Nav bar

Jumatano, 6 Agosti 2025

TUIFANYE TANZANIA KUWA KITOVU CHA CHAKULA AFRIKA - DKT. MPANGO

Na. Omary Mtamike

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewataka viongozi wa sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha chakula katika ukanda wa Afrika.

Mhe. Dkt. Mpango amesema hayo kupitia hotuba yake ya Ufunguzi wa Maonesho ya kimataifa ya Nane Nane aliyoitoa Agosti 1, 2025 kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ambapo amesisitiza Viongozi hao kuwa kinara kwenye utekelezaji wa dira ya Taifa Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025-2050.

“Pamoja na mambo mengine Viongozi tuna wajibu wa kuwaelekeza wakulima, wafugaji na wavuvi wetu kuweka nguvu zaidi kwenye mazao yenye thamani kubwa sokoni” Amesema Mhe. Dkt. Mpango.

Aidha Dkt. Mpango amewataka wafugaji kuwekeza katika uzalishaji wa kisasa wa bidhaa zinazotokana na mifugo ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje, kuendeleza uvuvi na ufugaji wa samaki na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye miundombinu baridi ya uhifadhi na usafirishaji wa mazao wa Mifugo na Uvuvi.

Akitoa taarifa ya Maendeleo ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agness Meena amesema kuwa katika Maonesho ya hayo ya mwaka huu Wizara yake imejikita katika kuonesha teknolojia za kisasa kwenye uzalishaji wa malisho, ufugaji wa samaki, uzalishaji wa mazao ya Mifugo na uchakataji wa mazao ya Mifugo na Uvuvi kwa lengo la kuongeza thamani, kupunguza upotevu na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“Agosti 5 mwaka huu itakuwa ni siku ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho haya ambapo kutakuwa na gwaride la Mifugo na onesho la usimamizi wa rasilimali za Uvuvi kwa kutumia Ndege nyuki lakini pia inaendelea kutoa huduma ya uchanjaji na utambuzi wa Mifugo hapa hapa viwanjani” Ameongeza Bi. Meena.

Mbali na Paredi ya Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeandaa Kijiji cha Protini kilichopo viwanjani hapo kwa lengo la kuhamasisha lishe bora itokanayo na mazao ya Mifugo na Uvuvi.

Mkurugenzi wa Uvuvi nchini Prof. Mohammed Sheikh akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango mambo watakayokutana nayo wadau wa Uvuvi wanaofika kwenye Maonesho ya kimataifa ya NaneNane 2025 muda mfupi baada ya Dkt. Mpango kuwasili kwenye eneo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Agosti 1, 2025 ambako alitembelea Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Shamba la kuzalisha Mifugo la Kitulo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili kwenye eneo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Viwanja vya Maonesho ya kimataifa ya Nane Nane Nzuguni jijini Dodoma Agosti 1, 2025 ambapo alitembelea mabanda ya Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) na Shamba la Uzalishaji wa Mifugo la Kitulo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agness Meena akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango huduma zinazopatikana kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi muda mfupi baada ya Dkt. Mpango kuwasili hapo Agosti 1, 2025 ambako alitembelea Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) nw Shamba la kuzalisha Mifugo la Kitulo.

Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Vyakula vya Wanyama na Maeneo ya Malisho Dkt. Asimwe Rwiguza akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango aina za malisho yanayopatikana kwenye Maonesho ya kimataifa ya NaneNane 2025 muda mfupi baada ya Dkt. Mpango kuwasili kwenye eneo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Agosti 1, 2025 ambako alitembelea Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Shamba la kuzalisha Mifugo la Kitulo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agness Meena akitoa taarifa ya sekta ya Mifugo na Uvuvi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya kimataifa ya Nane Nane kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma Agosti 1, 2025.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni