Nav bar

Jumanne, 18 Agosti 2020

HABARI PICHA ZA MAONYESHO YA NANENANE KATIKA MIKOA YA , MBEYA, SIMIYU, ARUSHA, , DODOMA TAREHE 04/08/2020

 

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Isabela Chilumba akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kwenye mabanda ya wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maadhimisho ya maonyesho ya nanenane yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya John Mwakangale  tarehe 04.08.2020. 


Afisa uvuvi kutoka kituo cha maendeleo ya ufugaji samaki Ruhila Mkoa wa Ruvuma Justine Ndayeze akitoa maelekezo jinsi ya kutengeneza chakula cha samaki kwa mdau alipotembelea katika maadhimisho ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi(nanenane) Nyanda za juu kusini Mbeya  tarehe 04.08.2020. 

 

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Isabela Chilumba (aliyevaa suti nyeusi) akipata picha ya pamoja na vijana kutoka HEIFER International ambao wanajihusisha na mambo ya teknolojia ya ufugaji na ufugaji bora, alipotembelea katika mabanda ya wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maadhimisho ya maonyesho ya nanenane yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya  tarehe 04.08.2020. 

 

SIMIYU

Afisa Uvuvi, Bw. George Mbena akielezea na kuonesha teknolojia rahisi ya ufugaji samaki kwa wadau waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu  (5/8/2020).

 


Wafugaji kutoka Halmashauri za wilaya za Butiama na Maswa wakihamasisha wafugaji wenzao kupitia vyombo vya habari kutumia teknolojia ya uhimilishaji ng’ombe baada ya wao kufanikiwa kuongeza idadi ya mifugo kutokana na uhimilishaji. Wafugaji hao wametoa wito kwa wafugaji wenzao kutembelea maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu ili kupata huduma hiyo bure.Mkufunzi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA-Nyegezi), Revocatus Charamila (mwenye kofia nyeupe) akitoa maelezo kuhusu mafunzo yanayotolewa na taaisisi hiyo ikiwa ni pamoja kuwaonesha teknolojia rahisi za ufugaji wa samaki kwa wadau waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane kitaifa yanayoendelea mkoani Simiyu  (5/8/2020).

 

ARUSHA

Msambazaji wa madini ya Mifugo kutoka kampuni ya usambazaji wa madini (JOSERA), Bw. Elirehema Laizer akitoa elimu ya madini na umuhimu wa madini kwa mifugo kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (04/08/2020) 

 


Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania, Bw. Imani Sichalwe akipata maelezo kutoka kwa daktari wa mifugo NAIC, Bw. Elibariki Njiku alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha themi Mkoani Arusha (04/08/2020) 

 

Mtaalam wa Sungura kutoka kampuni ya SAORE, Bi. Zaina Ramson akitoa elimu ya ufugaji wa sungura kibiashara kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi jijini Arusha (04/08/2020) 


DODOMA


Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani(WMUV), Dkt. Angello Mwilawa(kushoto) akimuonesha mbegu bora za malisho Mkurugenzi Mtendaji, Kampuni ya Kilimo, Mifugo na Ufugaji wa Samaki Tanzania(TALAS), Yvonne Robben walipokutana katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Mkoani Dodoma Agosti 4, 2020. 


Afisa Mauzo, Kampuni ya Pimak, Ally Pande akitoa maelezo kwa Wadau wa mifugo kuhusu huduma zinazotolewa na kampuni hiyo katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Mkoani Dodoma Agosti 4, 2020. Wa kwanza kulia ni Afisa kutoka Bodi ya Nyama, Irene Nselela. Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania(TALIRI), Neema Urassa(kulia) akitoa maelezo kuhusu ufugaji wa Sungura kwa Wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma Agosti 4, 2020Mkurugenzi, Kampuni ya Kilimo, Mifugo na Ufugaji wa Samaki Tanzani(TALAS), Felix Filangali(kulia) akimsikiliza mdau wa mifugo aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika kwenye Viwanja vya Nzuguni, Mkoani Dodoma Agosti 4, 2020. 


 
Hakuna maoni:

Chapisha Maoni