Nav bar

Jumatano, 5 Agosti 2015

WAZIRI OFISI YA RAIS IKULU MHE. GEORGE MKUCHIKA ATEMBELEA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI KWENYE MAONESHO YA NANENANE 2015 MKOANI LINDI TAREHE 5/08/2015


Waziri Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. George Mkuchika akisaini kitabu cha wageni kwenye Maonesho ya Nanenane 2015 yaliyofanyika Mkoani Lindi

Bw. Edgar Shabani Afisa Utumishi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu akimuelezea Waziri Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. George Mkuchika kuhusu masuala ya Kiutawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu

Wafanyakazi kutoka Shirika la Mitamba Tanzania (Heifer International Tanzania)  wakielezea huduma mbalimbali wanazotoa kwa jamiii


Bi. Joyce Daffa kutoka Idara ya Huduma za Mifugo akitoa maelezo mafupi kwaWaziri Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. George Mkuchika kuhusiana na magonjwa mbalimbali ya Mifugo

Bw. George Mtinda akimuelezea Mhe. George Mkuchika kuhusiana na  Usajili wa Mifugo
Bw. Jeremiah Temu Afisa Masoko Mwandamizi akimuelezea Waziri Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. George Mkuchila Usindikaji wa Nyama na uongezaji wa thamani kwa bidhaa za Nyama zinazotengenezwa na Mjasiriamali 

Waziri Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. George Mkuchika akiangalia tanki la samaki wanaofugwa aina ya Kambale na Sato
Bw. Mashaka Mtaalamu kutoka Wakala wa Elimu na Vyuo vya Mafunzo Tanzania akitoa elimu ya Ufugaji wa samaki kwa Waziri Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. George Mkuchika
Bw. Francis Mmanda Afisa Uvuvi Idara ya Ukuzaji Viumbe Kwenye maji akitoa mafunzo kuhusu Ufugaji Bora wa Samaki 

Wadau wakisikiliza kwa makini mafunzo yanayotolewa na Bw. Francis Mmanda Afisa Uvuvi Idara ya Ukuzaji Viumbe Kwenye maji (hayupo pichani)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni