Nav bar

Alhamisi, 7 Machi 2024

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAVUVI

 



Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga akifungua kikao cha kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wanufaika wa boti na vizimba na hivyo kuzipati utatuzi, Aidha amewasihi wanufaika kutumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa na kurejesha mikopo yao kwa uaminifu,  Februari 24,2024 Mkoani Mwanza.

 

Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe maji Dkt. Nazaeli Madalla akifafanua baadhi ya hoja zilizoibuliwa  na wanufaika wa mkopo wa vizimba usio na riba  wakati wa kikao kifupi cha kusikiliza changamoto mbalimbali za wanufaika hao kilichofanyika  Buchosa Mkoani Mwanza, Februari 24,2024

Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi Ukuzaji Viumbe Maji Baridi, Dkt. Imani Kapinga akujibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa  na baadhi ya wanufaika wa mkopo wa  vizimba usio na riba  (hawapo pichani)  wakati wa kikao kifupi cha kusikiliza na kujibu changamoto  zinazowakabili wanufaika hao kilichofanyika Buchosa  Mkoani Mwanza, Februari 24,2023

Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, (uvuvi) Bw. Anthony Dadu (aliyesimama) akijibu maswali mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa kikao kifupi cha kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wanufaika wa mkopo wa  vizimba na maboti, Februari 24,2024 Mkoani Mwanza

Afisa Maendeleo ya Biashara kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Glacia Marugujo (katikati) akitoa maelezo kwa wanufaika wa mkopo nafuu usio na riba  wa boti na vizima juu ya namna na siku watakayoanza kurejesha  mikopo hiyo Februari 24,2024 Mkoani Mwanza.

Katibu wa kikundi cha Sangara - Nyakaliro Ficos Bw. Revocatus Rugaba akieleza changamoto mbalimbali na kutoa maoni kwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga na watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) (hawapo pichani) wakati wa kikao kifupi cha kujadili changamoto hizo na kuzipatia utatuzi, kikao hicho kimefanyika Buchosa Mkoani Mwanza Februari 24, 2024











Hakuna maoni:

Chapisha Maoni