Nav bar

Jumatatu, 30 Oktoba 2017

SERIKALI YATAIFISHA KUNDI LINGINE LA NG'OMBE KUTOKA RWANDA


SERIKALI YATAIFISHA KUNDI LINGINE LA NG’OMBE KUTOKA RWANDA

NA; MWANDISHI MAALUM – KASULU

Kufuatia zoezi linaloendelea la oparesheni kamata mifugo linaloongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, serikali kwa mara nyingine imetaifisha kiasi cha ng’ombe 171 waliokamatwa katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Akiongea katika zoezi hilo Waziri Mpina amesema Wilaya za mipakani mwa Nchi jirani ziko katika tishio kubwa la kuvamiwa na mifugo na kuelekeza mwanasheria wa Wilaya ya Kasulu kuanza kuandaa utaratibu wa mahakama kuzipiga mnada. “Hatua ya kwanza sisi kama Serikali tunataifisha ng’ombe hawa na kufanya utaratibu wa kuzipiga mnada na mwanasheria wetu wa Serikali aanze taratibu ambapo ng’ombe hao tutawapiga mnada kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama No. 17 ya mwaka 2003.” alisema Mpina.

Mpina aliongeza kusema kuwa, ng’ombe hao kwa sasa wataendelea kuwa chini ya Serikali mpaka taratibu zitakapo kamilika, na kuitaka  kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kasulu  kuelendelea kwa kasi kubwa kukamata mifugo katika mapori na kuhakikisha mifugo yote inapatikana.

Sambamba na hilo, Waziri Mpina aliwataka wananchi kujiadhari  na kuondoka katika kununua kesi zisizokuwa za kwao kwa kuikubali mifugo kutoka nje ya nchi kuwa ni ya kwao, kwani ni kujitaftia matatizo na kuisadia serikali katika jitahada hizi za kukamata mifugo inayoingia ndani ya nchi kinyume na taratibu.

 “Kwa hiyo wananchi wawe namba moja kuwafichua watu hao, na wale tunaowabaini  kuwa wanaitikia mifugo toka nje ya nchi kuwa ni mali yao lazima wachukuliwe hatua.” alisisitiza Mpina.

Awali akitoa taarifa ya ng’ombe hao waliokamatwa katika Wilaya hiyo mkuu wa wilaya hiyo Mwanahawa Mrindoko alisema ng’ombe hao ni mali ya  raia wa Rwanda kwani Serikali ya wilaya ilikuwa inawatafuta Raia  wahamiaji haramu  na kuwapata, hivyo sheria itachukua mkondo wake, na aliongeza kwa kusema kuwa kamati ya ulinzi na usalama itaendelea na zoezi la kuwatafuta wafugaji ambao ni wahamiaji haramu.

Akiwa katika wilaya ya Kakonko Waziri Mpina aliagiza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo  kupitia Mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagalla kuanza mara moja zoezi la oparesheni ya kukamata mifugo toka nje ya nchi kwani tarifa za awali zinasema kuwa Wilaya hiyo ilikuwa haijaanza kabisa kutekeleza agizo hilo na ni moja ya Wilaya ya mpakani mwa nchi jirani ya Burundi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, akiangalia Ng’ombe aina ya nyankole waliopo katika kijiji cha Kakere baada ya kutaifishwa na serikali.


Waziri Mpina akiongea na wanahabari hawapo katika picha baada ya zoezi la kutaifisha kundi la ng’ombe waliovamia katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na team ya Wilaya ya Kasulu iliyoshiriki katika zoezi la kukamata ng’ombe aina ya nyankole kutoka Rwanda,  waliovamia katika kijiji cha Kakere, kushoto kwake ni kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Mwanahawa Mrindoko

 Ng’ombe aina ya nyankole kutoka Rwanda, waliotaifishwa na serikali katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu wakisubiri kukamilika kwa taratibu za mahakama kwa ajili ya kupigwa mnada.


MHE WAZIRI LUHAGA MPINA AMETEKETEZA NYAVU ZINAZOTUMIKA KATIKA UVUVI HARAMU ZILIZOKAMATWA MKOANI KIGOMA


WAZIRI MPINA ACHOMA NYAVU KUKOMESHA UVUVI HARAMU

NA MWANDISHI MAALUM KIGOMA

Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa Mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi Milioni thelalini na moja kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi hilo katika serikali hii ya awamu ya tano.

Akiongea mara baada ya kuteketeza nyavu hizo hizo mapema leo, Mpina alionyesha kushangazwa na suala la uvuvi haramu kuwa sugu “kwa nini vita hii haina mwisho? Lazima yawezekana mbinu zinazotumika ni dhaifu ama silaha zinazotumika ni duni, ifike mahala suala hili  liwe historia”. Alisema Mpina.


Akitoa Maelekezo kwa viongozi wa Mikoa ambayo shughuli hizi zinafanyika, Mpina aliwataka viongozi hao wawe na jukumu la kulinda rasilimali za taifa ikiwa ni mapoja na Bahari, Maziwa na mito.

“kama nitashindwa kushughulia suala zima la uvuvi haramu, niitaaachia dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, na mpaka kufikia hatua hiyo lazima wengi watakuwa wamejuruhiwa.” Alisisitiza Mpina.

Akiwa katika ziara ya Oparesheni Maalum ya Ondoa Mifugo kutoka katika mikoa ya mipakani na nchi jirani akiwemo Mkoani kigoma, Mpina Pia alitembea mwalo mpya wa Kibirizi Mjini Kigoma na kumtaka Afisa Mifugo na Uvuvi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kushughulikia changamoto za mitambo wa kugandisha barafu inayokikabili kikundi shirikishi cha rasilimali za uvuvi mwaloni hapo pamoja na suala la kuwauzia dagaa wafanya biashara wanaozisafirisha nje ya nchi. Waziri Mpina Pia alitembelea chuo uvuvi mjini Kigoma.

Zoezi la opareshini ondoa mifugo na kukomesha rasmi uvuvi haramu limeanza rasmi kwa viongozi wa Wizara husika wakiongozwa na mawaziri Luhaga Mpina na Abdalah Ulega kuingia kazini katika mikoa inayokabiliwa na changamoto hizo.

Katika Picha Nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zenye thamani ya shilingi milioni 31 zikiteketea kwa moto kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi la kupambana na uvuvi haramu nchini.


Katika picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwasha moto kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu Mjini Kigoma


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina akimimina mafuta ya taa kabla ya zoezi la kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu mjini Kigoma Nyuma yake ni baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma watumishi wa umma na wanahabari wakishuhudia tukio hilo.


Jumanne, 24 Oktoba 2017

MHE. WAZIRI ALIKUTANA NA WATUMISHI WA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMAIZI WA MAZINGIRA NEMC

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akitia saini katika kitabu cha wageni kwenye Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC  alipoenda kuagana nao na kutoa neno baada ya kufanya nao kazi kama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara Mpya ya Mifugo na Uvuvi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpinaakiwa katika mazungumzo na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC,

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza wakati wa kuagana na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, kulia ni mkaguzi wa Mazingirakanda ya Mashariki Bw. Jafari Chimgege na kushoto ni Dkt. Ruth Rugisha Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Baraza


Picha ya Pamoja Waziri Mpina na baadhi ya watumishi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.


Jumatatu, 23 Oktoba 2017

WAZIRI MPINA NA WAZIRI WA OMAN WAZUNGUMZIA MASUALA YA UWEKEZAJI WA VIWANDA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

                                          NA MWANDISHI MAALUM
Waziri anayeshughlia masuala ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekutana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail na kujadili suala zima la uwekezaji wa viwanda katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi.

Katika Mazungumzo hayo Waziri Mpina amemueleza  Waziri huyo wa uwekezaji wa Oman kuwa Tanzania imekuwa ikizalisha nyama kwa kiasi cha tani 36 kwa siku na imekuwa ikifanya biashara kwa kuuza tani za nyama ambazo hazijakatwa katika nchi za falme za kiarabu ikiwemo Oman. 

Wakati umefika sasa kwa nchi hizi mbili kushirikiana kwa pamoja katika Sekta hii kwa Oman kuwekeza katika Viwanda vya ndani vya nyama kwa kuendeleza viwanda vilivyopo na hata kujenga Viwanda vipya, akitolea mfano ujenzi wa kiwanda cha nyama cha Ruvu ambao umefikia 51% kukamilika.

“Tunataka viwanda vyote vya nyama vya ndani vikidhi mahitaji na kuweza kuuza nyama nje ya nchi”. Alisema Mpina.

Kwa upande wake Waziri Salim Al Ismail alipoelezwa kuhusu viwango na madaraja mbali mbali ya nyama nchini na mmoja wa mtaalam kutoka wizara hiyo, alisema kuwa Oman ipo tayari kuwekeza katika sekta ya viwanda vya nyama na kuisaidia Tanzania kutafuta soko la Marekani kupitia Oman kwani nchi hiyo ya Falme za kiarabu ina cheti  na kibali kilichothibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa cha Marekani.

 “Tunaweza kuchukua nyama kutoka Tanzania na kuingiza Marekani bila kulipa Ushuru, tunapaswa kuwa na vyeti halali ili kuweza kupata soko katika nchi nyingine, Alisema Waziri Ismail.”

Waziri Ismail aliendelea kusema kuwa, Makampuni Binafsi kutoka Oman yapo tayari kufanya biashara katika eneo hili hivyo ni wakati wa Tanzania sasa kuonyesha utayari.
“Hizi bidhaa za nyama ni lazima zitoke kwenu sababu sisi hatuna maji wala majani ya kulisha mifugo kama ngombe, mbuzi na kondoo ambao huchinjwa kwa wingi baada ya Hijja. Alisisitiza.”

Kwa Upande wa Sekta ya Uvuvi Waziri Huyo wa Oman alisema Oman imenunua teknolojia ya kisasa ya uwekezaji katika fukwe ya Bahari kutoka Texas Marekani, Teknolojia inayojulikana kitaalam kama Shrim farming inayoruhusu uzalishaji wa chakula cha samaki wavuliwao katika maji marefu bila kuharibu mazingira.

Alisema Tenkolijia hiyo inaweza kutumika katika uwekezaji wa Fukwe ya bahari ya Hindi akitolea mfano eneo la bagamoyo kwa kuzingatia tathmini ya athari ya mazingira na ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuwasaidia wavuvi wadogo.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dkt Yohana Budeba (Sekta ya Uvuvi) Alisema ni furaha yake kuona wafanya biashara wa Oman wanakuja kuwekeza Tanzania au kushirikiana na wavuvi wa ndani kwani kuna samaki wengi wa kutosha kumudu viwanda vya kuchakata  na kuwezesha biashara kubwa ya samaki.


Katika picha, wa pili kushoto Mhe. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi akizungumzia masuala ya uwekezaji wa viwanda katika sekta ya mifugo wa pili kulia ni Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, akimsikiliza kwa makini. Kulia ni Balozi wa Oman nchini Mhe. Ali Mahroqi, na kushoto ni Katibu Mkuu  sekta ya Uvuvi Dkt. Yohana Budeba.


Kushoto Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, akimtembeza Mhe. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika meli ya Oman baada ya mazungumzo yaliyohusu sekta ya Mifugo na Uvuvi Dar es Salaam juzi.



 Katika Picha Majadiliano kati ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, na wataalam kutoka pande hizo mbili kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kulia akijadili jambo na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Mhe. Salim Al Ismail, baada ya kuuonyeshwa mandhali ya meli ya Oman iliyotia nanga katika bandari ya Dar es Salaam.


Wakiwa katika picha ya Pamoja ,Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, Balozi wa Oman Nchini Mhe. Ali Mahroqi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) Dkt Yohana Budeba na watumishi wa Wizara hiyo baada ya Mawaziri hao kufanya mazungumzo kuhusiana na sekta ya Mifugo na Uvuvi juzi ndani ya meli ya Oman iliyotia nanga katika bandari ya Dar es salaam.