Nav bar

Ijumaa, 8 Januari 2021

WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UKAGUZI WA RASILIMALI YA VYAKULA VYA MIFUGO WAPEWA VITAMBULISHO.

Washiriki wa mafunzo ya ukaguzi wa rasilimali ya vyakula vya mifugo kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo ya Afisa Mifugo Mtafiti Mkuu kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Bi. Wende Maulaga (kushoto) wakati akitoa mafunzo hayo kwenye Maabara ya TVLA jijini Dar es salaam. (07/01/2021) 

 

Afisa Mtafiti Mifugo Mwandamizi, kitengo cha Upimaji Ubora na Usalama kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Scholastica Doto akionyesha na kutoa elimu ya namna  mashine ya kupimia madini kwenye vyakula vya mifugo inavyofanya kazi kwa washiriki (hawapo pichani) wa mafunzo ya ukaguzi wa rasilimali ya vyakula vya mifugo walipotembea maabara ya TVLA jijini Dar es salaam. 07/01/2021.* 


Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utambuzi na Huduma za Uchunguzi kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Chanasa Mpelumbe akimvalisha kitambulisho mmoja wa washiriki wa mafunzo ya ukaguzi wa rasilimali ya vyakula vya mifugo kutoka Tanga  Bw. Mustafa Khalifan baada ya kufunga mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika kwenye ukumbi wa TVLA jijini Dar es salaam. 07/01/2021.*


*Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Idara ya Uendelezaji malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Rogers Shengoto akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utambuzi na Huduma za Uchunguzi kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Chanasa Mpelumbe na washiriki wote (hawapo pichani) wa mafunzo ya ukaguzi wa Rasilimali ya Vyakula vya Mifugo wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika kwenye ukumbi wa TVLA jijini Dar es salaam. 07/01/2021* 



 Mkurugenzi wa Utambuzi na Huduma za Uchunguzi kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dr. Chanasa Mpelumbe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam waliotoa mafunzo ya ukaguzi wa Rasilimali ya Vyakula vya Mifugo pamoja na washiriki wa mafunzo  mara baada ya kuwakabidhi vitambulisho na kufunga mafunzo hayo kwenye ukumbi wa TVLA jijini Dar es salaam. 08/01/2021* 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni