Nav bar

Jumatano, 7 Julai 2021

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA MHE. PROF. JOYCE NDALICHAKO AFANYA ZIARA KWENYE TAASISI YA CHANJO TANZANIA (TVI) KIBAHA, MKOANI PWANI.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akisoma taarifa ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kuhusu miradi ya utafiti inayotekelezwa na Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) Kibaha kwa ufadhili wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH)  wakati wa ziara fupi iliyofanywa na Waziri wa elimu, Sayansi na teknolojia ,Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ili kuona utekelezaji wa miradi hiyo katika Taasisi hiyo iliyopo Kibaha, mkoani Pwani julai 3, 2021.* 

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (katikati) akiongea na viongozi pamoja na watumishi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) wakati wa  ziara fupi  iliyofanyika kwenye ofisi za Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani. Julai 3, 2021* 

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi (kulia) akimtembeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) kwenye majengo ya Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani. Julai 3, 2021* 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akipata maelezo ya namna kazi za uthibiti ubora wa chanjo zinavyofanyika kwa kutumia vifaa na mashine vilivyopatikana kwa ufadhili wa COSTECH  kwenye maabara ya Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani. Julai 3, 2021* 

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi ( wa pili kutoka kulia), viongozi wakuu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja   na watumishi wa Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI), mara baada ya ziara fupi iliyofanyika katika taasisi hiyo iliyopo Wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani. Julai 3, 2021* 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni