Nav bar

Jumanne, 18 Desemba 2018


MAJIBU YA SERIKALI KUHUSU HOJA ZILIZOIBULIWA NA WAVUVI KUPITIA GAZETI LA NIPASHE  LILILOKUWA NA KICHWA CHA HABARI ‘WAVUVI WATAKA BEI ELEKEZI SANGARA’ LA TAREHE 22 NOVEMBA, 2018
NA.
HOJA
MAJIBU
1.
Kukosekana kwa bei elekezi ya Sangara


Kufuatia malalamiko ya wavuvi kuhusu bei ya Sangara, Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi alishafanyia kazi suala hilo ambapo akiwa Kanda ya Ziwa, alifanya mkutano na wamiliki wa viwanda na bei elekezi ilitolewa kwamba kwa kila kilo moja ya Sangara  bei itakuwa ni Tsh. 5,500/=. Aidha, wadau wa viwanda pia walikiri kwa barua kwamba watatekeleza bei elekezi kama ilivyoamriwa.
2.
Kukandamizwa na kunyanyaswa kwa wavuvi na wanaosimamia sheria
Operesheni zinazoendelea zinatekelezwa kwa mujibu wa Sheria za Nchi zikiwemo:- Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya Mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2009; Sheria ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 1998 na marekebisho yake ya Mwaka 2007; Sheria ya Mazingira Namba 20 ya Mwaka 2004; Sheria ya Uhujumu Uchumi (Economic and organized Crime Act Cap 200 Re 2002 as amended by Act No. 3 of 2016); na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Namba 29 ya Mwaka 1994. Aidha, kutokana na malalamiko ya kunyanyaswa wananchi, wizara inashauri waliotendewa ukatili huo walete taarifa rasmi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
3.
Nyavu stahili hazipatikani
- Serikali imeendelea kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyavu za kuvulia samaki zinazokubalika kisheria. Mpaka sasa kuna viwanda sita (6) vya kutengeneza vyavu ambavyo ni pamoja na CFN na Nafaka, (Mwanza), Sunflag (Arusha), Nyota Venture, Nyamagana Fishing Net na Nashoni Mwita (Dar Es Salaam). Aidha, kuna maduka manne (4) yanayouza nyavu za kuvulia samaki, maduka hayo ni pamoja na Imara Fishnet, Kariakoo Fish net, Mbilinyi Enterprises na Walid Trading yote yapo Dar Es Salaam.
 Katika kuhakikisha kwamba wavuvi wanamudu bei za vifaa vya uvuvi, Serikali inatoa msamaha wa kodi kwa zana za uvuvi na malighafi zake zikiwemo nyuzi za kushonea nyavu (twines) na vifungashio. Aidha, Serikali imeendelea kushauri wavuvi kujiunga katika vikundi ili waweze kukopesheka kwa urahisi  na taasis za fedha kwa ajili ya kupata fedha za kununulia zana za uvuvi zikiwemo nyavu za kuvulia samaki.
- kwa sasa Serikali inatoa vibali vya kuingiza nyavu nchini ili kuziba upungufu ulipo.  Mpaka sasa jumla ya vibali 31vimeshatolewa toka Julai mpaka Novemba,2018 kwa ajili ya kutatua changamoto ya upungufu wa nyavu nchini.
4.
Wavuvi kutozwa Kodi nyingi kama kodi za TRA, Halmashauri, kodi za samaki, mialo na kodi za Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu
Kodi zote wanazopaswa kulipa wavuvi ziko kwa mujibu wa sheria za nchi na hivyo wavuvi wanashauriwa kufuata sheria zilizopo.