Serikali imedhamiria kukomesha utorishwaji na uingizwaji wa Mifugo na Vyakula vya Mifugo mipakani bila kufuata utaratibu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia Sekta ya Mifugo, Bw. Tixon Nzunda wakati
akifungua kikao kilichojadili hali ya biashara ya mifugo katika mikoa
inayopakana na nchi jirani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara uliopo kwenye
Mji wa Serikali - Mtumba Jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa na Makatibu
Tawala Mikoa kutoka Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Mara, Kagera na Rukwa pamoja na
watendaji wa Sekta ya Mifugo.
Katibu Mkuu Nzunda amesema tatizo
la utoroshwaji na uingizwaji wa mifugo bila kufuata taratibu limekuwa
likiongezeka kitu ambacho kinaikosesha serikali kupata mapato yanayotokana na
biashara ya mifugo. Lakini pia viwanda vya nyama hapa nchini vinakosa malighafi
ya kutosha ili viweze kuchakata nyama kulingana na uwezo wa kiwanda. Vilevile
wananchi wanakosa ajira zinazotokana na mnyororo mzima wa thamani.
Tatizo hili la utoroshwaji na
ungizwaji wa mifugo na vyakula vya mifugo linatokana na baadhi ya viongozi na
watendaji kutotimiza wajibu wao wa usimamizi kwenye maeneo yao.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya
Mifugo kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI imejipanga kuhakikisha tatizo hili
linakomeshwa kwa kuwataka viongozi na watendaji katika maeneo ya mpakani
kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika usimamizi na kuzuia utoroshwaji na
ungizwaji wa mifugo lakini pia wahakikishe wanakusanya maduhuli ya serikali.
Aidha, Katibu Mkuu Nzunda amesema
viongozi na watendaji katika maeneo ya mipakani lazima waendelee kutoa elimu
kwa wafugaji, wafanyabiashara na wananchi katika maeneo yao kuhusu athari za
uturoshwaji na uingizwaji wa mifugo na vyakula vya mifugo ili waweze kuelewa.
Athari hizo ni pamoja na uingizwaji wa magonjwa ya mifugo ambayo pia yanaweza
kuathiri binadamu pamoja na nchi kupoteza mapato ambayo yangetumika kujenga
taifa kiuchumi.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda (katikati) akifungua kikao kilichojadili Hali ya Biashara ya Mifugo katika Mikoa inayopakana na Nchi Jirani ambapo amewasisitiza watendaji katika ngazi zote kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika kuzuia utoroshwaji na ungizwaji wa mifugo bila kufuata utaratibu na kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa maduhuli ya serikali. Kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Mhandisi Enock Nyanda na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (Sekta ya Mifugo), Dkt. Charles Mhina. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Wizara – Mtumba Jijini Dodoma. (21.04.2022)
Mwakilishi wa Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Mhandisi Enock Nyanda (kulia) akisalimia wakati wa kikao kilichojadili hali ya biashara ya mifugo katika mikoa inayopakana na nchi jirani, kikao ambacho kilihudhuriwa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Mara, Kagera na Rukwa pamoja na Viongozi na Wataalam kutoka Sekta ya Mifugo. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Wizara – Mtumba Jijini Dodoma. (21.04.2022)Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (Sekta ya Mifugo), Dkt. Charles Mhina (kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu – Mifugo, Bw. Tixon Nzunda (katikati) kufungua kikao kilichojadili Hali ya biashara ya mifugo katika mikoa inayopakana na nchi jirani. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Wizara – Mtumba Jijini Dodoma. (21.04.2022)Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Mifugo, Prof. Hezron Nonga akiwasilisha taarifa ya udhibiti wa magonjwa mipakani wakati wa kikao kilichojadili Hali ya biashara ya mifugo katika mikoa inayopakana na nchi jirani. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Wizara – Mtumba Jijini Dodoma. (21.04.2022)






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni