Nav bar

Jumamosi, 24 Julai 2021

WAKAGUZI WA NGOZI WAMEASWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUZALISHA NGOZI ZENYE UBORA

Wakaguzi wa Ngozi wameaswa kusimamia Sheria ya biashara ya Ngozi Na.18 ya mwaka 2008 wanapotekeleza majukumu yao na kupata Ngozi inayokidhi viwango vinavyohitajika kwenye viwanda.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko (DPM) Steve Michael wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi Ngozi wa wilaya nane za Mkoa wa Arusha yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za ZVC Arusha 06.07.2021.

"Ni ajabu sana mtalaamu kushindwa kuzijua Sheria maana ndio zinazosaidia kuwaelewesha wachunaji wa Ngozi ni kwa namna gani wachunaji wafanye shughuli za uchunaji na kuweza kupata Ngozi iliyo bora ili kuweza kufika sokoni ikiwa na viwango na kupata bei nzuri kwenye soko". alisema Bw. Michael.

Amesema ili kupata Ngozi iliyo bora na isiyokuwa na madhara, wachunaji Ngozi wanatakiwa kuwa na vitendea kazi sahihi vinavyohitajika, kwa kufuata sheria katika uchunaji.

Aidha, amesema sheria ya biashara ya Ngozi inataka Ngozi iuzwe kulingana na madaraja (grade)
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe Bwana Gabriel Bura aliongeza kuwa wataalamu wana majukumu makubwa sana katika kutekeleza majukumu ya kusimamia masuala ya Ngozi na kuhakikisha inatoka Ngozi yenye viwango bora.

" wataalam wakifuata Sheria watasaidia nchi kupata Ngozi bora zitakazouzwa ndani na nje ya nchi".alisema Bw. Bura.


Kaimu Mkurugenzi wa  uzalishaji na masoko(DPM) Steve Michael akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa Ngozi  wa Wilaya nane za Mkoa wa Arusha, mafunzo hayo yamefanyika katika ofisi za ZVC Arusha. leo 06.07.2021.


Mkufunzi Mkuu kutoka Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) Frank Moshi akitoa mada   kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa Ngozi wa Wilaya nane za  Mkoa wa Arusha, leo tarehe 06.07.2021.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni