Nav bar

Ijumaa, 4 Mei 2018

WAZIRI LUHAGA MPINA AMEWATAKA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA KUCHINJA PUNDA NCHINI KUPANDISHA BEI


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina  amewataka wawekezaji wa viwanda vya kuchinja Punda nchini kupandisha bei ya kununua wanyama hao badala ya shilingi laki mbili ya sasa kwa punda mmoja ili kudhibiti utoroshaji wa  mifugo  nje ya nchi ambapo inakadiriwa kuwa  zaidi ya  mifugo elfu kumi inatoroshwa  mipakani kwa siku kwenda nje ya nchi inakonunuliwa kwa bei ya juu.

Akizungumza  leo  baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika Kiwanda  cha Punda  cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma  alichokifungua  hivi karibuni, Waziri Mpina alisema bei hiyo  haiendani na gharama halisi ya  ufugaji wa Punda hali
inayowafanya wafugaji kuwatorosha  mifugo na  kulikosesha taifa mapato makubwa.

Alisema ili punda aweze kufikia hatua ya kuchinjwa inachukua kiasi cha miaka  miwili ambapo  gharama zake za ufugaji  zinakuwa  juu ukilinganisha na bei ya shilingi laki mbili anayouzwa  kwa wenye viwanda vya punda nchini.

Aidha alisema kumekuwa  na  utoroshaji  mkubwa wa  mifugo wanaokadiriwa  kufikia takribani 1,614,035 kwa  mwaka  unaofanyika  kwenye mipaka ya nchi yetu ambapo  takribani shilingi bilioni 32.28 zinapotea kama ushuru na takribani  shilingi bilioni 24.21 zinapotea kutokana  na kodi  ya mapato ambayo ingelipwa  kwa nyama ambayo ingeuzwa  hapo nchini.

Aidha Mpina  ameunda  tume ya wataalam kutoka Wizarani  kwa ajili ya kuja kufanya tathmini kama  kiwanda hicho kimetimiza masharti yote yaliyotolewa na Serikali  baada ya kukifungua  Februari mosi mwaka  huu ambapo alisema  ikibainika  kuwa  kiwanda  hakijakidhi masharti yaliyotolewa na Serikali  kitachukuliwa hatua kali zaidi za kisheria ikiwa ni pamoja na kukifungia  kufanya kazi zake.

Aliyataja baadhi ya masharti  yaliyotolewa na Serikali wakati wa kukifunga kiwanda hicho Julai 2017 kuwa ni pamoja na  kuwa na ranchi  za punda, kuboresha kosaafu  za Punda nchini, kuunda na kuingia mikataba na vikundi vya wafugaji wa Punda na kuwa na Punda  wasiopungua mia tatu katika eneo la kuhifadhia mifugo kabla ya kuchinjwa  ili kuwa kuhakikisha kwamba  mifugo wanaangaliwa  kwa  wiki mbili kabla  ya kuchinjwa  ili wawe  katika ubora  wa kimataifa.

Waziri Mpina alisema uwekezaji wa aina hiyo wa kuongeza thamani ya mazao ya mifugo ni moja ya vipaumbele vya wizara yake kwa sasa ili kuchochea kwa kasi kufanikisha azma ya Tanzania ya viwanda.

Aidha aliwahakikishia  wawekezaji wa  kiwanda hicho kuwa endapo watakuwa wamekamilisha masharti atawapa kibali cha kudumu ambapo pia atawaongezea idadi ya kuchinja Punda   kutoka  punda  20 wa sasa ili  vijana  wengi wapate ajira  na kiwanda kiweze kuchangia zaidi katika  mapato ya Serikali.

Mpina aliwahimiza wawekezaji hao kuhakikisha wanawasaidia  wafugaji katika kuongeza uzalishaji, kupambana  na maradhi, upatikanaji wa maji na malisho kwa mifugo.
Alisema idadi ya punda waliopo nchini ni 520,000 tu hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuongeza uzalishaji.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Xun Long Go alimshukuru Waziri Mpina  kwa  kufungua  kiwanda hicho ambapo amesema hadi sasa  kiwanda  kimezalisha  na kuuza  tani 224 za  nyama  ya Punda kwenda nchini China na Vietinam ambapo  pia tani 52 za ngozi ya Punda  ilizalishwa na kuuzwa kuanzi mwezi Februari, 2018.

Alisema kiwanda hicho kimeajiri watanzania 55 ambapo hadi sasa  kina punda 88 katika  maeneo ya Chalinze na Zuzu mkoani Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa  Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Lucia Chacha  aliutaka   uongozi wa kiwanda hicho kwa kubuni mbinu za kuwasaidia  wafugaji kwa kuwapatia elimu bora zaidi ya ufufaji wa punda ili waweze kuwazalisha kwa  wingi zaidi kuliko ilivyo sasa

Hivi sasa Tanzania ina viwanda viwili tu vya kuchinja na kuuza  nyama ya punda ambavyo ni  kiwanda  cha Punda cha Huacheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma na Kiwanda cha Fang Hua kilichopo Shinyanga ambavyo vyote  vimepewa kibali cha kuchinja Punda 20 kwa siku kila kimoja.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani)  akikagua kiwanda cha  kuchinja  Punda  cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma  alichokifungua  hivi karibuni leo. (Picha na Jumanne Mnyau)


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani) akipokea maelezo ya usindikaji wa nyama  Punda  kutoka kwa mfanyakazi wa  wa kiwanda cha  kuchinja  Punda  cha Hua Cheng Limited Elizabeth Peter.(Picha na Jumanne Mnyau)


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani)  akikagua kiwanda cha  kuchinja  Punda  cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma  alichokifungua  hivi karibuni leo. (Picha na Jumanne Mnyau)


WAZIRI MPINA AKABIDHIWA HATI YA KIWANDA CHA NYAMA SHINYANGA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina mwenye (suti miwani) akishuhudia utiaji saini wa hati ya makabidhiano ya Kiwanda cha nyama cha Shinyanga. Hati hiyo zilisainiwa na Mkurugenzi wa Ubinafsishaji  na Ufuatiliaji Jones  Mwalemba(aliyekaa upande wa kushoto)  kutoka Hazina kwa upande wa Serikali na Balozi  Fouad Mustafa (aliyeinama upande wa kulia)  kwa upande wa Kampuni ya Albwardy Investment Group aliyemwakilisha  mmiliki wa Kampuni hiyo bwana Ali Saeed Juma Albwardy.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (aliyekaa mwenye miwani) akishuhudia ubadilishanaji wa hati ya makabidhiano ya Kiwanda cha nyama cha Shinyanga.Kushoto ni Mkurugenzi wa Ubinafsishaji  na Ufuatiliaji Jones  Mwalemba  kutoka Hazina aliyeiwakilisha Serikali na kulia ni Balozi  Fouad