Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika, linalofanyika, jijini Dakar, nchini Senegal, kuanzia Septemba Mosi hadi 5, 2025.
Jukwaa hilo limekutanisha Viongozi kutoka nchi mbalimbali wakiwemo, Marais, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Maafisa waandamizi kutoka sekta za mifumo ya chakula.
Washiriki wengine ni pamoja na Sekta Binafsi, wadau wa Maendeleo, Vijana, Wajasiriamali, wakulima, wafugaji na wavuvi.
Jukwaa hilo limebeba kaulimbiu isemayo "Vijana wa Afrika vinara wa ushirikiano, ubunifu na utekelezaji wa mageuzi ya Mifumo ya Chakula".
Bi. Agnes Meena ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Majadiliano ya mada mbalimbali zikiwemo, ushirikiano wa kikanda na kitaasisi katika utekelezaji wa mpango Jumuishi wa Maendeleo ya Kilimo Afrika (CAADP), vikao maalum vya Mawaziri wa sekta za mifugo Afrika na vikao maalum vya kujadili fursa za uwekezaji kwa nchi ya Tanzania.
Sambamba na hilo Katibu Mkuu amekutana na kufanya vikao na baadhi ya wadau wa Maendeleo (Bilateral Meetings) kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano kando ya mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni