Nav bar

Alhamisi, 20 Julai 2023

TAASISI ZATAKIWA KUTUMIA VYEMA MAPATO YA NDANI

Na. Edward Kondela


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi ametoa rai kwa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kujijengea uwezo wa kujipatia vyombo vya kazi ili wafanye kazi kwa ufasaha.


Dkt. Mushi amebainisha hayo (10.07.2023) wakati alipokuwa akizindua gari aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 GD STD Manual iliyonunuliwa na Bodi ya Nyama nchini (TMB) kwa thamani ya Shilingi Milioni 99.9.


Akizungumza katika ofisi za bodi hiyo jijini Dodoma amesema ni vyema taasisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa na matumizi mazuri ya fedha kwa kununua vifaa mbalimbali vya kutendea kazi badala ya kufanya matumizi ya fedha yasiyo na tija.


Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Bw. John Chassama amesema gari hilo wamenunua kwa mapato ya ndani ambapo wamepanga kulipeleka Kanda ya Arusha na kwamba mipango ni kuhakikisha kila kanda inakuwa na gari ili kuboresha utendaji kazi.


Bw. Chassama amesema pamoja na ununuzi wa magari mpango wa bodi ni kuimarisha ofisi za kanda kwa kununua vifaa vingine zikiwemo kompyuta ili kusogeza karibu huduma kwa wadau kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi akizindua gari aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 STD Manual mali ya Bodi ya Nyama nchini (TMB) iliyonunuliwa kwa thamani ya Shilingi Milioni 99.9.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi akiwasha gari ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa gari hilo aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 GD STD Manual mali ya Bodi ya Nyama nchini (TMB) na kuzitaka taasisi zilizo chini ya wizara kuwa na matumizi mazuri ya mapato yao. (10.07.2023)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi akiwasha gari ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa gari hilo aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 GD STD Manual mali ya Bodi ya Nyama nchini (TMB) na kuzitaka taasisi zilizo chini ya wizara kuwa na matumizi mazuri ya mapato yao. (10.07.2023)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni