Nav bar

Jumamosi, 6 Desemba 2025

RAIS SAMIA ANATAKA TUFANYE MAAMUZI YANAYOTOKANA NA UTAFITI-DKT. BASHIRU

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka viongozi na watendaji wa Serikali yake kufanya maamuzi yanayotokana na matokeo ya utafiti.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo Disemba 05,2025 jijini Dar-es-salaam wakati akizungumza na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) alikofika akiwa pamoja na Naibu Waziri Mhe. Ng’wasi Kamani, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Agnes Meena, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Edwin Mhede na baadhi ya watendaji wa Wizara   ambapo aliwataka wataalam hao kutambua umuhimu wa Taasisi hiyo kwa maslahi ya Taifa.

“Katika umuhimu wa Taasisi hii na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya 6 juu ya kukuza sekta hii ya Uvuvi ili iwe na mchango mkubwa kwenye uchumi wetu, nimetumwa na Mhe. Rais nifanye ziara ya kwanza kwenye kituo hiki ambapo anataka tufanye mambo yanayotokana na ushauri,tusifanye maamuzi kwa mihemko” Amesema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.

Mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye kituo hicho Mhe. Balozi Dkt. Bashiru na viongozi wengine alioambatana nao walielekea kwenye Shirika la Uvuvi nchini (TAFICO).

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) mara baada ya kukagua hatua za ujenzi unaoendelea kwenye Taasisi hiyo kanda ya Dar-es-salaam Disemba 05,2025.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (kulia), Naibu Waziri wake Mhe. Ng’wasi Kamani (katikati) na Mkurugenzi wa Uvuvi nchini Prof. Mohammed Sheikh wakifuatilia michango ya wajumbe kwenye kikao cha baina yao na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) kilichofanyika Disemba 05,2025 jijini Dar-es-salaam.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa pili kutoka kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Edwin Mhede (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi wa Uvuvi nchini Prof. Mohammed Sheikh (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) Dkt. Ismail Kimirei wakielekea inapojengwa maabara mpya ya Taasisi hiyo muda mfupi baada ya Mhe. Balozi Dkt. Bashiru kuwasili makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar-es-salaam Disemba 05,2025.

Kaimu Mkuu wa kituo cha Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kanda ya Dar-es-salaam Dkt. George Rushingisha (kushoto) akimueleza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati) huduma zinazotolewa na kituo hicho muda mfupi baada ya Mhe. Dkt. Bashiru kuwasili hapo Disemba 05,2025 jijini Dar-es-salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (kushoto) alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) Disemba 05,2025 jijini Dar-es-salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Ismail Kimirei.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni