Nav bar

Ijumaa, 5 Februari 2021

WAZIRI NDAKI MALORI NA VIFAA VYA MAZIWA MKOANI TANGA

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa vilivyotolewa na shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ambao umechangia Shilingi Bilioni 1.1 kwa ajili ya kununua malori na vifaa hivyo. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya kiwanda cha kusindika maziwa Tanga Fresh jijini Tanga, ambapo amesisitiza ufugaji wa ng'ombe bora wa maziwa ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maziwa nchini. (29.01.2021)

Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Stephen Michael  akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya malori na vifaa vya maziwa vilivyotolewa na shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), iliyofanyika katika viwanja vya kiwanda cha kusindika maziwa Tanga Fresh jijini Tanga, ambapo amesema wizara inaweka jitihada mbalimbali za kuhakikisha upatikanaji wa mbegu za ng'ombe bora wa maziwa nchini. (29.01.2021)

Mkurugenzi wa Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ulio chini ya shirika la kimataifa la Heifer International Bw. Mark Tsoxo akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya malori na vifaa vya maziwa vilivyotolewa na mradi huo kama mchango wake kwenye tasnia ya maziwa nchini ambapo ameshukuru ushirikiano uliopo kati ya serikali na sekta binafsi. (29.01.2021)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi malori manne yaliyotolewa na shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ikiwa ni mchango wake katika tasnia ya maziwa ambapo malori hayo ya kubebea maziwa yametolewa kwa wadau wa tasnia ya maziwa nchini vikiwemo viwanda vitatu vya kuchakata maziwa (ASAS, Kilimanjaro Fresh na Nronga) na Chama Kikuu cha Ushirika wa Wafugaji Mkoa wa Tanga (TDCU). Hafla hiyo fupi imefanyika katika viwanja vya kiwanda cha kuchakata maziwa Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga. (29.01.2021)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiwa kwenye moja ya malori ya kubebea maziwa yaliyotolewa na shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ikiwa ni mchango wake katika tasnia ya maziwa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya kiwanda cha kuchakata maziwa Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga. (29.01.2021)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akimkabidhi Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini Bw. Noel Byamungu moja ya matanki ya kubebea maziwa yaliyotolewa na shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ikiwa ni mchango wake katika tasnia ya maziwa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika viwanja vya kiwanda cha kuchakata maziwa Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga. (29.01.2021)

Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na baadhi ya wadau wa tasnia ya maziwa nchini waliokabidhiwa malori na vifaa vya maziwa na shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika tasnia ya maziwa ambapo hafla hiyo fupi imefanyika katika viwanja vya kiwanda cha kuchakata maziwa Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga. (29.01.2021)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella mara baada ya Waziri Ndaki kufika katika ofisi za mkuu wa mkoa kabla ya kushiriki katika hafla fupi ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa yaliyotolewa na shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ambapo Mhe. Shigella amemuarifu Waziri Ndaki juu ya changamoto ya uwepo wa mitamba ya kutosha Mkoani Tanga kwa ajili ya kuzalisha maziwa mengi. (29.01.2021)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa  kwanza kulia), wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Bodi ya Maziwa na wadau wengine wa sekta ya mifugo wakifuatilia somo la uboreshaji ng'ombe wa maziwa linalotolewa na Meneja wa  shamba la mifugo la Mruwazi lililopo Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga  Bw. William Mgunya muda huu baada ya timu hiyo kufika shambani hapo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa  kwanza kushoto) akipokea maelezo kuhusu aina ya ng'ombe aliowakuta kwenye shamba la mifugo la Mruwazi lililopo Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga yanayotolewa na Meneja wa shamba hilo  Bw. William Mgunya (kushoto kwake) muda huu (30.01.2021) baada ya kufika shambani hapo. Wengine pichani ni baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bodi ya Maziwa na Shirika la kimataifa la Heifer.








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni