Nav bar

Alhamisi, 24 Novemba 2011

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

          WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI


TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi imepanga kuajiri maafisa walioorodheshwa hapa chini katika mwaka 2011/12 hivyo tunapenda  kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa zilizoainishwa watume barua za maombi ya kazi zifuatazo:

2. Daktari Mifugo Mkufunzi Daraja la II (Veterinary Tutor II) (Nafasi 5)

(a)               Sifa za waombaji

Wawe wamehitimu Shahada ya kwanza  ya Sayansi ya tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali waliosajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo Tanzania

(b)               Majukumu

-                      Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo
-                      Kuandaa mtiririko  wa kila somo (lesson plan) kwa  upande wa nadharia na vitendo.
-                      Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada kwa  upande wa nadharia na vitendo.

·         Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.

·         Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.

·         Kufanya kazi nyingine zote kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

(c)                Mshahara

Mishahara ya watumishi wa Serikali ngazi ya TGS F.

3.Afisa Mifugo daraja la II (Livestock officer II) (Nafasi 128)

Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (kwenye Mashamba ya Uzalishaji Mifugo), Sekretarieti za  Mikoa, na Mamlaka za Mitaa.

(d)               Sifa za waombaji

Waombaji wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi ya Mifugo (Animal Science) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokone au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

(e)                Majukumu
·         Atabuni mipango ya uzalishaji Mifugo Wilayani
·         Ataratibu uzalishaji wa Mifugo katika mashamba makubwa ya Mifugo
·         Atasaidia  kuratibu mipango ya Ugani kuhusiana na Uzalishaji wa Mifugo Wilayani.
·         Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataalam wa mifugo na wafugaji.
·         Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya Masoko ya Mifugo Wilayani kwake na Mkoani.
·         Atabuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo Wilayani.
·         Atafanya  Soroveya  ya rasilimali (resource survey) kwa mfano: mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
·         Ataendesha mafunzo kwa wakala, na wataalamu juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
·         Atatafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali.
·         Atafanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
·         Atashiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibibu  wa malisho.
·         Ataandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
·         Atafuatilia,  kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
·         Atafanya kazi nyingine zinazohusiana  na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

(f)                Mshahara 
Mishahara ya watumishi wa Serikali ngazi ya TGS D.

4.Daktari wa Mifugo daraja II (Veterinary Officer II) (Nafasi 47)

Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi  Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (kwenye vituo vya Uchunguzi wa Afya za Mifugo), Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

(a)               Sifa za waombaji
Wawe wamehitimu shahada ya kwanza ya tiba ya mifugo kutoka chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali na wamesajiliwa na Bodi ya  Madaktari wa Mifugo Tanzania.

(b)               Majukumu
·         Kutoa  huduma za Afya ya Mifugo
·         Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo la sehemu alipo.
·         Kutayarisha  na kusimamia mipango ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
·         Kushiriki katika uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pori katika eneo lake.

(c)                Mshahara
Mishahara ya watumishi wa Serikali ya TGS. F

5.Afisa  Utafiti Mifugo daraja la II (Livestock Research Officer II) (Nafasi 10)

(g)               Sifa za waombaji

Wawe wamehitimu Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
           
(h)               Majukumu
·         Kujifunza  na kumudu mbinu na taratibu za Utafiti wa Mifugo/Ndorobo
·         Kufanya utafiti chini ya usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi.
·         Kuandika  na kuweka kumbukumbu za utafiti
·         Kusaidia  kuendesha Semina na Maonyesho ya Ufugaji bora
·         Kuandaa  mapendekezo ya Utafiti (Research Proposals) kwa kushirikiana na Afisa Utafiti Mifugo anayemsimamia.
·         Kufanya kazi zote kama atakavyoelekezwa na Mkuu wake wa kazi.

(i)                 Mshahara
Mishahara ya watumishi wa Serikali ngazi ya TGRS A

6.Daktari Utafiti Mifugo daraja la II (Veterinary Research Officer) (Nafasi 5)

(j)                 Sifa za waombaji
Wawe wamehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Sayansi ya tiba ya mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya madaktari wa Mifugo Tanzania.

(k)               Majukumu
·         Kujifunza na kumudu mbinu na taratibu za Utafiti wa Afya na Maradhi ya Mifugo.
·         Kuweka kumbukumbu za Utafiti
·         Kusaidia kuendesha Semina na Maonyesho ya Ufugaji bora
·         Kuandaa mapendekezo ya Utafiti (Research Proposals)  kwa kushirikiana na Daktari  Utafiti Mifugo anayemsimamia.
·         Kufanya  utafiti chini ya usimamizi wa Daktari Utafiti Mwandamizi
·         Kukusanya na kuchambua takwimu za Utafiti unaoendelea
·         Kuchapisha taarifa na makala za Utafiti
·         Kufanya kazi nyingine zozote kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

(l)                 Mshahara
Mshahara wa watumishi wa Serikali ngazi ya TGRS C.

MAMBO YA KUZINGATIA

Barua za maombi ziambatane na ‘Curriculum Vitae’ (CV), picha ndogo 2 ukubwa wa pasipoti, cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu elimu ya Sekondari na Shahada.

Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45

Wahitimu walioajiriwa Serikalini hawaruhusiwi  kuomba nafasi hizi kwa sababu tayari wana ajira.

Wahitimu waliotuma maombi yao kabla ya tangazo hili wanashauriwa kutuma maombi upya.

Barua  zote za maombi ziwasilishwe katika muda wa siku 21 kuanzia tarehe ya kwanza ya  kuonekana tangazo hili.

Barua za maombi zitumwe kwa:


Katibu Mkuu,
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,
S.L.P. 9152,
DAR ES SALAAM.