◼️YAWATANDIKA TUME YA UTUMISHI MAGOLI 26-21
Timu ya mpira wa Pete kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendeleza wimbi lake la ushindi kwenye michuano ya SHIMIWI 2025 inayoendelea jijini Mwanza baada ya kufanikiwa kuibugiza timu ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa jumla ya magoli 26-21 kwenye mchezo uliochezwa leo Septemba 02,2025 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Katika mchezo huo ambao timu ya Tume ya Utumishi ilianza kwa kufanikiwa kuongoza kipindi cha kwanza iliilazimu timu ya Mifugo na Uvuvi kufanya mabadiliko kadhaa hasa katika eneo la katikati na pembeni ambapo kivutio kikubwa kilikuwa ni kiwango kilichooneshwa na wakongwe wa mchezo huo Rachel Marcelo, Jamila Kalambo na kocha Emmanuela Mawoko waliolazimika kuingia ili kuongeza nguvu na ari ya ushindi.
Timu hiyo itacheza mchezo wake unaofuata Septemba 04,2025 dhidi ya timu ya RAS MWANZA ambapo ikifanikiwa kuibuka na ushindi itakuwa imejihakikishia kucheza hatua ya 16 bora ya michuano hiyo inayotarajiwa kukamilika Septemba 16,2025.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni