Mwenyekiti wa baraza
la Wafanyakazi Sekta ya Mifugo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, amewataka watumishi wa Sekta ya
Mifugo kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona kwa kufuata
maagizo yanayotolewa na wataalamu wa afya huku wakiendelea kuchapa kazi kwa
bidii.
Akizungumza na wajumbe
wa baraza la wafanyakazi kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika
katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Dodoma leo, Prof. Gabriel amesema
'Janga hili ni la kimataifa na kwa vyovyote vile mmesikia katika nchi
mbalimbali."
Amesema "Kwa
niaba ya sekta ya mifugo wafugaji wote wa Ng'ombe zaidi ya milioni 32.5 na
Mbuzi ambao wako zaidi ya milioni 20 na kondoo zaidi ya milion 5.5, kuku zaidi
ya milion 79 kwa kweli tunamshukuru sana Dkt. John Magufuli Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuchukua uamuzi mzito wa kutoipeleka nchi kwenye
kufungiwa watu kukaa nyumbani (Lockdown).
Vilevile, amesema
watumishi wanatakiwa kufanya mambo matatu, ya tahadhari, maombi ba na kuchapa
kazi kwa bidii.
"Baadhi ya watu
pengine hawafahamu, lakini kwenye sekta ya mifugo kuna athari ambayo
tungeipata, sidhani hata kama tungeweza kuziba pengo hilo," Amesema Prof.
Gabriel
"Hata hivyo
kwenye sekta ya mifugo nyama zinazoliwa ni zaidi ya kilo za nyama
2,628,000 maana yake ingefanyika Lockdown na hizo nyama zisingeliwa na maziwa yanayonyweka
ni lita 8,352,000 kwa maana pia maziwa hayo yasingenyweka.
Ameongezea kuwa fursa
kubwa kwa wafugaji kufuga kisasa na kuwa na mifugo yenye tija na mahitaji
yanapotokea ndani ya nchi huko duniani kunawezekana kutumia hiyo kama
fursa ya kuweza kupata mahitaji ya chakula.
Amewaasa pia watumishi
kufanya kazi kwa uadilifu na watumishi wazembe, wavivu na wabadhilifu
hawatakuwa na nafasi katika sekta ya mifugo, akawasihi watumishi kufuata
sheria, taratibu na kanuni za nchi na kuendelea na ushirikiano maana ni jambo
la muhimu sana.
Ameongeza kuwa
watumishi wa sekta ya mifugo wasikubali wafugaji waonewe na kupondwa haki yao
na mtu yoyote na kwa namna yoyote.
Kwa upande wa ufugaji,
wafugaji kote nchini we wametakiwa kufuata sheria, taratibu na kanuni bila
kukosea chochote na bila kujidanganya kwamba kuna watu wa kuwatetea pale
wanapokiuka sheria kwa makusudi.
Katibu Mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi, sekta
ya mifugo katikati akiwa ni Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi Prof, Elisante
Ole Gabriel kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza hilo , mara baada ya
kumaliza kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichifanyika kwenye ukumbi wa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo tarehe 12/05/2020.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni