Nav bar

Jumatatu, 17 Agosti 2020

HABARI PICHA ZA MAONYESHO YA NANENANE KWENYE MIKOA YA SIMIYU, ARUSHA, MOROGORO, MBEYA 03/08/2020

 


Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Jamii na Pembejeo za Mifugo (DVS) Dkt.Stanford Ndibalema akitoa maelezo kuhusu huduma bora za afya za wanyama kwa wadau waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu (3/8/2020).


Mkufunzi kutoka Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Bw. Heriel Mchome akitoa wito kupitia vyombo vya habari kwa wadau kujiunga na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na LITA katika kampasi zake zilizopo mikoa nane nchini, kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu  (3/8/2020).Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Bernard Kibese akihamasisha wafugaji kufika kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kujifunza teknolojia za ufugaji wa kisasa baada ya yeye kuvutiwa na teknolojia hizo ikiwemo mashine ya kuandalia chakula cha mifugo na ufugaji samaki kwenye matanki.Naibu Gavana ametembelea mabanda hayo kwenye maonesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu  (3/8/2020).


ARUSHA

Mtaalam wa Samaki kutoka SoulPeace AquaFish Limited, Bw. Goodluck Benjamin (wa kwanza kulia) akitoa elimu ya namna wanavyopata mayai ya kambale na utunzaji wa kambale hao kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (03/08/2020) 

 


Mchumi Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Sophia Mlote (kushoto) akipata maelezo juu ya ufugaji wa sungura na faida za mkojo wa sungura kutoka kwa mtaalam wa Sungura Bi. Renalda Chami kutoka kampuni ya SAORE kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha themi Mkoani Arusha. (03/08/2020) 

 

Afisa Mifugo kutoka kituo cha huduma za mifugo kanda ya kaskazini (ZVC), Bw. Conrad Ernest Massawe akitoa elimu ya magonjwa ya mifugo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (03/08/2020) Hakuna maoni:

Chapisha Maoni