Nav bar

Jumanne, 27 Juni 2023

DKT. SAMIA: UCHUMI WA BULUU NI FURSA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema, uchumi wa buluu ni fursa huku akiwataka wananchi  kujipanga na kuweka mazingira muafaka ya  uwekezaji ili waweze kunufaika kupitia rasilimali zinazopatikana katika sekta hiyo.


Dkt. Samia alisema hayo katika  sherehe za Msimu wa Pili wa Tamasha la Vyakula vya Baharini (Zanzibar Sea Food Festival) lililofanyika katika ufukwe wa Kendwa, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar Juni 23, 2023.


Wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Rais, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega  alisema maana halisi ya uchumi wa buluu ni matumizi endelevu ya rasilimali zilizomo kwenye bahari, maziwa na mito kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa, kutengeneza ajira na kuleta ustawi wa maisha ya watu na vilevile kutunza afya ya maumbile ya bahari.


Alisema kupitia tamasha hilo ni muhimu kujizatiti na kujipanga vyema ili kuweza kuzitumia fursa zilizopo na zinazojitokeza katika sekta ya uchumi wa buluu.


Aliongeza kwa kusema kuwa ili fursa hizo ziweze kuwa endelevu ni muhimu kuhakikisha kunakuwa na mipango ya matumizi sahihi ya bahari, usimamizi bora wa ikolojia za bahari, kudhibiti uchafuzi wa bahari, kuimarisha uvuvi wa bahari kuu na kusimamia mnyororo wa thamani wa mazao ya baharini na kuimarisha mifumo ya kitaasisi ya usimamizi bora wa uchumi wa buluu na rasilimali zake.


Alieleza kuwa ni muhimu kuweka kipaumbele kwenye hifadhi ya mazingira ya bahari kwani bila kufanya hivyo hakutakuwa na upatikanaji endelevu wa samaki na mazao mengine ya bahari.


"Hili sio suala la Kitaifa tu, bali la Kikanda na Kimataifa. kama mnavyofahamu pamoja na kwamba mabadiliko ya tabianchi yanaathiri maeneo yote ya nchi, maeneo ya visiwa yapo hatarini zaidi. Hivyo, hatuna budi kulisimamia vyema suala la uhifadhi wa mazingira," alifafanua


Aidha, alibainisha kuwa mipango ya maendeleo ya Kitaifa imeagiza kutekeleza ajenda ya uchumi wa buluu ya Tanzania, kama ilivyoainishwa kwenye Mpango wa (Vision) 2050 kwa Zanzibar na Dira ya Maendeleo ya 2025 kwa Tanzania.




SERIKALI YA DKT. SAMIA YAENDELEA KUWAINUA WAVUVI

Katika hatua za kutekeleza mikakati  ya kujenga na kuboresha uwezo wa wavuvi kufanya kazi zao kwa uhakika na kuimarisha usalama wao, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imegawa kwa wavuvi vifaa vya kujiokolea ili waepukane na matatizo ya kuzama baharini.


Hayo yalifahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akigawa vifaa hivyo kwa wavuvi wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini, Zanzibar Juni 22, 2023.


Wakati  wa hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo, Mhe. Ulega alisema kuwa utekelezaji na ugawaji wa vifaa hivyo kutoka kwa Serikali ni msukumo katika utekelezaji  wa Sera ya Uchumi wa Buluu.


"Vifaa hivi tunavyowakabidhi leo vitawasaidia kuboresha shughuli zenu lakini pia kuwawezesha kufanya uvuvi salama na kujiokoa na kuzama majini," alisema 


Aidha, Mhe. Ulega alitoa wito kwa wavuvi hao kuhakikisha wanahifadhi na kuyatunza mazingira ya Bahari ili kuwa na uvuvi endelevu na kutekeleza wa sera ya uchumi wa buluu.


Katika hafla hiyo, Wavuvi walikabidhiwa Makoti ya kujiokolea Mia moja (100), Gps Nne (4) ambapo vifaa hivyo vitatumiwa na vyombo 25.



UTALII WA BAHARI KUNUFAISHA WAVUVI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema  Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira mazuri kupitia fursa za Utalii wa Bahari ili wavuvi hasa  wadogo waweze kunufaika kwa kuuza samaki na mazao yake.


Waziri Ulega alisema hayo wakati wa tukio la mashindano ya Ngalawa (Ngalawa race) lililofanyika kwenye ufukwe wa Kendwa uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja Juni 22, 2023.


Alisema kuwa kupitia mashindano hayo shughuli za uvuvi zitatangazika duniani na kuvuta watalii wengi na  hivyo wavuvi  watapata fursa nzuri ya  kufanya biashara ya samaki.


Aliongeza kuwa mashindano hayo yanachagiza ujio wa watalii nchini na hivyo kupelekea utalii wa bahari  kushamiri kitendo ambacho kinaongeza fursa ya biashara kwa  wavuvi.


"Tunataka huu utalii wa bahari  uwanufaishe moja kwa moja wavuvi wadogo waweze kupata kipato chao kutokana na mauzo ya samaki na mazao yake kwa watalii hao," alisema


Aidha, Mhe. Ulega aliwashauri wavuvi  kutumia vyema mwambao wa Bahari kwa kuanza kufanya shughuli mbadala za kujiongezea kipato ikiwemo ufugaji wa Kaa, Kambakochi na Majongoo Bahari.


Alisisitiza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwainua wavuvi na ndio maana inafanya kila jitihada za kuboresha shughuli zao ili ziwe na mchango mkubwa na thamani yake ionekane kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.



SERIKALI YA RAIS, DKT. SAMIA YAENDELEA KUWAINUA WAVUVI

Katika hatua za kutekeleza mikakati  ya kujenga na kuboresha uwezo wa wavuvi kufanya kazi zao kwa uhakika na kuimarisha usalama wao, Serikali ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imegawa kwa wavuvi vifaa vya kujiokolea ili waepukane na matatizo ya kuzama baharini.


Hayo yalifahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akigawa vifaa hivyo kwa wavuvi wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini, Zanzibar Juni 22, 2023.


Wakati  wa hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo, Mhe. Ulega alisema kuwa utekelezaji na ugawaji wa vifaa hivyo kutoka kwa Serikali ni msukumo katika utekelezaji  wa Sera ya Uchumi wa Buluu.


"Vifaa hivi tunavyowakabidhi leo vitawasaidia kuboresha shughuli zenu lakini pia kuwawezesha kufanya uvuvi salama na kujiokoa na kuzama majini," alisema 


Aidha, Mhe. Ulega alitoa wito kwa wavuvi hao kuhakikisha wanahifadhi na kuyatunza mazingira ya Bahari ili kuwa na uvuvi endelevu na kutekeleza wa sera ya uchumi wa buluu.


Katika hafla hiyo, Wavuvi walikabidhiwa Makoti ya kujiokolea Mia moja (100), Gps Nne (4) ambapo vifaa hivyo vitatumiwa na vyombo 25.



SERIKALI YA DKT. SAMIA YAENDELEA KUWAINUA WAVUVI

Katika hatua za kutekeleza mikakati  ya kujenga na kuboresha uwezo wa wavuvi kufanya kazi zao kwa uhakika na kuimarisha usalama wao, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imegawa kwa wavuvi vifaa vya kujiokolea ili waepukane na matatizo ya kuzama baharini.


Hayo yalifahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akigawa vifaa hivyo kwa wavuvi wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini, Zanzibar Juni 22, 2023.


Wakati  wa hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo, Mhe. Ulega alisema kuwa utekelezaji na ugawaji wa vifaa hivyo kutoka kwa Serikali ni msukumo katika utekelezaji  wa Sera ya Uchumi wa Buluu.


"Vifaa hivi tunavyowakabidhi leo vitawasaidia kuboresha shughuli zenu lakini pia kuwawezesha kufanya uvuvi salama na kujiokoa na kuzama majini," alisema 


Aidha, Mhe. Ulega alitoa wito kwa wavuvi hao kuhakikisha wanahifadhi na kuyatunza mazingira ya Bahari ili kuwa na uvuvi endelevu na kutekeleza wa sera ya uchumi wa buluu.


Katika hafla hiyo, Wavuvi walikabidhiwa Makoti ya kujiokolea Mia moja (100), Gps Nne (4) ambapo vifaa hivyo vitatumiwa na vyombo 25.





​SERIKALI YAENDELEA KUTEKELEZA MPANGO WA UFUGAJI WA KISASA NA KIBIASHARA – SILINDE

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde amesema serikali inaendelea kutekeleza mpango wa kuhakikisha wafugaji wanafuga kisasa na kibiashara ili kuongeza tija kwa wafugaji na mchango wa Sekta ya Mifugo kwenye pato la taifa.

 

Silinde ameyasema hayo leo (17.06.2023) wakati akifungua mafunzo yenye Kauli Mbiu ya “Youth Bussiness Engangement Through Livestock” kwa vijana wajasiriamali wanaonenepesha mifugo kupitia vituo atamizi, Kampasi ya LITA Kikulula, Karagwe.

 

Katika kufanikisha utekelezaji wa mpango huo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliandaa mwongozo ambao umeainisha majukumu ya wadau mbalimbali walioko katika mnyororo wa thamani wa sekta ya mifugo. Kwa upande wa taasisi za fedha ikiwemo mabenki, Wizara, pamoja na mambo mengine, inawategemea kusaidia kubadilisha fikra na mitazamo ya vijana kuwa ya kibiashara ili kuweza kutengeneza fursa nyingi zaidi za ajira kupitia sekta ya mifugo; pamoja na kuwafundisha namna ya kuandaa mipango biashara kwa ajili ya kuanzisha au kuendeleza biashara zao mara baada ya kumaliza muda wao katika Vituo Atamizi.

 

“Nawapongeza LITA na Benki ya NMB kwa kutumia fursa hii kutoa mafunzo na kuwaandaa vijana wetu kikamilifu kuwa wawekezaji na wafanyabiashara watarajiwa. Kupitia mafunzo haya pia mnaendelea kuwandaa wateja wenu watarajiwa kupitia mikopo yenye riba na masharti nafuu. Naamni ninyi pamoja na wadau wengine mtaendelea kutoa mafunzo kama haya katika vituo vingine ambavyo viko chini ya Wizara yetu,” alisema Silinde

 

 

Silinde amewataka vijana kutokata tamaa kwa kuwa maisha ni mapambano hata pale watakapokutana na changamoto ya aina yoyote wanatakiwa kutafuta njia ya kukabiliana nayo na sio kukata tamaa. Vilevile amewataka vijana waliopata fursa ya kupatiwa mafunzo kuwa mfano katika kuleta taswira na dira mpya katika taifa kupitia Sekta ya Mifugo na Uvuvi.

 

Aidha, amewataka vijana wanufaika wa mpango huo kuwa wavumilivu, wasikivu na wadadisi zaidi ili kuweza kuzijua fursa mbalimbali zinazopatikana katika taasisi za fedha pamoja na asasi nyingine za maendeleo. Vijana wametakiwa kujituma zaidi ili kuweza kufikia ndoto na maono ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuendelea kuongeza kipato na fursa za ajira kwa vijana na wanawake wengi wa hapa nchini.

 

Mtendaji wa Wakala ya Vyuo vya Mifugo (LITA), Dkt. Pius Mwambene amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia LITA na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) imeanza kutekeleza program ya Jenga Kesho iliyobora kwa vijana wetu kupitia miradi ya ufugaji mifugo kibiashara kupitia vituo atamizi nane (8) nchi nzima. Vituo hivi viko katika mkoa wa Tanga, Mwanza na Kagera. Tayari kuna washiriki 240 wamedahiliwa ambapo kila mshiriki atapata fursa ya kunenepesha ng’ombe wasiopungua 40 katika mizunguko minne ndani ya mwaka mmoja. Mzunguko wa kwanza wa unenepeshaji umeanza ambapo ng’ombe wapatao 2,400 wamenunuliwa.

 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mhe. Julius Laizer ameishauri Wizara kuangalia uwezekano wa kutenga asilimia 20 ya maeneo ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kwa ajili ya kutumika na vijana kwa shughuli za ufugaji ili wanapomaliza mafunzo wasihangaike kutafuta ardhi kwa ajili ya kufugia.

 

Mshiriki wa Mafunzo Atamizi katika Kampasi ya LITA Kikulula, Resti Mgonja wakati akisoma risala amesema toka mafunzo hayo yameanza wamefanikiwa kupata elimu ya unenepeshaji kuanzia kwenye ushiriki wa ununuzi wa ng’ombe mnadani ambapo wamenunua ng’ombe 600, wamefanya uogeshaji wa ng’ombe ili kuwakinga na magonjwa, wamefanikiwa kuongeza uzito wa kilo 50 kwa ng’ombe ndani ya siku 90 na kufanikiwa kufyeka maeneo kwa ajili ya malisho takribani ekari 50.




Jumatatu, 26 Juni 2023

WANUFAIKA WA MIKOPO YA UFUGAJI SAMAKI WAPATIWA MAFUNZO

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima amewataka wanufaika wa mikopo ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kuhakikisha wanazingatia mafunzo ya utekelezaji wa miradi hiyo kitaalam ili iweze kuwaletea maendeleo na kuweza  kurejesha mikopo kwa wakati


Mhe. Sima alisema hayo Juni 14 mwaka huu wakati akifungua mafunzo kwa vikundi, vyama vya ushirika na watu binafsi wanaotarajiwa kunufaika na mkopo wa masharti nafuu usio na riba ukijumuisha pembejeo za vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki Mkoani Kagera


Aliseme lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa mikopo hiyo ni kutatua changamoto iliyopo kwa wananchi husasani ukosefu wa mitaji na upungufu wa samaki ziwani.


"Hakikisheni mnazingatia utaalamu katika usimamizi, mbegu bora ya samaki mtakaopandikiza, ulishaji wa samaki kwa kutumia chakula bora, ulinzi wa vizimba na biashara kwa kuzingatia taarifa za soko" alisema Mhe. Sima


Aidha alibainisha kuwa Serikali imeshatenga maeneo yanayofaa kwa ajili ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ambayo ni pamoja na eneo la Rubafu lililounganisha Wilaya ya Bukoba na Missenyi, eneo la Kitua na Ihumbo kisiwa na Bumbire Wilaya ya Muleba 


Alitaja maeneo mengine ni Kabasharo, kabwinyora, Mazinga, Ikuza na Nyakabango yote ya Wilaya ya Muleba  ambapo vibali vyote TAFIRI, NEMC na Mamlaka ya bonde la ziwa Victoria vimeshatolewa


"Tunategemea maeneo haya yatakuwa mfano wa kuigwa katika uzalishaji wa samaki kwa njia ya vizimba, msisitizo umewekwa kuhakikisha kuwa tunafanya ufugaji endelevu na wenye tija kwa maslahi makubwa ya nchi yetu na wananchi kwa ujumla" alisema Mhe. Sima


Aidha aliwakumbusha wakurugenzi na maafisa Ugani katika Sekta ya Uvuvi kuendelea kutekeleza majukumu yao hasa katika kuwasaidia wanufaika wa mikopo kwa kuwatembelea, kuwapa elimu, kuwashauri na kutatua changamoto watakazo kumbana nazo wakati wa upandikizaji wa samaki, ulishaji na masoko ya samaki.




FETA YATAKIWA KUTANUA WIGO WA MASHIRIKIANO KATIKA KUTOA MAFUNZO

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) imetakiwa kuongeza wigo wa mashirikiano katika kutoe elimu ya uvuvi.

 

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh wakati akifunga mafunzo ya siku 30 ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchini Somali, mafunzo ambayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

 

Prof. Sheikh amesema kuwa FETA inatakiwa kuongeza wigo wa mashirikiano na nchi mbalimbali kwani zipo rasilimali nyingi na wataalam wapo wa kutosha hivyo haitakiwi wataalam kujifungia wenyewe badala yake wajitokeze na kuhakikisha wanatoa mafunzo ili kuongeza utaalam kwenye utekelezaji wa shughuli za uvuvi.

 

Vilevile amewasihi kuendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo kwa watu wa ndani na nje ya nchi hasa wanaijishughulisha na shughuli za uvuvi.

 

Wataalam wa uvuvi kutoka Somalia wamekuwa wakishiriki mafunzo hayo hapa nchini kwa lengo la kuongeza uwezo katika kusimamia rasilimali za uvuvi na kuhakikisha kuwa kuna kuwa na uvuvi endelevu nchini kwao.

 

Prof. Sheikh amesema upo umuhimu mkubwa katika kuhakikisha mazao ya bahari yanakuwa na ubora unaotakiwa, hivyo ameitaka FETA kuhakikisha inaendela kuhamasisha na kutoa mafunzo hayo kwa washiriki kutoka nchi mbalimbali.

 

Vilevile amelishukuru Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambapo ameyaomba na mashirika mengine kuiga mfano huo ili kuwezesha mafunzo hayo kuwafikia washiriki wengi zaidi.

 

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Dkt. Semvua Mzighani amesema kuwa mafunzo yanayotolewa chuoni hapo msisitizo mkubwa huwa ni kwenye kufanya mafunzo kwa vitendo hivyo ni matarajio yake kuwa watakaporejea nchini kwao watakwenda kutekeleza yale waliyofundishwa kwa vitendo kitu ambacho kitawaongezea ujuzi zaidi na kusaidia kutoa elimu kwa wengine.

 

Vyuo vya vyao vinatoa mafunzo ya uhandisi katika maji, ubora wa samaki, uvuvi na ubaharia, ukuzaji viumbe maji, mazingira na rasilimali za bahari, sayansi ya bahari na menejimenti ya bahari.

 

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wengine Rais wa wanafunzi hao kutoka chuo cha Uvuvi nchini Somalia bwana Elm A. Mohamed alisema kuwa nchi zetu vyema zikashirikiana katika rasilimali zetu kwani zinafanana hasa ukanda wa bahari pamoja na ufugaji vilevile tushirikiane kati Nyanja za utamaduni kwani utamaduni wa watanzania ni mzuri sana.

 

Mafunzo hayo ya mwezi mmoja yameanza tarehe 12/05/2023 na kumalizika tarehe 13/06/2023 ambapo pamoja na mafunzo washiriki wamepata fursa ya kujifunza Kiswahili na Tamaduni za Kitanzania.



NYAMA YA TANZANIA KUANZA KUUZWA MISRI

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiongea na ujumbe kutoka Misri wakati wa kikao kifupi cha asubuhi "Breakfast Meeting" kilichofanyika jijini Dodoma mapema leo Juni 12, 2023. Ujumbe kutoka nchini Misri uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Taifa ya Huduma za Miradi (NSPO) Meja Jenerali, Hossam Nigeda ( kushoto kwa Mhe. Waziri).


Waziri Ulega alikutana na ujumbe  huo kujadiliana namna ya kuanza kufungua soko la nyama ya Tanzania nchini Misri.


Katika mazungumzo yao, Meja Generali, Nigeda alimueleza Mhe. Ulega kuwa lengo lao ni kuendelea kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili kwa kufungua soko la nyama ya Tanzania nchini Misri.


Aliongeza kuwa wamejipanga kuanzisha machinjio ya kisasa hapa nchini ambayo itawawezesha kusafirisha Tani Mia Sita (600) ya nyama kila Mwezi, pia kusafirisha wanyama hai wakiwemo ng'ombe, Kondoo na Mbuzi Elfu Kumi (10,000) kila Mwezi.


Alifafanua kuwa kwa siku za hivi karibuni wapo katika mipango ya kusafirisha Tani Mia Moja (100) za nyama kabla ya sikukuu ya Eid Al Hajj ili kuanza kutangaza  soko la nyama ya Tanzania nchini humo.


Misri ni miongoni mwa nchi zenye Idadi kubwa ya watu barani Afrika ambapo Idadi ya watu wake hawapungui Milioni 120 hivyo itakuwa fursa nzuri ya kibiashara kwa Tanzania hususan biashara ya nyama.


Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega alimuhakikishia Meja Jenerali Nigeda kuwa Tanzania ipo tayari na watawapa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha biashara hiyo iweze kuanza haraka iwezekanavyo.


Wajumbe wengine waliombatana na Meja Jenerali Nigeda ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji, Islam Attia Abdel Hamid, Mwenyekiti wa Huduma za Mifugo, Misri, Meja Jenerali, Dkt. Ihab Saber Youssef na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masr Trading, Dkt. Hatem Ahmed.


Ziara hiyo ni miongoni mwa jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kufungua milango ya kibiashara nje ya nchi.



Jumapili, 11 Juni 2023

ELIMU YA UANDAAJI NA UHAULISHAJI WA SAMAKI WANAOFUGWA KWENYE VIZIMBA YATOLEWA

 

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bw. Frederick Mussa akitoa elimu ya  uhandaaji na ulishaji wa samaki wanaofugwa kwenye vizimba  wakati wa  mafunzo ya Ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanufaika (hawapo pichani) wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Buchosa,Wilaya ya Sengerema Mkoani  Mwanza, Juni 08,2023.


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya dawati la Sekta binafsi, Mwalimu Ambakisye Simtoe akitoa elimu juu ya ujasiliamali, marejesho ya mikopo na utunzaji wa kumbukumbu  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Buchosa, Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, Juni 08,2023


Afisa Uvuvi  Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Clemence Katunzi  (kushoto) akiwaelekeza kwa  vitendo jinsi ya kutengeneza kizimba wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki   kwenye Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya  Sengerema Mkoani Mwanza  Juni 08,2023.


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Mkomanile Mahundi akitoa elimu juu ya mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu ufugaji wa samaki kwa vizimba  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye Halmashauri ya Buchosa, Wilaya  Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 08, 2023.


Timu ya watoa mafunzo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki   kwenye Halmashauri ya Buchosa, Wilaya ya  Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 08,2023


Mkurugenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya mji wa Bunda, Eng. Emmanuel Mkongo (aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Afisa uvuvi wa Mkoa wa Mara, walipoenda kutembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha walipoenda kutoa mafunzo ya Ufugaji Samaki kwa wanufaika wa mikopo ya riba nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), June 08.2023.


Afisa Uvuvi wa Mji wa Bunda, Bw. Reginald shirima, akiongea na wanufaika wa mikopo ya riba nafuu ya vizimba na pembejeo za ufugaji samaki kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Kwenye mafunzo ya Ufugaji Samaki kwenye vizimba, katika ukumbi wa ofisi za Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mkoani Mara, Juni 08,2023.


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Janeth Rukanda akizungumza kwa nyakati tofauti na baadhi wanavikundi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya za Muheza na Pangani Mkoani Tanga ambao wamefanikiwa kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ambapo amesema wanavikundi hao wameonesha utayari wa kupokea mikopo hiyo na kulima zao la mwani kwa tija. (08.06.2023)


Afisa Uvuvi Ukuzaji Viumbe Maji Tanga Bw. Onesmo Mwanyumba (fulana nyeupe) akiwaelekeza baadhi ya wanavikundi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Muheza na Pangani Mkoani Tanga ambao wamefanikiwa kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), namna ya ufungaji bora wa zao hilo ili lisiharibike au kupotea likiwa baharini (08.06.2023)


Baadhi ya wanavikundi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wakijifunza njia bora ya kufunga zao la mwani ili lisikatike na kupotea likiwa baharini baada ya kupatiwa mafunzo na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufuatia baadhi ya vikundi hivyo kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ambapo wanavikundi 200 wamenufaika na mafunzo hayo katika Mkoa wa Tanga. (08.06.2023)


Afisa Uvuvi Kata ya Pangani Mashariki katika Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Bw. Salim Said Mohamed, akifafanua kwa baadhi ya wanavikundi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani, namna serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilivyoamua kuwekeza kwenye vikundi hivyo ili kuhakikisha zao la mwani linalimwa kwa wingi na kuongeza pato kwa nchi na mwananchi mmoja mmoja kufuatia kukubaliwa kwa ombi la baadhi ya vikundi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). (08.06.2023)


Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Eliakim Mniko  akitoa mafunzo ya Ujasiliamali, Usimamizi wa Biashara na mikopo kwa vyama vya Ushirika ,vikundi,makampuni na watu binafsi  wanaojihusisha na Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Mkoa wa Mwanza ambao wanatarajia kupata mikopo ya riba nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ambapo watapatiwa vizimba na pembejeo za ufugaji samaki. mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, Juni 09,2023.


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bw. Fadhili Ruzika,akitoa elimu ya  uandaaji na ulishaji wa samaki wanaofugwa kwenye vizimba  wakati wa  mafunzo ya Ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanufaika  wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye ukumbi wa Halmashauri Wilaya ya Ukerewe Mkoani  Mwanza, Juni 09,2023.


Afisa Uvuvi wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Titus Kilo, akiongea na wanufaika wa mikopo ya riba nafuu ya vizimba na pembejeo za ufugaji samaki kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Kwenye mafunzo ya Ufugaji Samaki kwenye vizimba, katika ukumbi wa ofisi za Halmashauri ya Wilayaya Ukerewe, Mkoani Mwanza, Juni 09,2023.


Sehemu ya wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba unaotarajiwa kutolewa na Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki  wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na maafisa uvuvi (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya Ufugaji Samaki kwa njia ya vizimba kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya  Ukerewe Mkoani Mwanza, Juni 09,2023.


Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Happy Kapinga akiwapa elimu wakulima wa zao la mwani waliopo Kilwa Masoko mkoani Lindi kuhusu mkopo usio na riba wa pembejeo za zao hilo Juni 09, 2023.


Sehemu ya wakulima wa zao la Mwani waliopo Wilaya ya Kilwa Masoko mkoani Lindi wakisikiliza maelekezo ya mtaalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hayupo) kuhusu mkopo usio na riba wa pembejeo za zao hilo Juni 09, 2023.


Katibu Tawala Mkoa wa Geita Prof. Godius Kanyarara akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) na Mkoa wa Geita mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika ofisini kwake,  lengo likiwa ni pamoja na kueleza nia ya Wizara hiyo kwa kushirikiana  na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) ya kutoa mkopo wenye masharti  nafuu isiyo na riba kwa vikundi, vyama vya ushirika na watu binafsi ikijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki, Mkoani Geita, Juni 09,2023


Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki   kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Geita - Nzera, Mkoani Geita, Juni 09,2023


Timu ya Maafisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakikagua nyavu ambayo itatumika kutengenezea kizimba, wakati walipoenda kuangalia maendeleo ya utengenezaji wa vizimba kwa mmoja wa wazabuni walioshinda tenda ya kusambaza vizimba hivyo kwa wanufaika wa mikopo nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), katika Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu, Juni 10,2023.


Muonekano wa Nyavu ambazo ziko tayari kufungwa kwenye fremu za Vizimba vitakavyosambazwa , kwa  wanufaika wa mikopo nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ambazo zinaendelea kutengenezwa kwa mzabuni kampuni ya KCG AQUATEC aliyeshinda tenda ya kusambaza vizimba hivyo, iliyopo Wilaya ya Busega, Mkoani Simiyu, Juni 10,2023.

JUHUDI ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA KULINDA BAHARI- DKT. MPANGO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema zinahitajika juhudi za pamoja za ndani ya nchi, kikanda na kimataifa katika kuweka mikakati ya kulinda rasilimali za bahari vinginevyo ifikapo mwaka 2050 bahari itakuwa imeelemewa. 

 

Makamu wa Rais alisema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 08 Juni 2023. 


Alisema inapaswa kuwepo kwa uwiano sawia kati ya hali ya bahari na kuimarika kwa uchumi kwani Afya ya Bahari na mifumo imara ya kiikolojia ya baharini ni muhimu kwa uchumi wa buluu ambao ni sehemu ya ajenda ya nchi kufikia maendeleo endelevu.


Dkt. Mpango aliongeza kwamba tafiti zinaonesha kufikia 2030 Bahari itakuwa ndio nguzo kuu ya uchumi duniani ambapo takriban watu milioni 40 watakuwa wameajiriwa moja kwa moja na viwanda vinavyotumia rasilimali za bahari.

 

Aidha, Makamu wa Rais aliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana Wizara ya Mifugo na Uvuvi  na Taasisi za Utafiti wa Bahari kama Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI), Taasisi ya Sayansi za Bahari iliyoko Zanzibar (IMS) kuhakikisha utafiti wa kina unafanyika kwa wingi zaidi ili kuongeza uelewa wa sayansi ya bahari pamoja na athari za changamoto zilizojitokeza kwa jamii na ikolojia.

 

Vilevile Makamu wa Rais amesema upo umuhimu mkubwa wa kuhusisha na kushirikishwa kikamilifu kwa jamii za asili ya pwani katika ulinzi wa rasilimali za bahari kwa kuwa wao ndio wafaidika au waathirika wa kwanza wa mazingira ya bahari. Pia ameagiza Mamlaka zinazohusika na uvuvi na uhifadhi ziongeze jitihada katika kutoa elimu zaidi kwa wavuvi ili washiriki kikamilifu katika uhifadhi wa rasilimali endelevu za bahari na kuondokana na njia zisizofaa za uvuvi.


Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema Wizara hiyo inatoa umuhimu mkubwa katika shughuli za uhifadhi wa rasilimali za bahari na kudhamiria kuilinda bahari na viumbe wake. Ameongeza kwamba ili kuwa na uvuvi endelevu ni lazima kuwa na maeneo ya uhifadhi baharini ambayo yanalenga katika kulinda, kuhifadhi na kudumisha uvuvi endelevu na kukuza mchango wa sekta ya uvuvi na pato la taifa.


Naye, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde alisema kuwa pamoja na changamoto ya matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo imekuwa moja ya kisababishi cha uharibifu wa mazingira ya bahari, yeye pamoja na Waziri Ulega wamedhamiria kuhakikisha kuwa wanaendelea kusimamia  matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari ili ziendelee kuchangia vyema kwenye uchumi wa buluu.


Kauli Mbiu ya Siku ya Bahari Duniani kwa mwaka 2023 ni “Sayari ya Bahari: Mawimbi Yanabadilika” (Planet Ocean: Tides Are Changing)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (kulia) akizindua rasmi Tovuti ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023. Kushoto ni Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini Dkt. Immaculate Sware Semesi na (katikati) ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi, Watumishi, Wadau wa Bahari pamoja na Wananchi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akitoa hotuba fupi wakati akiongea na Viongozi, Watumishi, Wadau wa Bahari pamoja na Wananchi mbalimbali wakati akitoa neno fupi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde akiongea na Viongozi, Watumishi, Wadau wa Bahari pamoja na Wananchi mbalimbali wakati akitoa neno fupi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akiongea wakati akitoa utambulisho wa Viongozi, Watumishi na Wadau mbalimbali wa Bahari kwenye Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Walid Alhad Omar (wa pili kutoka kushoto) na Mchungaji wa Kanisa la Arise and Shine na Boniface Mwamposa (wa tatu kutoka kulia) ni miongoni mwa waalikwa walioshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Bahari yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 8, 2023

Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023

Naibu Katibu Mkuu(Uvuvi), Bi. Agnes Meena (kushoto) akiwa  katika Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023. katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Bw. Stephen Lukanga.

Mhifadhi Bahari, Kitengo cha Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu, Mohamed shamte (kulia) akimueleza jambo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango kuhusu elimu ya uhifadhi wa Bahari kidigitali katika Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023. Kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Kitengo cha Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Prof. Riziki Shemdoe

 SHEKHE WALID, MCHUNGAJI MWAMPOSA MABALOZI UHIFADHI WA BAHARI 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema Wizara yake itawatumia Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Walid Alhad Omar na Mchungaji wa Kanisa la Arise and Shine na Boniface Mwamposa kuwa mabalozi wa uhifadhi wa Bahari ili wasaidiane nao katika kuelimisha jamii hasa zinazoishi kando ya Bahari juu ya athari ya uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira ya Bahari kwa ujumla.


Waziri Ulega alisema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 8, 2023.


Alifafanua kuwa pamoja na uwepo wa Sheria  kwenye usimamizi na uendelevu wa rasilimali za Bahari, ni muhimu pia kushirikiana na jamii katika kuhakikisha mazingira ya Bahari yanahifadhiwa vizuri kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.


Alisema kwa kutambua umuhimu wa kushirikisha jamii wameamua kuwatumia Viongozi hao wa Dini kuwa mabalozi na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kuepuka vitendo ambavyo vinapelekea uharibifu wa mazingira ya Bahari.


"Sisi Wizara na Kitengo chetu cha MPRU tupo tayari kushirikiana na viongozi hawa ili waweze kutusaidia kutoa elimu kwa jamii juu ya athari ya Uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira", alisema


Naye, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde alisema kuwa pamoja na changamoto ya matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo imekuwa moja ya kisababishi cha uharibifu wa mazingira ya bahari, yeye pamoja na Waziri Ulega wamedhamiria kuhakikisha kuwa wanaendelea kusimamia  matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari ili ziendelee kuchangia vyema kwenye uchumi wa buluu.


Kiongozi mwingine wa dini atakayeshiriki kuelimisha jamii ni kutoka Kanisa Katoliki Tanzania, Padri James Ngonyani.


Kauli Mbiu ya Siku ya Bahari Duniani kwa mwaka 2023 ni “Sayari ya Bahari: Mawimbi Yanabadilika”.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini pamoja na wawakilishi wa jamii ya watu wanaoishi jirani na bahari wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam Juni 8, 2023.

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WANUFAIKA WA MIKOPO YA VIZIMBA YAENDELEA NCHINI

 

Mteknolojia wa samaki mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Hamidu Njengite akitoa elimu kuhusu mikopo isiyo na riba ya pembejeo za zao la Mwani kwa wakulima wa zao hilo waliopo kata ya Mchinga mkoani Lindi Juni 08, 2023

Sehemu ya wakulima wa zao la Mwani kutoka kata ya Mchinga mkoani Lindi wakisoma mwongozo wa kilimo cha zao hilo waliopewa na timu ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi  iliyofika hapo Juni 08, 2023 kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu mkopo usio na riba wa pembejeo za zao la Mwani.

Katibu  Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mwanza Bw. Emil Kasagara akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa hao kufika ofisini kwake, kumuelezea juu ya ujio wao wa kuwajengea uwezo wanufaika wa mkopo wa vizimba wenye masharti nafuu na usio na riba katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Buchosa mkoani Mwanza, Juni 07,2023

Picha ya pamoja ya wanavikundi wa "Busumi fishing corporation Society" na Bwai Fisheries, vinavyojishughulisha na Uvuvi katika Halmashauriya ya Musoma Vijijini (DC), wakiwa na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkoa wa Mara, baada ya kupatiwa mafunzo mafupi juu ya Ufugaji wa Vizimba  na namna bora ya kuimarisha vikundi vyao wakati wakisubiri kukamilika kwa taratibu za kupatiwa mkopo usio na riba ambao waliomba kutoka serikalini na kukubaliwa ombi lao. Mkopo utatolewa kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). (07.06.2023)

Afisa Uvuvi mwandamizi Bw. Clemence Katunzi (kulia) akitoa elimu  juu ya mfumo wa M-Kilimo kwa baadhi ya maafisa Uvuvi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 07,2023


Sehemu ya wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba unaotarajiwa kutolewa na Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki  wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na maafisa uvuvi (hawapo pichani) wakati wa kikao kifupi kilichofanyika  kwenye Halmashauri ya Wilaya ya  Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 07,2023

Afisa Uvuvi  Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Clemence Katunzi  akiwaelekeza kwa  vitendo jinsi ya kutengeneza kizimba wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki   kwenye Halmashauri ya Wilaya ya  Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 07,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya dawati la Sekta binafsi, Mwalimu Ambakisye Simtoe akitoa elimu juu ya ujasiliamali, marejesho ya mikopo na utunzaji wa kumbukumbu  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani wa Mwanza, Juni 07,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bw. Fredrick Mussa akitoa elimu ya  uhandaaji na ulishaji wa samaki wanaofugwa kwenye vizimba  wakati wa  mafunzo ya Ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani wa Mwanza, Juni 07,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Mkomanile Mahundi akitoa elimu juu ya mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu ufugaji wa samaki kwa vizimba  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi (hawapo pichani) kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 07,2023

Maafisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Afisa uvuvi Mkoa wa Mara wakiwa kwenye ofisi ya kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Musoma vijijini,Bw. Magange Mwita (wapili kushoto) ikiwa lengo ni kujitambulisha na kutoa dhumuni la kufika kutoa mafunzo katika Wilaya hiyo kwa wanufaika wa mikopo ya vizimba na pembejeo zake, ambapo mikopo hiyo imetoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). tarehe (07.06.2023)

Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Eliakim Mniko  akitoa mafunzo ya Ujasiliamali, Usimamizi wa Biashara na mikopo kwa vyama vya Ushirika ,vikundi,makampuni na watu binafsi (hawapo pichani) wanaojihusisha na Uvuvi katika Halmashauri ya Wiala ya Musoma Vijijini,  Mkoa wa Mara ambao wanatarajia kupata mikopo ya riba nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ambapo watapatiwa vizimba na pembejeo za ufugaji samaki.(07.06.2023)


Wanufaika wa mikopo ya vizimba na pembejeo zake kutoka Halmashauri ya Wilaya Musoma Vijijini wakiuliza maswali kuhusu upatikanaji wa mikopo iliyotolewa na serikali, kwenye mafunzo ya Ufugaji Samaki kwenye vizimba kutoka kwa maafisa uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hawapo pichani). (07.06.2023).