Nav bar

Ijumaa, 13 Juni 2025

MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO KIDIJITALI WA UTAMBUZI WA MIFUGO YATOLEWA

Na Chiku Makwai-WMUV SIMIYU

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Abdul Mhinte amefungua mafunzo ya matumizi ya mfumo kidijitali  wa utambuzi wa mifugo kwa Waratibu wa Chanjo na Maafisa Tehama kanda ya ziwa.

Akizungumza na wataalam hao leo Juni 12, 2025 Mkoani Simiyu Bw. Mhinte amesema kuwa lengo la kuwapatia mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa kuhusu matumizi ya mfumo huo wa kidijitali.

Aidha Mhinte amewasisitiza kuwa ni wajibu wa kila mtaalam kutunza vifaa hivyo ili viweze kuwasaidia katika shuguli hiyo mpaka itakapo kamilika.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni