◼️Yawakanda 4-0 huku Valentino kikoti akiondoka na mpira baada ya kufunga magoli yote
◼️TAKUKURU washukuru kutokutana tena na timu hiyo
Timu ya soka ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi imerudi kwenye makali yake baada ya kufanikiwa kuibaruza timu ya RAS DODOMA kwa jumla ya magoli 4 katika mchezo uliopigwa leo Septemba 04,2025 kwenye dimba la Nyamagana ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya SHIMIWI inayoendelea jijini Mwanza.
Timu hiyo ambayo iliingia dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha magoli 2-1 ilichopata kutoka timu ya TAKUKURU jana, ilianza mchezo huo kwa kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa timu ya RAS DODOMA na kama si maamuzi ya kutatanisha ya mwamuzi wa mchezo wa leo huenda idadi ya magoli ingekuwa kubwa zaidi.
Magoli yote katika mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji hatari wa timu ya Mifugo na Uvuvi Valentino kikoti katika dakika ya 22, 28,30 za kipindi cha kwanza kabla ya kuhitimisha kalamu ya magoli hayo dakika ya 28 kipindi cha pili na kumfanya kuondoka na mpira kufuatia “hatrick” hiyo.
Timu hiyo ambayo imekuwa kivutio kwa wapenzi wengi wa soka wanaofuatilia michuano hiyo sasa itamenyana na timu ya RAS Mwanza katika mchezo wao wa mwisho katika hatua ya makundi.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni