Nav bar

Jumatano, 1 Oktoba 2025

MIFUGO NA UVUVI KAMBA WANAUME WATOSHANA NGUVU NA ARDHI

◼️Kamati ya mashindano kuamua hatma ya atakayeongoza kundi lao

Timu ya mchezo wa kuvuta kamba (Wanaume) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoshana nguvu na timu ya Wizara ya Ardhi kwa kila upande kushinda mvuto mmoja katika mchezo uliochezwa leo Septemba 03,2025 kwenye uwanja wa Furahisha ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya SHIMIWI inayoendelea jijini Mwanza.

Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali kutoka kila upande, timu ya Mifugo na Uvuvi ilifanikiwa kushinda mvuto wa kwanza kabla ya timu ya Wizara ya Ardhi kushinda kwenye mvuto wa pili.

Pamoja na timu zote kujihakikishia nafasi ya kucheza 16 bora, matokeo hayo ya leo yamezifanya timu hizo kulingana alama huku zikisubiri maamuzi ya kamati ya mashindano ili kupata timu itakayoongoza kundi hilo hilo.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni