Nav bar

Alhamisi, 4 Desemba 2025

BI. MEENA AMPONGEZA DKT. MRUTTU KWA KUHITIMISHA SAFARI YAKE YA UTUMISHI

Na. Stanley Brayton, WMUV

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena amempongeza aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Vyakula vya Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Hassan Mruttu kwa kuhitimisha Utumishi wake bora uliotukuka.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga Dkt. Mruttu katika kuhitimisha Utumishi wake, leo Novemba 28, 2025, Jijini Dodoma, Bi. Meena amesema Dkt. Mruttu ni mwalimu mzuri sana, na amekuwa akiwafundisha wengi ili waweze kujifunza na kupata Ujuzi zaidi katika masuala ya Mifugo na lishe.

“ni vyema kuenzi na kufuata ushauri wa kitaalamu ambao Dkt. Mruttu alikuwa anawapatia ili kuleta tija katika Sekta ya Mifugo.” amesema Bi. Meena

Aidha, Bi. Meena amemtakia heri Dkt. Mruttu katika maisha yake mapya nje ya Utumishi wa Umma na kumsisitiza kuwa aendelee kutoa ushauri kwa vijana juu ya ufugaji na kuwataka watumishi wengine wa Wizara hiyo kujifunza kupitia yeye ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa Sekta hiyo ya Mifugo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Utawala, Bw. Samwel Mwashambwa amesema ni furaha sana kuona mtumishi ana hitimisha Utumishi wake akiwa na Afya njema na mwenye furaha.

Vilevile, Bw. Mwashambwa amemuelezea Dkt. Mruttu kama mtu ambaye alikuwa anapenda ukweli na uwazi katika utendaji wake, na kusisisitiza kuwa ni vyema watumishi wengine kuiga mfano wake na kumtumia kama kitabu cha kujifunza katika Utumishi wake.

Naye, aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Vyakula vya Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Hassan Mruttu amemshukuru sana Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na kusema kuwa amefalijika sana kupata ushirikiano wa kutosha toka anapoanza Utumishi na mpaka anapohitimisha Utumishi wake katika Wizara hiyo.

Dkt. Mruttu amesisitiza kuwa ni vyema viongozi na wakurugenzi kujua asili ya watu wanaofanya nao kazi na tabia zao ili iweze kuwasaidia katika utendaji kazi wao.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni