Nav bar

Alhamisi, 13 Agosti 2020

HABARI PICHA ZA MAONYESHO YA NANENANE KWENYE MIKOA YA SIMIYU, ARUSHA , MOROGORO NA MBEYA TAREHE 02/08/2020

 

SIMIYU

Mkufunzi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA-Nyegezi), Revocatus Charamila (kulia) akitoa maelezo kuhusu mafunzo yanayotolewa na taaisisi hiyo kwa wadau waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane kitaifa yanayoendelea mkoani Simiyu  (2/8/2020).

Afisa Mifugo (DGLF) Bi.Theodata Salema akitoa maelezo kuhusu aina, utengenezaji, utunzaji na matumizi ya vyakula vya Mifugo kwa wadau waliotembelea mabanda ya Wizara na Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima, wafugaji na Uvuvi (nanenane) yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu  (2/8/2020).Mdau wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Hatibu Issa, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (nanenane) kitaifa yanayoendelea mkoani Simiyu  (2/8/2020).


Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt.Nazael Madala (mwenye kofia nyeusi) akimuonesha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu mh.Antony Mavunde (mwenye tai) aina mbalimbali za teknolojoa ya ufugaji samaki alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu (2/8/2020).


MOROGORO


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Uhifadhi- Utalii, TANAPA- Kanda ya Mashariki, Apaikunda Mungure(kushoto anayemuangalia) alipotembelea banda la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika katika Uwanja wa Mwl. Nyerere, Mkoani Morogoro Julai 2, 2020. 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akisaini katika kitabu cha Wageni kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa Mwl. Nyerere Mkoani Morogoro Julai 2, 2020. 

 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akionesha kuvutiwa na Samaki aina ya Kambakochi aliyemshika alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika katika Uwanja wa Mwl. Nyerere Mkoani Morogoro Julai 2, 2020. 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(kushoto) akimsikiliza Msimamizi wa Idara ya Mauzo, Kampuni ya Agricom Afrika, Mathias Lusendamila alipotembelea banda la Kampuni ya Agricom Afrika katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika katika Uwanja wa Mwl. Nyerere, Mkoani Morogoro Julai 2, 2020. ARUSHA


Afisa Mtafiti Mifugo kutoka Wakala ya Maabara ya Vetenari Tanzania (TVLA), Bw. Deogratius Mshanga (kulia) akitoa maelezo kwa mdau kuhusu chanjo za Mifugo zinazotolewa na Maabara hiyo, alipotembelea mabanda  ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (02/08/2020) 

 


Afisa Mifugo kutoka kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) Usariver Arusha, Bw.Abdallah Thabiti ( kulia) akitoa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na kituo hicho kwa wadau waliotembelea mabanda  ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha  (02/08/2020) 


Mkufunzi kutoka LITA Tengeru, Bw. Frank Moshi (kulia) akielezea hatua  za kuandaa ngozi kuanzia zinapotoka machinjioni adi kufikia hatua ya kutengeneza bidhaa kwa watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea katika kiwanja cha Themi Mkoani Arusha  ( 02/08/2020) 


MBEYA


Afisa Mtafiti wa magonjwa ya mifugo Geofrey Thomasi akitoa maelezo kwa mdau jinsi ya upimaji wa magonjwa ya mifugo kimaabara na kumjulisha juu ya uwepo wa chanjo mbalimbali za mifugo kama  chanjo ya kideli,chanjo ya kimeta na chanjo ya Chambavu(BQ) alipotembelea kwenye mabanda ya wizara ya mifugo na uvuvi katika maonyesho ya wakulima, wafugaji na uvuvi (nanenane) viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya  tarehe 02.08.2020. Afisa kutoka bodi ya nyama Ephraim Chawala akitoa maelezo kwa wadau kuhusu matumizi ya vifaa vya kisasa katika uandaaji wa nyama bora na salama walipotembelea kwenye mabanda ya wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya kilimo, Mifugo na uvuvi (nanenane) katika viwanja vya John Mwakangale mkoa wa Mbeya  tarehe 02.08.2020. 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni