Nav bar

Jumanne, 2 Desemba 2014

WIZARA YAFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KWA MFUGAJI WA KUKU MIEMBE SABA - KIBAHA NOVEMBA 2, 2014



Mfugaji wa kuku Bibi Fransisca Macha akitoa maelezo kwa Waaandishi wa Habari (wapo nje ya banda ) Kuwa ana kuku 2200 na Kuku wanazalisha trei 21 kwa siku, Ameeleza Changamoto kubwa ni Soko 
Sehemu ya Kuku wa Mayai wanaofugwa na Bibi Fransisca Macha Shamba hilo lipo eneo la Miembe Saba Kibaha  

Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mohammed Bahari (mwenye suti katikati) akiwa na mfugaji wa kuku Miembe Saba- Kibaha  Mama Fransisca Macha (mwenye mtoto), Afisa Mawasiliano Bibi Judith Mhina, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko  Bibi Magreth Mkami, na kutoka kushoto ni Afisa Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Fatma Salum na Dkt. Niwael Mtui Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo na Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake.

Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mohammed Bahari (mwenye suti kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  nyumbani kwa mfugaji wa kuku  Miembe Saba - Kibaha.
Vijana wanaotoa huduma kwa kuku hao wakisikiliza kwa makini  hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa .

Mwandishi wa Habari  kutoka gazeti la Tanzania Daima Bi. Asha Bani, Akiuliza swali juu ya uagizaji  wa kuku kutoka nje ya nchi.
Mwandishi wa Habari kutoka TBC-1 Bw Egidius Audax, akiomba ufafanuzi wa ni jinsi  gani Elimu inawafikia wafugaji nchini Tanzania, na Katikati ni Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar Bw Edward Lusagwa

Mwanahabari kutoka kituo cha television cha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) bwn. Edward Lusagwa akitaka ufafanuzi wa hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti ugonjwa wa Kideli  nchini.
  Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo na Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake Dkt. Niwael Mtui, akijfafanuahoja mbalimbali za wahahabari  (hawapo pichani) .
Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mohammed Bahari na baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo wakisikiliza kwa makini hoja mbalimbali zilizotolewa na wanahabari .

Mwanahabari kutoka kituo cha televisheni cha Channel Ten Bi. Kisa  Mwaipiana akiuliza swali juu ya uvumi wa dawa za ARV  kupewa kuku wa kisasa .


mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko  Bibi Magreth Mkami akifafanua hoja mbalimbali zilizotolewa na wanahabari (hawapo pichani)

kuku wa nyama na mayai wanaofugwa na Mama Fransisca Macha wakiwa katika mabanda ya kisasa.





Jumamosi, 15 Novemba 2014

WAZIRI KAMANI ASHIRIKI MKUTANO WA KUJADILI MKAKATI WA MAENDELEO WA SEKTA YA MIFUGO NAIROBI KENYA


Dkt . Titus Mlengeya Kamani (Mb)  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Akishiriki  Kwenye Mkutano wa Mawaziri Wenye Dhamana ya Sekta ya Mifugo.Kujadili Mkakati wa Maendeleo wa Sekta ya Mifugo Afrika kwa Kipindi cha 2015-2035 (The Livestock Development Strategy for Africa -LiDeSa 2015-2035).  Katika ukumbi wa Mikutano wa AU-IBR Nairobi, Kenya. 
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mkutano wa Kujadili Mkakati wa Maendeleo wa Sekta  ya Mifugo Afrika kwa Kipindi cha 2015-2035 (The Livestock Development Strategy for Africa -LiDeSa 2015-2035).  Katika ukumbi wa Mikutano wa AU-IBR Nairobi, Kenya. 

 

Ijumaa, 14 Novemba 2014

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DKT. YOHANA BUDEBA AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA WIZARA YAKE KATIKA VIWANJA VYA MVUVI HOUSE 14/11/2014

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt Yohana Budeba Akionyesha Kikombe kwa Juu Kama Ishara ya Furaha na Kuwapongeza Wachezaji Waliofanikisha Kupata Kikombe Hicho Ambacho ni cha Msindi wa Tatu Katika Mchezo wa Karata Mashindano ya Shimiwi Yaliyomalizika Mwezi Oktoba Morogoro Sherehe Hizo Fupi Zilifanyia Kwenye Uwanja wa Mvuvi House, Wakati wa Katibu Mkuu Kujitambulisha kwa Wfanyakazi wa Wizara   

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt Yohana Budeba Akimkabidhi Khatibu Muhtasi Bibi Mtage Kitule  Kikombe  cha Ushindi wa tatu cha Uchezaji Karata Kilichotolewa Wakati wa Mashindano ya Shimiwi yaliyomalizika mapema mwezi wa Oktoba 2014 Morogoro. Wakati wa Hafla fupi ya Kuzungumza na Wafanyakazi wa Wizara na na kuwapongeza kwa Ushindi huo 
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akifungu Mkutano Mfupi wa Kazi Uliomtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara Dkt Yohana Budeba aliyeketi katikati Ili azungumze na wafanyakazi pia Atoe muelekeo wa Utendaji kazi wa Wizara hiyo Add caption
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt Yohana Budeba Akibadilishana Mawazo na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bibi Tabu Chando ambaye naye alipata fursa ya Kutambulishwa . Amehamia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ametoka  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Bibi Tabu Chando Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu akijitambulisha na kuwasalimia Wafanyakaziwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi 
Katibu Mkuu wa Wzara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt Yohana Budeba akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvihawapo pichani
Wafanyakazi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Wakimnsikiliza kwa Makini Katibu Mkuu wakati akitoa maelekezo na utaratibu wa utendaji kazi wa Wizara Hayupo pichani

Wafanyakazi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Wakimnsikiliza kwa Makini Katibu Mkuu wakati akitoa maelekezo na utaratibu wa utendaji kazi wa Wizara Hayupo pichani 

Msema Chochote wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bw  Deodath Mmanda Afisa Utawala na Rasilimali Watu, akisherehesha Hafla fupi ya Katibu Mkuu Kuzungumza na Wafanyakazi na Kuwapongeza Wana Michezo kwa Ushindi Walioupata
Baadhi ya Wanamichezo walioshiriki katika Michezo ya SHIMIWI Mwaka 2014 Huko Morogoro Wakiwa Mbele ya Meza Kuu kwa Ajili ya Kupongezwa kwa Kikombe na Medali walizowasilisha Wizarani. Aliyeshika Kikombe cha Ushindi wa  Tatu wa Karata ni Bibi Crecencia Lucas
Katibu wa Shimiwi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bibi Mwnamkasi Abassi Akisoma Risala ya Ushiriki wa Wizara kKatika Mashindano ya Shimiwi na Matokeo ya Mashindano hayo Mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Hayupo Pichani
Wanamichezo wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Wakipongezana kuhusu Ushindi wao wWakati wa Shimiwi