Nav bar

Ijumaa, 5 Februari 2021

KATIBU MKUU GABRIEL AKABIDHI MAGARI KWA WAKUU WA VITENGO

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akikabidhiwa funguo za Magari Matatu mapya aina ya Suzuki Ertiga (yaliyonunuliwa na Sekta ya Mifugo) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali Watu (Mifugo), Bi. Josephine Temihango kwa ajili ya matumizi ya kikazi katika Wizara hiyo. Zoezi hilo la makabidhiano limefanyika katika viwanja vya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mji wa Serikali - Mtumba Jijini Dodoma. (02.02.2021).


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti nyeusi) akikabidhi funguo za Magari madogo matatu aina ya Suzuki Ertiga yaliyonunuliwa Sekta ya Mifugo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Manunuzi, Bw. Emmanuel Mayage (picha ya kwanza juu kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bi. Selina Warioba (picha ya pili juu kulia) na picha ya chini ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Rehema Mbulalina. Makabidhiano hayo ya magari yamefanyika katika viwanja vya Wizara hiyo vilivyopo katika Mji wa Serikali - Mtumba, Jijini Dodoma (02.02.2021). Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti nyeusi) akikabidhi funguo za Magari madogo matatu aina ya Suzuki Ertiga yaliyonunuliwa Sekta ya Mifugo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Manunuzi, Bw. Emmanuel Mayage (picha ya kwanza juu kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bi. Selina Warioba (picha ya pili juu kulia) na picha ya chini ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Rehema Mbulalina. Makabidhiano hayo ya magari yamefanyika katika viwanja vya Wizara hiyo vilivyopo katika Mji wa Serikali - Mtumba, Jijini Dodoma (02.02.2021).


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kukabidhi funguo za magari madogo mapya  aina ya Suzuki Ertiga kwa Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano, Ukaguzi wa Ndani na Manunuzi katika viwanja vya Wizara hiyo  vilivyopo kwenye mji wa Serikali - Mtumba, Jijini Dodoma. (02.02.2021).


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kukabidhi funguo za magari madogo mapya  aina ya Suzuki Ertiga kwa Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano, Ukaguzi wa Ndani na Manunuzi katika viwanja vya Wizara hiyo  vilivyopo kwenye mji wa Serikali - Mtumba, Jijini Dodoma. (02.02.2021).


Picha ya pamoja kati ya  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyevaa suti nyeusi katikati) na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kumalizika kwa makabidhiano ya magari katika viwanja vya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mji wa  Serikali Mtumba, Jijini Dodoma. (02.02.2021)

Magari matatu madogo mapya aina ya Suzuki Ertiga yaliyonunuliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo) kwa ajili ya matumizi ya ofisi na kugawiwa kwa kwa vitengo vya Mawasiliano Serikalini, Manunuzi na Ukakaguzi wa ndani. (02.02.2021)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni