Na. Stanley Brayton, WMUV
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Ndg. Abdul Mhinte ameihimiza Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) kuendelea kuwatambua na kuwasajili wadau wa Tasnia ya Maziwa ili kuongeza Uzalishaji wa maziwa nchini.
Ndg. Mhinte amesema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa TDB katika Kikao kazi kinachofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Aprili 16, 2025.
"kama wadau wa Tasnia ya Maziwa hawafahamiki na hawajasajiliwa, ni ngumu sana kufikia Malengo na kuzalisha Maziwa kwa wingi, kwani wanahitaji kutatuliwa changamoto zao, ikiwemo za Masoko ya Maziwa hayo" amesema Ndg. Mhinte
Vilevile, Ndg. Mhinte amesema kuwa wadau wa Tasnia ya Maziwa wapo sehemu mbalimbali nchini, na ni vyema Vituo vya ukusanyaji Maziwa vikarekebishwa na kuongezwa, ikiwa pamoja na Usimamizi mzuri ili Maziwa yakusanywe kwa wingi.
Ndg. Mhinte, pia amehimiza Bodi kubuni Miradi mbalimbali kama ya Bar za Maziwa ili kuhakikisha Watumishi wanayapata kiurahisi na kuongeza Pato la Taifa.
Naye, Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Prof. George Msalya amesema kuwa leo wamekuwa na Kikao na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kujadili Maendeleo ya Taasisi yao hususani Maendeleo ya Tasnia ya Maziwa hapa nchini pamoja na utendaji kiujumla.
"tumepokea maagizo yote tuliopewa na Naibu Katibu Mkuu ambayo yatatujenga na kuongeza hali ya utendaji kazi katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku katika Tasnia ya Maziwa" amesema Prof. Msalya
Halikadhalika, Prof. Msalya amesema kwa sasa Maziwa yanakusanywa katika vituo 258 maalum vya kukusanyia, na wataendelea kuongeza vituo vingine pamoja na Miradi mingine kama Bar za Maziwa ili kuhakikisha Maziwa yanapatikana kwa wingi nchini.
Prof. Msalya amebainisha kuwa kwa sasa Takwimu zinaonyesha kila Mtanzania mmoja anatumia takribani Lita 67.5 kwa mwaka, ila viwango vilivyowekwa Kimataifa kwa mtu mmoja kunywa Maziwa kwa mwaka ni Lita 200.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Ndg. Abdul Mhinte, akihutubia Watumishi wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Prof. George Msalya, akizungumza na watumishi wa Bodi hiyo, katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utumishi na Utawala - Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bi. Victoria Masanja, akielezea kuhusu umuhimu wa utoaji Taarifa kwa Utumishi, katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Afisa Matekelezo Mkuu - Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Juma Milinga, akielezea jinsi PSSSF inavyofanya kazi na Taratibu za kuomba Mafao kwa Mtumishi, ni katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Meneja Fedha Utawala na Rasilimali Watu - Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Walter Vasolela, akichangia hoja katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Mchumi - Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Davis Wambura, akifanya mapitio ya Mpango Mkakati wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) ya mwaka 2025/26 na kuelezea Utekelezaji wa Bajeti ya Bodi hiyo kwa Mwaka wa Fedha wa 2024/25, katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Afisa Mteknolojia wa Chakula - Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bi. Neema Moshi, akielezea umuhimu wa Ushirikishwaji wa Idara ya Sheria katika kuwawajibisha wadau wa Maziwa wanaoshindwa kufuata Taratibu za Kisheria katika Tasnia hiyo na umuhimu wa ushirikiano katika utendaji kazi, ni katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Afisa Mteknolojia wa Chakula - Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Francisco Juma, akielezea kuhusu umuhimu wa kubuni vyanzo vya Mapato na kuweka Mikakati mizuri ya Ukusanyaji Mapato katika Bodi na swala la ushirikishwaji wa Watumishi katika kupanga Bajeti kwa kukaa pamoja na kujadili kipi Cha kufanya kwa Mwaka wa Fedha ujao, ni katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Mhasibu - Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Christian Makawa, akielezea umuhimu wa kufungua Kituo cha Taarifa za Maziwa (Information Center) ili wadau wa Tasnia ya Maziwa wapate Habari zinazohusu Maziwa, ni katika Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Picha ni Watumishi wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), wakiwa katika Kikao kazi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Ndg. Abdul Mhinte (aliyesimama katikati mstari wa mbele), akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), baada ya Kikao kazi cha Watumishi wa Bodi hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (Mkapa House), Aprili 16, 2025, Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni