Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea na kufanya ukaguzi wa maandalizi ya Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya mifugo na utambuzi leo, Juni 13, mwaka 2025 katika Viwanja vya nane nane eneo la Nyakabindi wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu.
Mhe. Dkt. Ashatu ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Riziki Shemdoe, Naibu Katibu Mkuu (Mifugo) Bw. Abdul Mhinte na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa wizara hiyo Dkt. Benezeth Lutege.
Katika Ukaguzi huo Waziri Dkt. Kijaji amekagua eneo la uzinduzi wa kampeni ya chanjo, sehemu ya itakayotumika kuwakabidhi vitendea kazi wataalam watakaotekeleza zoezi la Chanjo Kitaifa. Pia ametembelea eneo ambalo litafanyika Kongamano la Wafugaji siku ya Jumapili ya Juni 15, 2025 kabla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo na Utambuzi Kitaifa Juni 16, mwaka 2025 mkoani Simiyu.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni