* Mkutano umetoa miezi mitatu kwa
kila mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanya
tathmini ya madhara ya ugonjwa wa Covid - 19 katika sekta ya kilimo, mifugo na
uvuvi.
* Mkutano umeweka mikakati ya usalama
wa chakula na lishe katika ukanda wa SADC licha ya changamoto mbalimbali.
* Mkutano umeazimia mikakati ya
kulinda magonjwa yanayovuka mipaka yanayohusu mimea na wanyama na kuathiri
kilimo na mifugo.
* Mikakati imewekwa kutathmini namna
wavuvi wanavyoathirika na ugonjwa wa Covid - 19.
* Mikakati imewekwa kwa shughuli za
uvuvi katika ukuzaji viumbe kwenye maji hususan kwa nchi zizisizokuwa na maji
ya asili (maziwa, bahari na mito).
* Mkutano umeweka mikakati ya nchi
wanachama wa SADC kujilinda na ugonjwa wa covid - 19.
![]() |
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (Mb) ambaye pia Mwenyekiti wa Mawaziri wa Kilimo,
Usalama wa Chakula, Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
(SADC) (kulia), akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.
Elisante Ole Gabriel ambaye ni mwenyekiti wa maafisa waandamizi wa SADC katika
sekta hizo, wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mkutano wa SADC kwa
njia ya video 'video conference' jijini Dar es Salaam. (22.05.2020)
|
![]() |
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina
(Mb) ambaye pia Mwenyekiti wa Mawaziri wa Kilimo, Usalama wa Chakula, Kilimo,
Mifugo na Uvuvi wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) akizungumza na
mawaziri 11 kati ya 16 wakati wa mkutano wa SADC kwa njia ya video 'video
conference' jijini Dar es Salaam. (22.05.2020)
![]() |
Baadhi ya maafisa
waandamizi kutoka Tanzania, wakifuatilia mkutano wa mawaziri wa Kilimo, Usalama
wa Chakula, Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)
kwa njia ya video 'video conference' jijini Dar es Salaam. (22.05.2020)
![]() |
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina
(Mb) ambaye pia Mwenyekiti wa Mawaziri wa Kilimo, Usalama wa Chakula, Kilimo,
Mifugo na Uvuvi wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) akionyesha ishara ya
kuwaaga mawaziri 11 kati ya 16 wa SADC (hawapo pichani) walioshiriki
mkutano wa SADC kwa njia ya video 'video conference'. (22.05.2020)
|
![]() |
Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Luhaga Mpina (Mb) ambaye pia Mwenyekiti wa Mawaziri wa Kilimo, Usalama wa
Chakula, Kilimo, Mifugo na Uvuvi akiwa na baadhi ya maafisa waandamizi kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Kilimo ambao wamehudhuria mkutano
wa SADC kwa njia ya video 'video conference' jijini Dar es Salaam. (22.05.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni