Na. Stanley Brayton, WMUV
Dodoma
Agosti 20, 2025
⬛ Yaingalagaza Wizara ya Viwanda na Biashara goli 3-1 kwenye mchezo wa Mpira wa Miguu
⬛ Kamba Wanaume na Wanawake zatakata kwa Mivuto yote Miwili
Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaibuka kidedea Maandalizi ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) kwa kuichakaza Wizara ya Viwanda na Biashara goli 3-1 kwenye mchezo wa Mpira wa Miguu, mechi ambayo imechezwa katika Viwanja vya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma, leo Agosti 20, 2025.
Ambapo magoli ya upande wa Mifugo na Uvuvi yalifungwa na wachezaji Nkana Eliud, Fred Joseph (kipindi cha kwanza) pamoja na Joseph Onesmo (kipindi cha pili), na goli la kufutia machozi kwa upande wa Viwanda na Biashara lilifungwa na Mchezaji Edward Nkomola (kipindi cha kwanza).
Aidha, Mifugo na Uvuvi imeibuka kidedea mbele ya Viwanda na Biashara kwa kushinda mivutano yote miwili ya kamba kwa upande wa mwanaume na wanawake.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni