Nav bar

Alhamisi, 4 Desemba 2025

KATIBU MKUU BI. MEENA AZINDUA KIKAO CHA KWANZA CHA USIMAMIZI WA MRADI WA TASFAM

Na Daudi Nyingo Dar Es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes K. Meena, ameongoza kikao cha kwanza cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) kilichofanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika ukumbi wa TVLA ulipo Temeke Dar es salaam. 

Akizungumza mbele ya Mwenyekiti Mwenza, Wakurugenzi, Wataalam wa Sekta ya Uvuvi na wajumbe mbalimbali, Bi. Meena ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar, Mhe. Hussein Ali Mwinyi, kwa kutoa kipaumbele kikubwa kwa sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu.

“Mradi wa TASFAM una thamani ya Dola za Marekani milioni 117, umeandaliwa tangu mwaka 2021 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia, mradi huu utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano (2025–2030) na unalenga kuimarisha mnyororo wa thamani wa uvuvi, kupunguza upotevu wa mazao, kulinda mazingira na kuongeza kipato cha wananchi.” 

“mradi utahusisha Halmashauri 16 za pwani ya Tanzania Bara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, na wanufaika wakuu watakuwa ni wavuvi wadogo, jamii za pembezoni mwa pwani, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.” Alisema Bi Meena

Bi. Meena ameyataja baadhi ya maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya masoko na mialo ya kisasa, kuimarisha kilimo cha mwani, ufugaji wa jongoo bahari na kaa, pamoja na usambazaji wa vyombo vya kisasa vya uvuvi na ununuzi wa meli ya utafiti wa bahari. Zaidi ya vikundi 300 vya wakulima wa mwani na wafugaji wa viumbe baharini vitanufaishwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes K. Meena, akiongoza kikao cha kwanza cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) kipindi cha 2025/2026 kilichofanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika ukumbi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ulipo Temeke, Dar es salaam. Bi. Meena ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kikao hicho.

Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar, Kapt. Hamad B. Hamad (kulia) akichangia mada kwenye kikao cha kwanza cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) kipindi cha 2025/2026 kilichofanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika ukumbi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ulipo Temeke, Dar es salaam. Kapt. Hamad alikuwa Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho. kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes K. Meena

Mratibu wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) Dkt. Nichrous Mlalila akiwasilisha mada kwenye kikao cha kwanza cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) kipindi cha 2025/2026 kilichofanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika ukumbi wa wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ulipo Temeke, Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Mbaraka Kambona akiwasilisha mada kuhusu usanifu wa Nembo ya Mradi kwenye kikao cha kwanza cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) kipindi cha 2025/2026 kilichofanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika ukumbi wa wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ulipo Temeke, Dar es salaam.

Pichani Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes K. Meena (aliekaa kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar Kapt. Hamad B. Hamad (aliekaa kulia) wakiwa kwenye picha na Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) kilichofanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika ukumbi wa wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ulipo Temeke, Dar es salaam.

Pichani Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes K. Meena (aliekaa kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar Kapt. Hamad B. Hamad (aliekaa kulia) wakiwa kwenye picha na kamati tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) kilichofanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika ukumbi wa wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ulipo Temeke, Dar es salaam.

Pichani Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes K. Meena (aliekaa kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar Kapt. Hamad B. Hamad (aliekaa kulia) wakiwa kwenye picha na waratibu wa mradi wa Usimamizi wa Mradi wa Tanzania Scaling-Up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management (TASFAM) kilichofanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika ukumbi wa wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ulipo Temeke, Dar es salaam.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni