samaki na kuleta wataalamu kupima kiwango cha samaki tulichonacho” alisema Mghwira

Kwa upande wake Dismas Gondwe mkazi wa kijiji cha kigongo kata ya Lang’ata amesema uvuvi haramu katika bwawa hilo unatokana na kukosekana kwa utaratibu maalumu unaowaelekeza wavuvi kuendesha shughuli zao katika bwawa hilo.

Gondwe ameiomba serikali kuwawezesha wavuvi wa bwawa la Nyumba ya Mungu zana harali ambazo serikali inazitambua.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi wa kijiji cha Kagongo kata ya Langata mkoani Kilimanjaro juu ya serikali kutokumuonea huruma mtu yoyote ambaye anajiusisha na shughuli za uvuvi haramu 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (wa kwanza kulia) kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro , Anna Mghwira na  Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Aatron  Mbogho wakiteketeza zana haramu zilizokuwa zikitumika katika uvuvi haramu kwenye Bwawa la Nyumba  ya Mungu.



UZINDUZI WA BODI YA KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA (NARCO)*



Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imezinduliwa rasmi  tarehe 27/10/2018 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina.

Ninawashukuru wote kwa kukubali uteuzi huu kwa sababu natambua hakuna kazi iliyo nyepesi - Waziri Mpina

Namshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa uteuzi huu kwani ametambua uwezo na uzalendo wenu, Nchi hii inapaswa kuendelezwa na wananchi wazalendo watakaowezesha Nchi kusonga mbele - Mhe. Mpina

Ni matarajio yangu kuwa; Bodi hii itaweza kufikia Mikakati tuliojiwekea na ndani ya Wiki mbili zijazo lazima kikao cha Bodi kiitishwe ili kuanza utekelezaji wa mikakati tutakayojiwekea - Waziri Mpina

Sekta ya Mifugo ina mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa letu ambapo mpaka sasa jumla ya Mifugo tuliyonayo ni mil 57 na tunazalisha Lita Bil 2.4 za Maziwa - Waziri Mpina.

Tunahitaji mpaka mwakani tuongeze idadi kubwa ya Mifugo kwa sasa, tuna Ngombe milioni 30.5, mbuzi 18.8 mil, kondoo Mil. 5.3, nguruwe Mil. 1.9, Kuku wa kienyeji Mil. 38.2, na wa kisasa ni Mil. 36.6.

Mpaka sasa idadi ya mifugo inayouzwa Nje ya Nchi kwa njia haramu na halali ni asilimia 70 na mifugo michache tuliobaki nayo ni asilimia 30 - Waziri Mpina.

 Mazao mengi yanaingia Nchini bila kufuata taratibu na Mifugo inatoroshwa kwakuwa hatuna Viwanda vya uhakika hapa Nchini, tuna viwanda 32 lakini ni machinjio- Waziri Mpina.

Ifike mahali kwenye Taasisi za Serikali ikiwemo na NARCO Kuwe na viwanda vya uhakika Itakuwa ni mfano na kielelezo kwa Sekta binafsi - Waziri Mpina.

 Tumepandisha tozo kuanzia 1000 hadi 10,000 ili kila mmoja aweze kumiliki eneo ambalo anauwezo
nalo - Waziri Mpina.

Shirika lifike mahali linatoa nyama ya ng’ombe ndani na Nje ya Nchi na kutengenza bidhaa zitokananzo na ngozi - Waziri Mpina

Naitaka Bodi na timu nzima  kuhakikisha mnaandaa mpango kazi na wa biashara kwa kushirikiana
na Dawati la Sekta Binafsi - Waziri Mpina

 kwa mashirika yangu yote kabla ya tarehe 30/11/2018 lazima tuandae gawio letu kwa Serikali - Waziri Mpina

Ni lazima kila mmoja afahamu wajibu wake ili tuweze kufikia mafanikio tuliyojipangia - Waziri Mpina

Watendaji wa Wizara yangu mtakuwa na kazi ya kusimamia mikakati tuliojiwekea inatekelezaa hadi
kufikia tarehe 30/11/2018 nipatiwe mikakati hiyo - Waziri Mpina.

Naimani pamoja na magumu haya mageuzi lazima yafanyike “ penye nia Pana njia” - Waziri Mpina.

Bodi inayozinduliwa leo iko kisheria kwa mujibu wa Mashirika ya Umma na. 2 ya mwaka 1992 kifungu cha 9 (1). Natangaza rasmi uzinduzi wa Bodi hii - Waziri Mpina.

 Naamini kuzinduliwa kwa Bodi hii kutaleta mapinduzi Makubwa na ni matumaini tutalinda rasilimali za Nchi yetu - KM Prof Ole Gabriel.

Bodi hii imesheheni wataalam wanaoaminika,tunaamini wataenda kuondoa changamoto mbalimbali
zinazolikabili shirika hili - Katibu Mkuu, Prof Ole Gabriel.

Tanzania ni Nchi ya 2 kuwa na ng’ombe wengi lakini hatufanyi vizuri kwenye eneo hili ila naimani
wajumbe hawa watafanya kazi ambayo wameiandaa kuifanya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Kilimo, Mifugo, na Maji, Mhe. M. Mgimwa.

 Tunataka mwakani tuwe na idadi kubwa ya ng’ombe ambapo tukijidhatiti kukuza Ranchi zetu na
kuhusisha Sekta binafsi tunauwezo wa kupata wadau nje na ndani ya Nchi. - Mhe M. Mgimwa .

Namshkuru Rais Dkt. Magufuli kwa uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi hii, kwani najua umezingatia mengi pamoja na utendaji wako wa kazi na uzoefu wa kuitumikia nchi ya Tanzania pia tunaamini ni chaguo sahihi kwa wakati sahihi - Katibu Mkuu Mifugo Prof. Ole Gabriel.

Namshukuru Mhe. Rais kwa kuniteua naahidi mimi na wajumbe tuna uwezo wa kuifanya kazi hii -
Mwenyekiti wa Bw. Bodi Paul Kimiti.

Tutajenga timu ya kufanya kazi kwani uzoefu uliopo katika vichwa vya wajumbe hawa utakua ni
rasilimali ya kubwa katika utendaji wetu - Mwenyekiti wa Bodi Bw. Paul Kimiti

Tayari tumeanza kuweka malengo na mikakati ya utendaji kazi itakayorudisha imani ya shirika la
NARCO - Mwenyekiti wa Bodi Bw. Paul Kimiti.




Mhe Waziri akimpongeza  Mwenyekiti wa Bodi ya NARCO Bw. Paul Kimiti baada ya kuteuliwa na Mhe. Raisi.

Mhe. Waziri akisalimiana na Katibu Mkuu Mifugo

Picha ya pamoja Mhe. Waziri akiwa na Bodi ya NARCO iliyoteuliwa, Waheshimiwa Wabunge, Wakurugenzi na Watumishi wa Baraza wakati wa uzinduzi wa Bodi , Jijini Dodoma.

Alhamisi, 25 Oktoba 2018

KATIBU MKUU MIFUGO, PROFESA ELISANTE OLE GABRIEL AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA OMAN MHE. ALI A. AL MAHRUQI NCHINI TANZANIA JUU YA KUTAFUTA SOKO LA NYAMA NCHINI OMAN.



Katibu Mkuu ( mwenye suti nyeusi ) na Balozi wa Oman wakiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya mambo ya nje na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel akisema jambo kwenye kikao kifupi mapema leo  jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel akijadili jambo na Balozi wa Oman Mhe. Ali A. Al Mahruqi mapema leo jijini Dar es salaam.

Jumatatu, 15 Oktoba 2018

KATIBU MKUU MIFUGO AFANYA UKAGUZI MINADA YA SHANWA MASWA NA MWANUZI MEATU




Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.Elisante Ole Gabriel leo amefanya ukaguzi mnada ya Awali wa Shanwa uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na Mwanuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

Akiongea na Katibu Mkuu, Dkt. Gabriel Bura kutoka Wizarani ambaye pia ni mmoja wa timu Nzagamba, Dkt. Bura,amemweleza Katibu Mkuu kuwa tangu wamewasili hapo, kazi zinaenda vizuri bila shida yoyote.

Katibu Mkuu tangu timu Nzagamba imeanza kutekeleza majumu yake,katika mnada wa Senai timu ilifanikiwa kukusanya jumla ya Tsh.7,028,000/= ukilinganisha na Tsh.756,000/= zilizokuwa zinakusanywa kabla ya Nzagamba kuanza kutekeleza Majukumu yake. alisema.

Aidha Bura amesema kuwa wafanyabiashara wameanza kuelewa mabadiliko ya tozo mpya,isipokuwa bado kuna changamoto chache, baadhi ya wafanyabiashara wanafanya biashara nje Minada kinyume cha sheria ili kukwepa kwa Makusudi kulipa tozo zilizowekwe kisheria.

Wakati huo huo baadhi ya wafugaji waliokuwepo katika mnada wa Shanwa Maswa walitoa baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na kupigwa faini pale Ngombe wanapofika pungufu katika mnada wa Kizota au Pugu hata kama atakuwa amekufa njiani kwa kukanyagwa na wenzake.

Akijibu baadhi ya changamoto zilizotolewa na wafugaji na Wafanyabiashara hao, Katibu Mkuu Mifugo Prof. Ole Gabriel aliwambia wafugaji/Wafanyabiashara hao kuwa ni vyema kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa kwa mujibu wa sheria ili waweze kufanya biashara zao za mifugo bila bugudha yoyote.

Katika hatua nyingine Dkt. Benezeth Lutege akiwa katika Mnada wa awali wa Mwanuzi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,amemwambia Katibu Mkuu kuwa zoezi la ukusanyaji ushuru kwa kutumia tozo mpya liliingia dosari baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kugoma kukusanya ushuru huo kwa kutumia tozo mpya kwa kisingizio cha kutokupata Taarifa hizo Mapema.

Mkuu nililazimika kutumia nguvu kuwatangazia wafugaji na Wafanyabiashara kuwa wanatakiwa kulipa viwango vipya vya tozo vilivyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka huu wa fedha na sio vya Mwaka jana. ;alisema.

Katibu Mkuu akimsikiliza kwa makini Bw. Adam Noti, Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya MASWA (Aliyenyoosha mkono)

Katibu Mkuu akiwa na badhi ya Wafugaji na wafanyabiashara wa Mifugo katika Mnada wa Shanwa Halmashauri ya Wilaya ya MASWA.

Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika Mnada wa Shanwa katika Halmashauri ya Wilaya ya MASWA

Katibu Mkuu akiongea na baadhi ya wafanyabiashara waliopanga foleni wakisubiri kulipia tozo mbalimbali.


ULEGA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NNE YA NDEGE WAFUGWAO




Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amezindua rasmi maonesho ya nne ya ndege wafugwao katika viwanja vya maonesho (sabasaba) jijini Dar es salaam.


Akizungumza katika uzinduzi huo Ulega ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yamehusisha makampuni mengi ya ndani na nje ya nchi kama Kenya, Poland na China na amewakaribisha kuwekeza nchini kutokana na kuwepo kwa fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali.


Aidha ametoa pongezi kwa vyama vyote vya wadau wa ndege wafugwao chini ya chama mama cha Tanzania Poultry show (TPS) kwa kutoa kipaumbele katika suala la ufugaji wa kuku.


Pia amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na wao kama serikali wapo pamoja kama walezi wao, katika kuhakikisha wanasonga mbele zaidi na amewapongeza kwa ushirikiano wao kupitia vyama vyao.


Ulega amesema kuwa Rais Magufuli ameendelea kusimamia maendeleo ambapo hadi sasa tozo zilizokuwa kero kwa wafugaji, wakulima na wavuvi zimeondolewa ili kuweza kuendeleza shughuli hizo.


 Kuhusiana na changamoto zilizotolewa na wafugaji hao hasa katika mashudu na soya ambazo huagizwa kutoka nje Ulega amesema kuwa maandalizi yameanza katika nyanda za juu kusini ambako soya zimelimwa na wanavutia uwekezaji katika usindikaji ili kuweza kuvutia uwekezaji wa kuchakata soya na kupunguza gharama za kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.


Kuhusiana na machinjio zinazochinja kuku Ulega amesema kuwa sehemu hizo zimekuwa na ubora wa chini sana na amewataka wahakikishe wanaboresha machinjio hayo yanayosimamiwa na halmashauri na manispaa hasa kwa kuzingatia wanaweka  sehemu ya machinjio ya kuku ili kuleta thamani.


Mwenyekiti wa chama cha ndege wafugwao Harko Bhaghat amemshukuru Naibu Waziri na Wizara kwa ujumla kwa kutoa kipaumbele kwa wafugaji na kusema kuwa hadi sasa wamepata mafanikio makubwa na kubwa zaidi ni baada ya serikali kuondoa tozo katika bidhaa za mifugo.


Bhaghati amewataka wafugaji kujisajili ili waweze kupata fursa mbalimbali za kuendeleza soko la ndege wafugwao hasa kuku.


Mtaalamu na Mshauri wa Mifugo kutoka kampuni ya Hill Poultry Feed akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kuhusu uzalishaji na utunzaji wa mifugo unaofanywa

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa ndege wafugwao katika ufunguzi wa maonesho ya nne ya ndege wafugwao nchini jijini  Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akitembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam




Jumanne, 25 Septemba 2018

ULEGA AWATAKA WAFUGAJI KUFUGA KIBIASHARA




Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka Wafugaji kuachana na tabia ya kufuga kuku kwa mazoea badala yake wafuge kibiashara ili kujikwamua kiuchumi.

Naibu waziri amesema hayo Septemba 21 leo, wakati akifungua mafunzo ya siku  moja ya wafugaji wa kuku Mkoa wa Dar es Salaam. Wafugaji hao wametoka wilaya za Ilala, Kinondoni, Kigamboni, Temeke na Ubungo.

Alieleza Ulega ni watu wachache wanaofuga kuku kibiashara, lakini  waliobaki wanafanya shughuli kama sehemu ya maisha yao, hali inayosababisha kutofanikisha  malengo ya  kukuza uchumi.

 “Nataka mfuge kibiashara, hatutaki mfuge kuku kimazoea. Watu watambue  ufugaji kuku ni biashara kama zingine na ni fursa ya kujikwamua kimaisha,”amesema Ulega

Amesema ufugaji wa kuku sehemu mojawapo itakayowakomboa wanawake na vijana  kuondokana na changamoto ya ajira ambayo  imekuwa kilio kwa watu mbalimbali.

Ulega amesema nyama ya kuku inapendwa kila mahali  na kila mtu hususani kwenye miradi mikubwa ya maendeleo inatumika kama kitoweo chao .

“Ni vyema wafugaji wakaiona fursa hii,  kwa kuzalisha kwa wingi kuku. Tunataka watu wazalishe kuku wa kutosha ili nyama yake ishuke bei.

“Sasa hivi baadhi ya watu kula kwao nyama ya kuku hadi kuwe na shughuli fulani au sherehe jambo ambalo halileti picha nzuri hasa kwa karne hii ya uchumi wa viwanda unaosimamiwa na  Rais John Magufuli,”amesema.

Aliendelea kueleza Ulega kuwa, ifikapo 2020 nataka ugonjwa wa mdondo uwe wa kihistoria, na ifike mahala tusiagize chanjo kutoka nje bali tuzalisha wenyewe.

"Dozi moja ya mdondo kwa sasa inauzwa Tshs elfu 20 ambayo ni sawasawa na wastani wa kuku zaidi ya 300", alisema Mhe. Ulega

Ulega amewataka washiriki wa mafunzo hayo, kujiskia kuwa huru kupata ufafanuzi au kuuliza maswali yoyote kwa Wataalamu kuhusu Sekta ya ufugaji na  changamoto zake na njia za  kukabiliana nazo.

Awali ya yote Naibu Waziri alisema, ni muhimu wataalamu wangu Washirikiane na Halmashauri ili kuona ni namna gani wafugaji wetu wanaojiunga na Vyama vya Ushirika iwe njia rahisi ya kujipatia  mikopo.

"Nia yetu sisi tunataka benki ziwe rafiki kwa wafugaji wadogo wadogo na vileville mfugaji aweze kukopesha kirahisi kupitia Ushirika. Alisema

" Nataka mtumie muda huu kujadiliana na kupata mafunzo, watu wapewe vipeperushi vya ratiba ya uchanjaji wa dawa, " alielekeza Ulega

"Ni matarajio ya Serikali kuwa, baada ya mafunzo haya, maarifa ya wafugaji wetu wa kuku yataongezeka, idadi ya vijana na wanawake wanaoingia kwenye tasnia hii itaongezeka, hivyo kupanua soko la uhakika la kuku na mazao yake, alimalizia kusema.

Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti Mafunzo na Ugani Dkt Angelo Mwilawa amesema mafunzo hayo yameshirikisha wafugaji wa wilaya hizo na lengo ni  kuwajengea uwezo.

Mmoja wafugaji akizungumza kwa niaba ya wenzake, Eva Nyella, amesema “ Tulikuwa tunafuga tu, bila kujua nini cha kufanya, fursa zilizopo lakini mafunzo haya yatatusaidia. Hili ni jambo kubwa tunaahidi tutakuwa wafugaji bora.



DKT. ANGELO MWILAWA MKURUGENZI WA UTAFITI, MAFUNZO NA UGANI AKIONGEA MACHACHE NA KUMKARIBISHA MGENI RASMI

 MGENI RASMI MHE. NAIBU WAZIRI AKISOMA HOTUBA FUPI WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA KUKU  JIJINI DAR ES SALAAM



WAFUGAJI NA WATAALAMU WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI HAYUPO PICHANI


PICHA YA PAMOJA MGENI RASMI AKIWA NA WAFUGAJI NA WATAALAMU KUTOKA WIZARANI