Nav bar

Jumatano, 1 Oktoba 2025

KAMBA WANAUME NA WANAWAKE ZAENDELEZA UBABE SHIMIWI

◼️WANAUME WAFUZU 16 BORA HUKU WAKIPANIA KUONGOZA KUNDI

Timu za mchezo wa kuvuta kamba kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi zimefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo yao ya pili iliyochezwa leo Septemba 02,2025 ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya SHIMIWI inayoendelea jijini Mwanza.

Katika mchezo wa mapema, timu ya kamba (wanaume) ndo ilianza kuwasha taa za ushindi wa leo baada ya kufanikiwa kuivuta timu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa mivuto yote miwili kabla ya timu ya wanawake kuibuka na ushindi wa mvuto 1-0 dhidi ya timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais baada ya kipindi cha kwanza matokeo kuwa suluhu.

Kwa matokeo hayo ya leo timu ya Kamba wanaume imejihakikishia kucheza hatua ya Makundi kwenye michuano hiyo huku timu ya wanawake ikihitajika kushinda kwenye moja ya michezo yao iliyosalia ili kufuzu hatua hiyo.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni